Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Taarifa kutoka Mbeya ni kuwa kijana Chaula aliyefungwa miaka miwili jela kwa kosa la kuchoma picha ya Rais Samia, na baadaye kuachiwa baada ya kuhangiwa na wananchi amechukuliwa na watu wasiyojulikana toka jana Agosti 1, 2024.
Pia soma: Shadrack Chaula, aliyechoma picha ya Rais Samia aachiwa kutoka Gerezani
Mpaka muda huu hakuna mtu ambae anajua amepelekwa wapi na simu zake zote hazipatikani!
Pia soma: Aliyekamatwa kwa kuchoma picha ya Rais Samia ahukumiwa faini Tsh. Milioni 5 au miaka miwili jela
UPDATE:
Baada ya kusambaa kwa taarifa mitandaoni ikidaiwa kuwa kijana Shadrack Chaula ambaye ni Msanii wa Sanaa ya Uchoraji amepotea katika mazingira ya kutatanisha huku baadhi wakidai amechukuliwa na Watu ambao utambulisho wao haujajulikana, baba mzazi wa Shadrack, mzee Yusuph Chaula amesema ni kweli mwanaye hajulikani alipom Mkoani Mbeya.
Akizungumza na JamiiForums, mzee Yusuph amesema “Hatujui alipo mpaka sasa (Saa mbili Usiku Agosti 2, 2024), majira ya asubuhi nilijulishwa kuna watu ambao bado hatuwajui wamemchukua na kuondoka naye, namba zake hazipatikani tangu wakati huo.”
Ameongeza “Tumeshafika Polisi kutoa taarifa, tunasubiri mrejesho kutoka kwa Polisi, kesho tutafutilia zaidi. Sikuona kama ana tatizo na mtu yeyote tangu yale matatizo ya wakati ule yalipomalizika.”
Alipoulizwa kama naweza kuhusisha kilichotokea na kile kilichomtokea wiki chache zilizopita amesema “Sijui kama kuna uhusiano kwa kuwa, baada ya ile kesi aliendelea kuishi maisha yake ya kawaida.”
Julai 8, 2024, Shadrack Chaula aliachiwa huru kutoka gerezani baada ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 5 ikiwa ni siku chache tangu alipohukumiwa kifungo cha Miaka Miwili jela au kulipa Faini hiyo kwa kosa la kutoa taarifa za uongo Mtandaoni.
Chaula ambaye ni Msanii wa Sanaa ya Uchoraji, Julai 2, 2024 alionekana kupitia kipande cha video akichoma moto picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya, alishindwa kulipa faini na kwenda jela, Wadau mbalimbali walianza kumchangia fedha kupitia Mtandao kwa nia ya kumlipia faini