Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA, Saed Kubenea amejiondoa ndani ya chama hicho na kujiunga na ACT-Wazalendo

Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA, Saed Kubenea amejiondoa ndani ya chama hicho na kujiunga na ACT-Wazalendo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
MBUNGE wa Ubungo, Dar es Salaam anayemaliza muda wake kupitia Chadema, Saed Kubenea amejiondoa ndani ya chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.

Kubenea amejiunga na ACT-Wazalendo leo Jumamosi tarehe 18 Julai 2020 na kupokelewa na Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa chama hicho Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Pia, katika hafla hiyo, zaidi ya wanachama 48 wa Chadema wamejiunga na ACT-Wazalendo.

Mara baada ya kukabidhiwa kadi, Kubenea amemshukuru Maalim Seif kwa kumpokea.
“Nimekuwa kwenye harakati za kutetea mfumo wa vyama vingi, haki sawa kwa watu wote, haki za kisheria, haki za binadamu kwa karibu miaka 20 sasa. Nimekuwa mbunge wa Ubungo kwa miaka mitano,” amesema
Kubenea amesema, “nimelazimika kuondoka huko nilokokuwa. Nawashukuru sana viongozi wakuu bila kuwataka majina waliofanikisha mimi kufika leo.”

“Uamuzi huu haukuwa mwepesi, ulikuwa mgumu sana, kwa sababu katika maisha yangu, hiki ndicho chama cha pili kujiunga,” amesema mwandishi huyo wa habari

Kubenea amesema, “nilifika mahali nikasema, kama Maalim Seif alifika mahali akaondoka CUF aliyoianzisha. Mabere Marando mwasisi wa NCCR-M`ageuzi aliondoka na kujiunga na Chadema na wengine wengine, sembuse mimi.”

“Nilijifunza kwa wazee wangu hawa kwamba lazima safari ya mabadiliko iendelee. Nawashukuru sana wananchi wa Ubungo waliokuja kwenye chama chetu,” amesema

Kubenea amesema, katika Jiji la Dar es Salaam, upinzani una nguvu kubwa na kama vyama vya upinzani vikishirikiana vitafanya vizuri kuliko mwaka 2015 huku akiomba vyama hivyo kutanguliza maslahi ya wananchi mbele kuliko maslahi binafsi.
 
Good for you Kubenea, una haki kikatiba kuhamia chama chochote. Siasa ni ajira kama zilivyo nyingine muhimu ni itikadi za huko unakoenda.
 
Naamini Kubenea ana kitu kinamsumbua japo hajawa muwazi, maana nikijaribu kutafakari amekuwa akihusishwa na tuhuma za usaliti na hata kuhama chama mara kadhaa na kuna siku aliitisha press conference ikihusishwa na kutangaza kuhama chama japo alibadili gia angani.

Ila imekuwa tofauti na matarajio ya kuhama kwake maana alitarajiwa kuhamia CCM kuunga juhudi ama NCCR-Mageuzi baada ya kugain momentum lakini ameshangaza kuhamia ACT-Wazalendo.

Ameonekana mara kadhaa kupoteza imani ndani ya Chadema na kuonekana hana raha wala amani huko ndani. Nadhani Kubenea ana kitu ambacho hakiko sawa ila amekuwa akijistahi sana kuelezea umma.
 
Back
Top Bottom