Aliyekaa mahabusu miaka 7 kwa kukisababishia Chuo Kikuu Huria hasara, ahukumiwa

Aliyekaa mahabusu miaka 7 kwa kukisababishia Chuo Kikuu Huria hasara, ahukumiwa

Ndio wangemaliza upelelezi mapema ili ahukumiwe, kulikuwa na haja gani yakumuweka miaka 7 mahabusu?!!. Ndio maana jamaa hapo juu kalalamikia mfumo wetu wa upelelezi ni hovyo.
Wapi umesoma kuwa alikaa miaka 7 kwa kuwa "upelelezi haujakamilika"?

Nilichoona mimi alikuwa na kosa la "utakatishaji fedha" ambalo, nijuavyo, halina dhamana
 
ni hasara gtani aliitia chuo mbona hakisemwi?
 
Kwakuwa ana mtoto mdogo anaemumwa saratani na ameshakaa miaka 7 gerezani nadhani angeachwa tu hiyo pesa aende akamuuguze mwanawe, tuwe na utu kidogo, ameshakiri na kujutia, aachwe tu.
Bado ngumu kumeza,
yupo kifungo cha nje atamuhudumia mwanae
Je mwanae ni miaka mingapi km ni chini ya 7 basi alimpata akiwa huru au
kwa Kesi hizi za kukiri Makosa na kulipa wangeachiwa huru kabisa km Magufuli alivyosema akilipa muachieni akashiriki na wenzake Uraiani
 
Miaka saba upepelezi ulikua bado sio? Kuna haja ya kubadili huu utaratibu maana miaka saba na isinge kua haya mabadiliko ya sheria ange kaa zaidi ya hapo maana kuchelewa kwa haki ni chanzo cha kukosa au kunyimwa haki kwa mtuhumiwa alie mahabusu.
 
Wapi umesoma kuwa alikaa miaka 7 kwa kuwa "upelelezi haujakamilika"?

Nilichoona mimi alikuwa na kosa la "utakatishaji fedha" ambalo, nijuavyo, halina dhamana
weee nawe ina maana makosa ya utakatishaji wa pesa yanamfanya mtu ake mahabusu miaka 7!!!!!!!!!!!!
 
Na baada ya miaka yote hiyo, serikali bado imeshindwa kuiletea mahakama ushahidi, mpaka mtuhumiwa aamua kukubali ili yaishe.
Vyuo vyetu vinatoa wahitimu vilaza.
Mahabusu miaka saba! Kuna haja ya kubadili mfumo wa upelelezi katika nchi yetu haiwezekani unapeleleza miaka saba huku mtuhumiwa akiwa Mfungwa wa Mahabusu bila kuthibitishwa hatia yake
 
Mfumo wetu wa utoaji haki haufai tena haufai sana.

Watu wanakaa mahabusu hata miaka kumi eti upelelezi haujakamilika.

Kimsingi huu ni uonevu tu kama uonevu mwingine tu
 
Na baada ya miaka yote hiyo, serikali bado imeshindwa kuiletea mahakama ushahidi, mpaka mtuhumiwa aamua kukubali ili yaishe.
Vyuo vyetu vinatoa wahitimu vilaza.

Tuna sheria za kikandamizaji sana utetezi Wake wanasema mtuhumiwa ataharibu ushahidi
 
Mahabusu miaka saba! Kuna haja ya kubadili mfumo wa upelelezi katika nchi yetu haiwezekani unapeleleza miaka saba huku mtuhumiwa akiwa Mfungwa wa Mahabusu bila kuthibitishwa hatia yake
No hurry in Africa
 
Back
Top Bottom