Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Ryan Wesley Routh: Picha na Reuters.
Shirika la upelelezi la FBI laendelea na uchunguzi wa jaribio la kumuua mgombea wa kiti cha uraisi wa Marekani bwana Donald Trump katika viwanja vya mchezo wa golf vya Trump internation Golf Course.
Mtu aliejaribu kumuua bwana Trump ametambuliwa kwa jina la Ryan Wesley Routh mwenye umri wa miaka 58.
Taarifa zaidi zinomhusu mtu huyo ikiwemo historia yake zasema kuwa Ryan amepigana vita vya Ukraine na amekuwa mara kwa mara akienda na kurudi nchini Marekani kutafuta wapiganaji wa kwenda kushiriki vita hivyo.
Ryan pia ni mhandisi wa kazi mbalimbali za kiufundi au General Contractor na ni mwanachama wa chama cha Democrat. Amewahi kuliambia gazeti la New York Times kuwa mwaka 2023 alikwenda nchini Ukraine kupigana vita na pia BBC wameripoti kwamba aliweza kusajili wapiganaji kutoka Afghanstan ambao walikuwa wakikimbia utawala wa Taliban.
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa jimbo la Palm Beach bwana Dave Aronberg, Ryan alikuwa amejilaza mahali hapo akisubiri muda ufike amlenge risasi Donald Trump.
Ryna aligunduliwa kuwepo kwenye eneo hilo la michezo na afisa wa idara ya usalama wa viongozi ya Secret Service akijaribu kumlenga shabaha afisa huyo na afisa mwingine akamrushia risasi Ryan ambae alianza kukimbia kuelekea vichakani huku akidondosha bunduki ya aina ya AK-47.
Soma pia: Risasi zarindima katika eneo la karibu alipokuwepo Donald Trump, Maafisa usalama wanasema yupo salama
Raia mwema aliweza kumuelezea Ryna wajihi (description) yake, muinekano wake, amevaaje na amebeba nini na kwamba alikwenda kuingia katika gari yake aina ya Nissan SUV.
Taarifa ya mwananchi huyo iliwawezesha polisi kuingiza namba ya gari hilo katika mfumo uitwao "Real-Time Crime Surveillance" mfumo wa kuwawezesha polisi kuwasiliana popote walipo kuhusu gari inotiliwa mashaka au kushiriki shughuli za uhalifu.
Polisi wasema hawakutaka kumfanya Ryan astuke kwa kuona polisi lakini polisi kwa kuwa walikuwa wakiwasiliana sehemu zote waliweza kukusanyika na kwa pamoja wakaweza kulisimamisha gari ya Ryan na kumweka chini ya ulinzi.
Ryan alikubaliana na kusimamishwa kwake na polisi na tangia hapo amekuwa akitoa ushirikiano na maafisa wa FBI ili kuwapa maelezo yoye yanohusu mpango wake. Ndani ya gari yake Ryna amekutwa pia na begi kubwa la kubeba mgongoni.
Masuali kadhaa yamezuka kuhusiana na tukio hili la pili ndani ya miezi miwili kwani itakumbukwa tarehe 13 mwezi Julai, Donald Trump alinusurika kuuawa kijana Thomas Mathew Crooks aliekuwa na umri wa miaka 20 huko Pennsylvania.
Masuali mengine ya msingi ni kwamba Je, Ryan ameiga kile kilofanywa na Thomas (yaitwa Copycat)?
Je, ana watu nyuma yake na ni akina nani?
Je, ni miongoni mwa kundi la watu wasojulikana?
Je, kwa sasa ana msimamo upi wa kisiasa?