Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mrembo wa Nigeria aliyefutiwa Uraia nchini Afrika Kusini, Chidimma Vanessa Adetshina ameshika nafasi ya tatu Duniani kwenye Miss Universe Pre Arrival Hot Picks.
Soma, Pia: Afrika Kusini yamfutia uraia mrembo wa Nigeria, Chidimma Adetshina pamoja na Mama yake
Chidimma Adetshina, ambaye alikuwa na uraia wa nchi mbili za Afrika Kusini na Nigeria, ameshika nafasi hiyo kwenye orodha ya warembo wanaotarajiwa kufanya vizuri kabla ya mashindano ya Miss Universe kuanza rasmi.
Adetshina alikumbana na changamoto za ubaguzi alipokuwa akijaribu kushiriki katika mashindano ya urembo ya Miss South Africa. Hata hivyo, sasa ataiwakilisha Nigeria katika mashindano ya Miss Universe, akijivunia asili yake na kuleta ushindani mkubwa kwenye jukwaa la kimataifa.