Lilikuwa tukio kubwa sana, ilikuwa 1987 nilishinda pale kwa takriban siku nne hivi ili nipate kushuhudia, lakini nilichofanikiwa ni kumuona dada wa kimakonde ambaye ndiye inasemekana aliweka dawa kwenye maji ya kuoga ya huyo Mtu Chatu inayesemekana alitolewa mlango wa nyuma wa kituo hicho, mahabusu wote WALIRUHUSIWA watu wa Maliasili walimbeba wakaondoka naye,, mambo ya serikali, wakakanusha kwa nguvu zote, si tukio hilo tu jingine lilitokea Mwananyamala A kwenye gesti iitwayo Kajima,,,,siku hizi imebadilishwa jina,,,, inatazamana na CCM Mwinyijuma jirani sana na shemeji yetu Pamela, RiP aliyeimbwa na Msondo, kuna wazinifu kutoka Tandale walinasiana, madereva wa teksi walikataa kuwabeba kuwapeleka hospitali,,,,umbali mfupi tu, ikabidi wabebwe na mkokoteni, hospitali ya Mwananyamala wakati huo ilikuwa na seng'enge tu, mtiti wake ulikuwa siyo wa kawaida!