The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Siku chache baada ya kufutwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana sababu ya kupinga uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa CCM, Mchungaji Dkt.Godfrey Malisa amedai kuanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu maisha yake na kuwa yupo katika hatari baada ya kusema ukweli.
Akizungumza na Jambo Tv kuhusu kinachoendelea, Malisa amesema “na niwaambie watanzania wajue tu kwamba nipo kwenye wakati mgumu sana kwa sababu tu nimesimama kusema kweli, tumefika mahali hata watu wanatoa ushauri kwamba afadhali uondoke hata nchini”
Soma pia: Aliyepinga Rais Samia kupitishwa Mgombea pekee wa Urais kupitia CCM afukuzwa uanachama
Aidha Dkt. Malisa ameongeza kuwa ameshangazwa sana na hali hiyo ya kufikia kutishiwa hali ya kuwa tu ni kasema ukweli “Tunafika mahali tunasema hivi nchi yetu tupo hapo mahali pa kutishiwa kwa sababu tu unasema kweli. Nakumbuka mwanzoni kuna watu walikuja wakaniambia bana jihadhari” amesema Dkt. Malisa
Aidha amewaomba watanzania kumuombea kwa Mungu kwani anaamini ulinzi wa Mungu utamuwezesha kuivuka hali anayopitia