Aliyegundua kusoma historia ya marehemu siku ya maziko ana akili nyingi sana

Aliyegundua kusoma historia ya marehemu siku ya maziko ana akili nyingi sana

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Mwaka fulani nikiwa wilaya moja mkoani Iringa nikifanya kazi katika hospitali ya wilaya ya Kilolo katika idara ya TEHAMA.
Nikakutana na chotara wa kihehe na kizungu kwenye korido, wapo wengi sana Iringa sijui walitokea wapi, zile dizaini ya Hanspope.

Binti mdogo wa miaka 21, nikamtongoza akaniuliza umri nikapunguza miaka 10 ili asinione kizee na mwili wangu mdogo akakubali, akauliza kazi nikasema mimi ni daktari bingwa wa wanawake. Nikajifanya niko nae dini moja na dhehebu moja. Nikamwambia niko single kumbe nina mke na watoto wawili nimewaacha mjini.


Lengo langu nipite tu,

Ila shemeji yenu alinipa vitu adimu sana nikajikuta nimenogewa na yeye kanogewa anataka tuishi kama mke na mume.

Ule uongo ukawa kikwazo nikajua ili nimuweke ndani inabidi nimchane ukweli kuhusu mimi.

Nikamfanyia visa tukaachana.

Siku moja nikajiuliza, hivi ningekufa nikiwa nae akagundua ule uongo wangu siku ya mazishi yangu wakati wa kusoma historia ya marehemu ingekuwaje?

Uzuri sijafa mpaka leo bado naboresha historia yangu.

Mtaani kuna familia ilikuwa inadharaulika sana ,ila siku baba yqo alipofariki ikasomwa historia yake mzee kasoma makerere na Oxford watu wote wakaduwaa msibani,walikuwa wanamchukulia poa

R I P Mzee

We danganya kuhusu elimu, umri, marital status ila ukifa ukweli tutaujua, tutengeneze historia zetu sasa.
 
*marehemu amezaliwa mwaka_
*marehemu alikuwa anafanya kazi katika hosptal ya_
*marehemu ameamua kumuacha mke mmoja na watoto_

..zaidi ya yote, marehemu alikuwa mtu mwema sana.
 
Sijawahi sikia wakisema marehemu kafa kwa ngoma
 
Sisi wengine hatuna mambo mengi, tunauliza tu kama Kuna mtu anamdai au anadaiwa na marehemu basi.

Muda wa kuandaa sare, historia , mtu wa makeup, mziki ni kumpotezea muda tu marehemu wa kwenda kwenye nyumba yake ya milele
 
Historia yenyewe hupambwapambwa tu kama ya bibi harusi. Kuna dada alipigwa mimba shuleni wazazi waka comand aolewe. Kwenye historia sasa. Kahitimu mafunzo ya u nurse na kuajiriwa juu wakati hana hata miaka 18 kwenye umri wake nilichoka
 
Waelewa wanaanda historia zao na kuziacha kwa ajili ya editing ndogo ndogo
 
Back
Top Bottom