Pre GE2025 Aliyekosoa uteuzi wa Samia kuwa mgombea Urais ahofia maisha yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndivyo ilivyo kwa nchi yetu! Ukichagua kusema Ukweli ujiabdae kwa lo lote baya.
Hata hivyo mchungaji ametoa tahadhari kama kinga.
 
Kwa hiyo huyo mshuganji alikuwa hajasoma kisa cha Daudi na Mfalme Sauli?

Li Sauli ile kuona Daudi anaimbiwa kuwa ameua makumi elfu halafu lenyewe wanaliimbia limeua maelfu likasema moyoni

Wamebakiza kumpa ufalme pekee.

Kuanzia hapo, Daudi aliishi kama ndege mpaka alipokufa Sauli.
 
Siku chache baada ya kufutwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana sababu ya kupinga uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa CCM, Mchungaji Dkt.Godfrey Malisa amedai kuanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu maisha yake na kuwa yupo katika hatari baada ya kusema ukweli.

Akizungumza na Jambo Tv kuhusu kinachoendelea, Malisa amesema “na niwaambie watanzania wajue tu kwamba nipo kwenye wakati mgumu sana kwa sababu tu nimesimama kusema kweli, tumefika mahali hata watu wanatoa ushauri kwamba afadhali uondoke hata nchini”

Soma pia: Aliyepinga Rais Samia kupitishwa Mgombea pekee wa Urais kupitia CCM afukuzwa uanachama

Aidha Dkt. Malisa ameongeza kuwa ameshangazwa sana na hali hiyo ya kufikia kutishiwa hali ya kuwa tu ni kasema ukweli “Tunafika mahali tunasema hivi nchi yetu tupo hapo mahali pa kutishiwa kwa sababu tu unasema kweli. Nakumbuka mwanzoni kuna watu walikuja wakaniambia bana jihadhari” amesema Dkt. Malisa

Aidha amewaomba watanzania kumuombea kwa Mungu kwani anaamini ulinzi wa Mungu utamuwezesha kuivuka hali anayopitia

View attachment 3240687
Huyo wenge ndio litamuua na sio kingine. Yaani CCM itishwe na mtu ndogo kama huyo? Ujinga kabisa!
 
Uzuri watakao kuua na kukutishia wanajitengenezea laana .Ona sasa watoto wa viongozi walivyo kaputi .Viongozi wanaumwa magonjwa ya kutatanisha nk .Na wao hawaishi milele watakufa tu hata uwe raisi au papa.
Kivip wakati hata wewe ulietapeliwa na hao viongozi pia unateseka kwa ugumu wa maisha na kuumwa na hatimae kufa?
 
Aidha Dkt. Malisa ameongeza kuwa ameshangazwa sana na hali hiyo ya kufikia kutishiwa hali ya kuwa tu ni kasema ukweli “Tunafika mahali tunasema hivi nchi yetu tupo hapo mahali pa kutishiwa kwa sababu tu unasema kweli. Nakumbuka mwanzoni kuna watu walikuja wakaniambia bana jihadhari” amesema Dkt. Malisa
Wanaomtishia watashindwa kwa jina la Mungu iwapo alichokisema kina ukweli ndani yake
 
Ajabu ya wanadamu......

MTU unaipigania dunia mpaka uko tayari kuwaangamiza wanadamu wenzako kana kwamba utaishi milele.....

Unapata ujasiri wa kuwaangamiza, kuwadhuru, kuwaringia na hata kujikweza kwenye huu ulimwengu hali ya kuwa siku moja utakufa na mwili wako utahifadhiwa kwenye kipande kidogo cha ardhi......

Hizo fedha, mali na madaraka vinavyokuvua utu kwa wanadamu wenzako vyote utaviacha na hata ukifukiwa navyo havitakuwa na manufaa yoyote kwako.....

Mwanadamu wewe ambaye maiti yako hata wale wapendwa wako watakuwa wanaiogopa unajivuna nini wewe kwenye mgongo wa ardhi....

Ndugu zangu.... maisha ya mwanadamu hapa duniani ni mfano wa msafiri aliyejificha kivulini........

Vyeo, madaraka na mali visitutie upofu na ujivuni mbele ya binadamu wenzako.......

Siku moja utakufa au kupata mtihani na utaiona dunia chungu.....

TUISHI KWA WEMA.....
Umenena vyema mkuu,
Aione Tlaatlaah na aifikishe mezani kwa anayemtuma, na bila kusahau machawa wote
 
Siku chache baada ya kufutwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana sababu ya kupinga uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa CCM, Mchungaji Dkt.Godfrey Malisa amedai kuanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu maisha yake na kuwa yupo katika hatari baada ya kusema ukweli.

Akizungumza na Jambo Tv kuhusu kinachoendelea, Malisa amesema “na niwaambie watanzania wajue tu kwamba nipo kwenye wakati mgumu sana kwa sababu tu nimesimama kusema kweli, tumefika mahali hata watu wanatoa ushauri kwamba afadhali uondoke hata nchini”

Soma pia: Aliyepinga Rais Samia kupitishwa Mgombea pekee wa Urais kupitia CCM afukuzwa uanachama

Aidha Dkt. Malisa ameongeza kuwa ameshangazwa sana na hali hiyo ya kufikia kutishiwa hali ya kuwa tu ni kasema ukweli “Tunafika mahali tunasema hivi nchi yetu tupo hapo mahali pa kutishiwa kwa sababu tu unasema kweli. Nakumbuka mwanzoni kuna watu walikuja wakaniambia bana jihadhari” amesema Dkt. Malisa

Aidha amewaomba watanzania kumuombea kwa Mungu kwani anaamini ulinzi wa Mungu utamuwezesha kuivuka hali anayopitia

View attachment 3240687
Huyu wanae Tu LAZIMA watamla kichwa
 
Back
Top Bottom