Aliyehukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kuchoma picha ya Rais amechukuliwa na watu wasiyojulika, mpaka sasa hajulikani alipo

Aliyehukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kuchoma picha ya Rais amechukuliwa na watu wasiyojulika, mpaka sasa hajulikani alipo

Tatizo hata wakipatikana huwa hawasemi wamefanywa nini nakumbuka Roma alikua jasiri hadi akaimba
Leta Defender🎶 leta wajeda🎶 leta wagambo🎶 Roma nimejitoa sadaka🎶
Na mkitaka kuniua hiki kichwa sifii hapa🎶
nichinjeni mkanitupe kwenye daraja la Mkapa🎶

Wakamficha siku mbili alivyoachiwa tu hakusema kafanywa nini akatafuta nauli kimya kimya akakimbilia marekani
 
Halafu mambo kama haya wenye kimbelembele ni vinabo tu ambao hata hawajatumwa na mwenye picha kumtesa kijana wa watu.

Kuna vinuka mbupu havina kazi za kufanya vinajipa majukumu yasiokuwa yao ili tu waonekane wapo kazini na wao.

Chura Kiziwi anaweza kuwa na mapungufu mengi lakini nina hakika hawezi amrisha mateso kwa mtu kwa ajili ya maswala ya kipumbavu kama picha.
 
Wamemficha wa nini wakati alishahukumiwa na akalipa faini? Au Mama Samia hakuridhika na maamuzi ya mahakama?
 
Hii nchi ina mijitu ya ajabu sana. Halafu imepewa dhamana kubwa kwa Taifa.

Kwa vitendo vya hovyo kiasi hiki, hii nchi haitakuja kuwa na upendo kati ya watawala na wananchi.

Huko kwenye nchi za wenzetu, Rais akifanya mambo ya kukera, watu huweza kumrushia kiongozi wa nchi mpaka mayai, lakini Serikali haihangaiki nao. Fikiria tukio kama hilo litokee Tanzania, huyo aliyerusha yai, si watamkatakata vipande vipande!!

Bush akiwa Rais aliwahi kurushiwa kiatu na mwananchi, alikikwepa, halafu akawaambia walinzi wake wasihangaike na huyo aliyerusha hicho kiatu.

Wenzetu wanaangalia tu kama tendo lililofanywa lililenga kumjeruhi au kuonesha tu hisia? Matendo ya kuonesha hisia, hawana muda nayo. Ni yale tu yanayolenga kumjeruhi au kumwua kiongozi, hapo watapambana hasa na huyo mwovu.

Sasa huyo wa kuchoma picha ya Rais, kwani kwa kuichoma hiyo picha, Rais Samia alijeruhiwa mahali popote katika mwili wake? Au kwa kuchomwa picha yake, uhai wake utaondoka?

Ni vizuri Rais Samia akakemea mambo ya kijinga au ya kipuuzi yanayofanywa na vyombo vya dola, ambayo hayana msaada wowote kwa Taifa. Tuna mambo mengi sana ya msingi ambayo vyombo vya dola vinatakiwa kuyafanya kuliko kujihangaisha na petty issues.
 
Kama ndio hivo Bora angebaki magereza tu mtu ukiwa huru shida ukiwa ndan ya neti shida nchi ngumu hii
 
Back
Top Bottom