Aliyekuwa askofu Konde aondolewa wakfu. Fimbo, msalaba na pete yake vyaondolewa wakfu pia. Sasa atabakia kuwa muumini wa kawaida

Aliyekuwa askofu Konde aondolewa wakfu. Fimbo, msalaba na pete yake vyaondolewa wakfu pia. Sasa atabakia kuwa muumini wa kawaida

Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde leo imetangaza kumwondolea wakfu wa Uaskofu aliyekuwa askofu wa Dayosisi hiyo, Dk. Edward Mwaikali.

Pia imeviondolea wakfu vifaa vya Kiaskofu alivyokuwa anatumia kama pete, msalaba pamoja na fimbo ambavyo alikabidhiwa tarehe 18 Januari 2018 alipowekwa wakfu kuiongoza Dayosisi ya Konde.

Uamuzi huo umefanyika leo Jumapili Juni 5, 2022 wakati wa lbada ya kumweka wakfu mrithi wake, Dk. Geofrey Mwakihaba.

Wamefikia hatua hiyo baada ya Dk. Mwaikali kugoma kuvirejesha ili vitumike kwa mrithi wake kwa mujibu wa taratibu za kanisa hilo.

Dk. Mwaikali aliondolewa madarakani tarehe 22 Machi 2022 na Mkutano Mkuu Maalum wa KKKT Dayosisi hiyo kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuiongoza vyema.

Vitu vingine ambavyo amegoma kuvirejesha ni kiti cha uaskofu na mavazi ambavyo navyo vimeondolewa wakfu.

View attachment 2251168

Fimbo, msalaba na pete yake vyaondolewa wakfu ila ameruhusiwa kuvitumia akihamia au kuanzisha kanisa jingine kwani vyote hivyo ni mali ya bwana.​

 
Ila Papa hana huwezo wa kumvua Mtumishi wakfu, wanaamini ni MUNGU pekee. Ndiyo maana Mtumishi akikengeuka atatupwa jela ama Segerea au Vatican akimaliza kifungo anahamishiwa Japan au US nk, wakfu wake unaendelea hadi mauti. RC muumini hawezi kumpiga Mtumishi au kumfukuza Parokia, KKKT hiyo ni rampant!
Kila mtu anautaratibu wake kwenye maisha hatufanani
 
Kuwa mburula siyo tatizo kwa sababu fani yo yote isiyo yako utakuwa mburula kwenye hiyo fani may be huyo hayupo kwenye masuala yanayoweza mpa hizo taarifa.Yaani ni sawa na wewe ulivyo mburula kwenye elimu inayomhusu Mungu ndo maana umburula huo unakupa hitimisho hakuna Mungu, ilhali wenye ufahamu na elimu kumhusu Mungu tuna uhakika yupo,alikuwepo na milele atadumu kuwepo.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
Achana na hadithi za kitaahira za kwenye quran na biblia. Mungu hayupo.

Dini ni taasisi za kitapeli, mungu hayupo.
 

Fimbo, msalaba na pete yake vyaondolewa wakfu ila ameruhusiwa kuvitumia akihamia au kuanzisha kanisa jingine kwani vyote hivyo ni mali ya bwana.​

Huko kwingine atakuwa Askofu bila uchaguzi? Anahamia navyo huko kwani kachaguliwa kuwa Askofu huko?
Hata Wakimchagua kanisa litakuwa na nembo zake kwenye mavazi nk huwezi kutumia nembo za KKKT sheria za hatimiliki haziruhusu.Inabidi atafute vyake sio hivyo vya KKKT
 
Mkuu kufanikiwa kwa kupata wafuasi ama kupata Mali nyingi hakuna uhusiano na kuupata uzima wa milele.

