Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA, Saed Kubenea amejiondoa ndani ya chama hicho na kujiunga na ACT-Wazalendo

Basi atakuwa amepatwa na uwendawazimu. Mtu yeyote anayeanza kukisema vibaya chama alichokuwepo kabla, lazima ana shida kichwani.

Siku zote umekaa huko, hukuwahi kulalamika, siku unaondoka au umefukuzwa, unaanza kusema kuwa namwaga mboga - really stupid. Na atakayezingatia unayoyasema, kichwani lazima kuwe na upungufu.

Wenye akili
- Lowasa alipotoka CCM kwenda CDM alisema nini dhidi ya CCM? Alipotoka CDM kwenda CCM alisema nini dhidi ya CDM?

- Dr. Slaa alipotoka CCM kwenda CDM alisema nini dhidi ya CCM? Alipotoka CDM kwenda CCM alisema nini dhidi ya CDM?

- Nyarandu alipotoka CCM kwenda CDM alisema nini dhidi ya CCM?

- Rwakatare alipotoka CUF kwenda CDM alisema nini dhidi ya CUF, alipoenda tena CUF alisema nini dhidi ya CDM

Wapo wengi wa namna hiyo. Hivyo ndivyo wenye akili wanavyofanya.

Lakini wale ambao wanasimama kwenye mstari unaogawanya waliowazima na wenye upungufu wa akili, kama akina Lijuakali, fuatilia walisema nini siku walipoondoka vyama vyao vya awali kwenda vyama vingine. Na ndivyo watakavyofanya watakapoondoka waliko leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najaribu kumbuka tu. Hivi Lowassa alipoondoka CHADEMA alisemaje? Mi sikuwepo Ila walokuwepo watasema
 
Tunafahamu kuna mengi unayajua, ndio maana hata msaidizi wa Mbowe ( Kijana wa Rombo ) ilipokuwa ikisemwa amepotea, wewe ulisema yupo na watu wamekutana nae na kuongea.

Utatusaidia sana , yawezekana kama yaliyompata LISSU ni mchezo wa chama cha Mbowe wewe ukafahamu. Na hii inaweza kusaidia taifa kupata ufumbuzi wa mafumbo ambayo tumeshindwa kupata ufumbuzi.. Na hata suala la FARU JOHN wakati akitokea nyumba ndogo Mukya, utata unaweza kumalizwa kabisa. KARIBU KARIBU KARIBU.
 
Hana madhala,alishapima upepo,hata kura za maoni angepigwa chini,limeshakuwa Galasa.
 
Halafu utasikia CHADEMA wanajiendelea kujifariji tu, jikoni fukuto sio la nchi hii.
 
safari salama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…