Aliyehukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kuchoma picha ya Rais amechukuliwa na watu wasiyojulika, mpaka sasa hajulikani alipo

Aliyehukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kuchoma picha ya Rais amechukuliwa na watu wasiyojulika, mpaka sasa hajulikani alipo

Acha wakamnyooshe ili aelewe nini maana ya dola iwe funzo kwa wengine
 
Wakati mwingine ukiwez kujiepusha na matatizo yanayoepukika ni vizuri kujiepusha nayo
Nakazia EPUKA MATATIZO YANAYOEPUKIKA,Watu watakuhurumia LAKINI UMEKWISHA UMIA.
 
Safari ya Demokrasia Africa ni ndefu mno, tutafika tumechoka - bado tuna ka ushamba flani hivi.

Wenzetu hayo yalikuwaga karne ya 14 na 15.
 
Madhara ya kurithisha Nchi ma mutu mashamba.yakikosolewa yanakimbilia kuwatumia polisi kuua
 
Na pengine labda baada ya kutoka jela alionekana bado anajifanya shujaa na kukejeli mamlaka.
Yawezekana hata hao waliomuona akichukuliwa walikuwa wamemchoka... Kwanini?..Kwa sababu wangelimsaidia kijana wao aliye na tabia njema.
Pengine na labda ni lugha ya wajinga
 
Hii nchi ina mijitu ya ajabu sana. Halafu imepewa dhamana kubwa kwa Taifa.

Kwa vitendo vya hovyo kiasi hiki, hii nchi haitakuja kuwa na upendo kati ya watawala na wananchi.

Huko kwenye nchi za wenzetu, Rais akifanya mambo ya kukera, watu huweza kumrushia kiongozi wa nchi mpaka mayai, lakini Serikali haihangaiki nao. Fikiria tukio kama hilo litokee Tanzania, huyo aliyerusha yai, si watamkatakata vipande vipande!!

Bush akiwa Rais aliwahi kurushiwa kiatu na mwananchi, alikikwepa, halafu akawaambia walinzi wake wasihangaike na huyo aliyerusha hicho kiatu.

Wenzetu wanaangalia tu kama tendo lililofanywa lililenga kumjeruhi au kuonesha tu hisia? Matendo ya kuonesha hisia, hawana muda nayo. Ni yale tu yanayolenga kumjeruhi au kumwua kiongozi, hapo watapambana hasa na huyo mwovu.

Sasa huyo wa kuchoma picha ya Rais, kwani kwa kuichoma hiyo picha, Rais Samia alijeruhiwa mahali popote katika mwili wake? Au kwa kuchomwa picha yake, uhai wake utaondoka?

Ni vizuri Rais Samia akakemea mambo ya kijinga au ya kipuuzi yanayofanywa na vyombo vya dola, ambayo hayana msaada wowote kwa Taifa. Tuna mambo mengi sana ya msingi ambayo vyombo vya dola vinatakiwa kuyafanya kuliko kujihangaisha na petty issues.

Sent using Jamii Forums mobile app
Waafrika hasa watanzania wana upumbavu wa milele.
 

Taarifa kutoka Mbeya ni kuwa kijana Chaula aliyefungwa miaka miwili jela kwa kosa la kuchoma picha ya Rais Samia, na baadaye kuachiwa baada ya kuhangiwa na wananchi amechukuliwa na watu wasiyojulikana toka jana Agosti 1, 2024.

Pia soma: Shadrack Chaula, aliyechoma picha ya Rais Samia aachiwa kutoka Gerezani

Mpaka muda huu hakuna mtu ambae anajua amepelekwa wapi na simu zake zote hazipatikani!

Pia soma: Aliyekamatwa kwa kuchoma picha ya Rais Samia ahukumiwa faini Tsh. Milioni 5 au miaka miwili jela

UPDATE:
Baada ya kusambaa kwa taarifa mitandaoni ikidaiwa kuwa kijana Shadrack Chaula ambaye ni Msanii wa Sanaa ya Uchoraji amepotea katika mazingira ya kutatanisha huku baadhi wakidai amechukuliwa na Watu ambao utambulisho wao haujajulikana, baba mzazi wa Shadrack, mzee Yusuph Chaula amesema ni kweli mwanaye hajulikani alipom Mkoani Mbeya.

Akizungumza na JamiiForums, mzee Yusuph amesema “Hatujui alipo mpaka sasa (Saa mbili Usiku Agosti 2, 2024), majira ya asubuhi nilijulishwa kuna watu ambao bado hatuwajui wamemchukua na kuondoka naye, namba zake hazipatikani tangu wakati huo.”

Ameongeza “Tumeshafika Polisi kutoa taarifa, tunasubiri mrejesho kutoka kwa Polisi, kesho tutafutilia zaidi. Sikuona kama ana tatizo na mtu yeyote tangu yale matatizo ya wakati ule yalipomalizika.”

Alipoulizwa kama naweza kuhusisha kilichotokea na kile kilichomtokea wiki chache zilizopita amesema “Sijui kama kuna uhusiano kwa kuwa, baada ya ile kesi aliendelea kuishi maisha yake ya kawaida.”

Julai 8, 2024, Shadrack Chaula aliachiwa huru kutoka gerezani baada ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 5 ikiwa ni siku chache tangu alipohukumiwa kifungo cha Miaka Miwili jela au kulipa Faini hiyo kwa kosa la kutoa taarifa za uongo Mtandaoni.

Chaula ambaye ni Msanii wa Sanaa ya Uchoraji, Julai 2, 2024 alionekana kupitia kipande cha video akichoma moto picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya, alishindwa kulipa faini na kwenda jela, Wadau mbalimbali walianza kumchangia fedha kupitia Mtandao kwa nia ya kumlipia faini
Kumekucha
 
Back
Top Bottom