Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Tembo mwenye thamani ya shilingi milioni 30 katika hifadhi ya taifa ya Serengeti amekufa baada ya kugongwa na gari namba T 388 DUF Toyota Kluger wakati akikatiza kwenda kunywa maji Ziwa Victoria kwenye barabara ya Mwanza kuelekea Musoma wilayani Bunda mkoani Mara.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mara Daniel Shillah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa dereva na mmiliki wa gari hajafahamika na wanaendelea na uchunguzi ikiwamo kumsaka aliyehusika na ajali hiyo.
Aidha, Mkuu wa hifadhi ya taifa Serengeti, Bw. Masana Mwishawa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwataka madereva wa vyombo vya moto kujali na kuzingatia usalama wa wanyamapori kwenye maeneo ya hifadhi.
ITV