Mungu ametuacha huru hapa Duniani na uchaguzi wetu.
Unaweza ukawa maskin duniani na ukaenda motoni umaskin sio kipimo Cha uadilifu
 
N
Huko kwingine atakuwa Askofu bila uchaguzi? Anahamia navyo huko kwani kachaguliwa kuwa Askofu huko?
Hata Wakimchagua kanisa litakuwa na nembo zake kwenye mavazi nk huwezi kutumia nembo za KKKT sheria za hatimiliki haziruhusu.Inabidi atafute vyake sio hivyo vya KKKT
Ningekuwa mimi ningeviuza au luwagawia watoto yatima ili fedha zitakazopatika ziwasaidie
 
Wewe mwenye elimu kubwa nionyeshe mungu yuko wapi ama umewahi kumuona wapi.

Usiniletee hadithi za kitaahira za kwenye quran na biblia.
Jifunze kuheshimu watu wanachoamin hata kama wewe uami hujashikiwa fimbo umin kama Mungu yupo au hayupo au kwanin unaumia kwa watu wengine kuamin Mungu yupo na Tanzania Kuna uhuru huo

Huamin Mungu hayupo lakin uko bize kwenye nyuzi zinazohusu kanisa ambalo linaamin Mungu yupo
Live your life
 
natanguliza samahani, naomba mnipe jina la askofu KKKT wa kinyakyusa AMBAYE HAJA-CREATE MIGORORO PALE ALIPO, AU ALIPOKUWA
kwakuangalia majina yao aliyeondolewa na aliyewekwa wote wanyakyusa
 
Jamaa amekomaa hataki kuachia ulaji wa madhabahuni
 
Mimi sio muumini wa dini kwa sababu mungu hayupo ila dini kama taasisi za kihiyari zina taratibu zake na lazima kama unataka kua muumini ama kiongozi ufuate hizo taratibu.

Huyo askofu alienda kinyume na taratibu za kanisa na kujiona ni mkubwa kuliko kanisa sasa kanisa limemmaliza kabisa.

Ni vyema watu kuheshimu taratibu za taasisi walizokubali kwa hiyari yao kua wanachama ama viongozi.

Nakumbuka miaka ile ya kuibuka kwa makanisa ya kilokole, kiongozi mmoja wa kanisa la kilokole, Kulola aliasi TAG na akaamua kukatalia majengo na makanisa ya TAG. Tukawa tunajiuliza kama umeamua kua mwenyewe kivyako si uachie vitu vya watu, ikawa shida kubwa.

The same ikaja kwa Free Pentecoste church na Pentecoste church of Tanzania.
Mungu hayupo ?🤔

unadhani kila kitu unachokiona ulimwenguni hakuna controller?
 
Aombe MSAMAHA aache kiburi cha Uzima!
 
ugomvi wa nini? Mbona karahisishwa kuanzisha huduma yake. Huu mtifuano kwake una faida kubwa
 
Ni nini wameamua kumdhihaki hivi.

Wameshindwa kumstahi hata kidogo mpaka wanamdhalilisha hivi.

Hivi vitu unaweza ona ni kawaida ila vinaumiza moyo.

Wao wana uhakika upi kuwa ni watumishi halali wa Bwana.
Ukitaka kulielewa hili vizuri ni kama Magufuli alivyomuondowa CAG Profesa Assad wakati hakuwa na mamlaka hayo kikatiba.

Hivyo basi Askofu wa mnyororo akishawekwa wakfu hakuna mwenye uwezo wa kumvuwa huo Uaskofu hilo halipo.

Kinachowezekana ni kumvuwa tu madaraka ya Kiaskofu kwenye dayosisi na mfano mzuri ni Askofu Mokiwa wa Anglican alivuliwa madaraka tu lakini bado ni Akofu.

Huwezi kumvuwa Jaji title yake, huwezi kumvuwa mwalimu tittle yake, kinachoendelea Konde ni bangi tu kuzidi kutuamsha kwamba dini ni biashara na hii ni vita ya kimaslahi.
 
natanguliza samahani, naomba mnipe jina la askofu KKKT wa kinyakyusa AMBAYE HAJA-CREATE MIGORORO PALE ALIPO, AU ALIPOKUWA
D ah ni kama kweli hivi....maana mgogoro wa konde ka create Malasusa halafu.......
 
Back
Top Bottom