Aliyeidanganya EFF ya Afrika ya Kusini ndiye anayeidanganya ACT Wazalendo ya Tanzania?

Aliyeidanganya EFF ya Afrika ya Kusini ndiye anayeidanganya ACT Wazalendo ya Tanzania?

Lengo na madhumuni ya ACT wazalendo ni kuhakikisha inaififisha CDM na huo mchongo unatoka serikalini, na ndio maana utaona wanauma na kupuliza, ila nayo ACT itakufa tu kama CUF
vyama dhaifu visivyo na malengo huwa vinavisingizio duni sana vya kukata tamaa kama hivi,dah🐒
 
Hapa Tanzania ACT wako bize kupambana na CHADEMA badala ya kujijenga yenyewe. Mwisho wa siku CHADEMA ama itaongoza nchi au itakuwa chama kikuu Cha upinzani wakati huo ACT itakuwa haina nguvu za kisiasa Zanzibar.
Vinakuaga vi chama vya kimkakati
 
Julius Malema wakati wa harakati zake za kisiasa na wakati wa Kampeni za mwaka huu, alijiegemeza Sana kwenye kukishambulia chama cha siasa cha pili kwa ukubwa nchini Afrika ya Kusini.

Malema alikuwa anaonesha kuwa tatizo la Afrika ya kusini ni "wazungu" wanaobebwa na ANC kuwepo kwake madarakani.

Akajenga hoja kuwa ili Afrika ya Kusini ikombolewe kiuchumi na kijamii, ni lazima kwanza ANC itoke madarakani ili chama chake cha Economic Freedom Fighters (EFF) kiweze kupambana na wazungu kikiwa madarakani.

Ghafla aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma, akaunda chama na kukipa jina la uMkhonto we Sizwe (MK) ambacho kina mfanano kifalsafa na kisera na ANC isipokuwa kwenye sera ya utaifishaji migodi ya dhahabu na Platinum.

EFF ikapoteza uungwaji mkono na MK ikachukua zaidi ya Viti 58 huku Democratic Alliance (DA) iliyokuwa inapigwa vita na EFF ikijiongezea Viti 5 na EFF yenyewe ikipoteza Viti 5 vya ubunge.

Leo hii DA iliyokuwa inashambuliwa na EFF ndiyo Iko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuunda serikali ya mseto na ANC kuliko ilivyo Kwa EFF ya Julius Malema.

Hapa Tanzania ACT wako bize kupambana na CHADEMA badala ya kujijenga yenyewe. Mwisho wa siku CHADEMA ama itaongoza nchi au itakuwa chama kikuu Cha upinzani wakati huo ACT itakuwa haina nguvu za kisiasa Zanzibar.
Kumbe nimesoma upuuzi, najilaumu
 
N
Zitto ni mmojawapo wa wanasiasa niliokuwa nawaona wako makini sana nchi hii, sijui nani alimdanganya kujianzishia hicho kijiwe cha ACT, chama kipo Zanzibar tu halafu mafaniko makubwa wanayojisifia nayo ni kumiliki ofisi na kuchambua sera!
Ndiyo maana tunakiita CCM B kutokana na miendeno yake. Yaani kama Zito mjanja mjanja mpaka kapoteza umaarufu Kwa ajili ya kutumika.
 
Vyama vyote vikubwa Africa Kusini vinaheshimu haki za mashoga na ndoa za jinsia moja zilipitishwa na utawala wa ANC chini ya Thabo Mbeki.
Pia Africa Kusini ushoga sio kipaumbele kwao ni jambo petty mno kuliko uhalifu, rushwa, matatizo ya umeme na ukosefu wa ajira.
Hatukuona vyama vingine vikiandamana kwenda ubalozi wa Uganda kuterea ushoga isipokuwa EFF
Kama una taarifa viliandamana tufahamishe.
 
Kuongea tu bila maneno machafu hamuwezi,
Tukiwapa nchi si mtawafundisha matusi watoto zetu..??
Watoto wenu wanatoka majumbani mwenu tayari wanayajua.Angalia wakipewa mitihani wanaandika nini na kurudi majumbani mwenu!
 
Back
Top Bottom