Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu TPA, Deusdedit Kakoko aachiwa kwa dhamana baada ya TAKUKURU kukamilisha Uchunguzi dhidi yake kwa 98%

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu TPA, Deusdedit Kakoko aachiwa kwa dhamana baada ya TAKUKURU kukamilisha Uchunguzi dhidi yake kwa 98%

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndio taarifa ya TAKUKURU iliyotolewa kwa vyombo vya habari , na kwamba hizo 2% zilizobaki zitakamilishwa na ofisi ya CAG

Hakuna Taarifa kama atafikishwa Mahakamani au la .

Tuendelee kufuatilia .

====

Takukuru yamwachia ‘bosi’ bandari, “waulizwe CAG”

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Brigedia Jenerali, John Mbungo amesema, imemwachia kwa dhamana, aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa bandari Tanzania (TPA), Deusdedit

Ni baada ya kushikiliwa kwa siku kadhaa na Takukuru, siku chache kupita, tangu Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kutangaza kumsimamisha kazi, kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh.3 bilioni ndani ya mamlaka hiyo.

Rais Samia alitoa maagizo hayo, Jumapili ya tarehe 28 Machi 2021, mara baada ya kupokea ripoti mbili za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na ya Takukuru zote za mwaka 2019/20, Ikulu ya Chamwoni, mkoani Dodoma.

Mara baada ya maagizo hayo, Kakoko ilimkamata kwa mahojiano ambapo leo Jumamosi, tarehe 17 Aprili 2021, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbungo akijibu swali la MwanaHALISI Online, lililotaka kujua kinachoendelea ambapo amesema “tumemwachia kwa dhamana.”

Mbungo amesema, “uchunguzi wenye tuhuma kubwa kama hii, unahusisha watu wengi sana na akikosekana hata mmoja, unaweza usikamilike. Lakini sisi (Takukuru), tumekamilisha kwa asilimia 98 na asilimia mbili zimebaki kwa CAG.”

Amesema, CAG anafanya ukaguzi wa athari iliyotokana na ubadhirifu huo kisha apelekewe Mwendesha Mashataka wa Serikali (DPP), ambaye naye atapeleke jalada hilo mahakamani.

“CAG lazima aandae uchunguzi maalum wa hasara iliyopatikana na sisi tunaweza kuwa tumekamilisha, lakini CAG kama hajamaliza hawezi kupeleka kwa DPP na DPP hawezi kuupeleka mahakamani,” amesema Mbungo

Bosi huyo wa Takukuru amesema “Takukuru imekamilisha asilimia 98 na asilimia mbili niya CAG ya ukaguzi maalum. Sasa waulizeni CAG kuwa ukaguzi huo maalum mmekwisha ukamilisha? Na ukienda kwa DPP, mnamuuliza DPP, lini litakwenda mahakamani?

MwanaHALISI Online, limeutafuta uongozi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujua ukaguzi huo maalum ulipofikia, bila mafanikio. Jitihada zaidi zinaendelea kuutafuta, akiwemo CAG mwenyewe, Charles Kichere.

Credit: Mwanahalisi


Pia soma:

 
Wakimalizana na Kakoko, anaefuatia ni Dr. Kigwangalla.
Watu wameanza kufukua makaburi _joy__joy__joy_ kosa la  @hamisi_kigwangalla amewaambia wa ( 62...jpg
 
Hii ndio taarifa ya TAKUKURU iliyotolewa kwa vyombo vya habari, na kwamba hizo 2% zilizobaki zitakamilishwa na ofisi ya CAG

Hakuna Taarifa kama atafikishwa Mahakamani au la.

Tuendelee kufuatilia.
CCM ni ile ile. Huyo hachukuliwi hatua zozote. Kwani wenzake kama Kingwangala wamemfanyaje na anajulikana amekwiba mahela kibao kwa promo fake za mlima Kilimanjaro.
 
Hii ndio taarifa ya TAKUKURU iliyotolewa kwa vyombo vya habari , na kwamba hizo 2% zilizobaki zitakamilishwa na ofisi ya CAG

Hakuna Taarifa kama atafikishwa Mahakamani au la .

Tuendelee kufuatilia .
Kama ni 98%maana yake wakati wowote atafikishwa mahakamani, ni kama kaambiwa akaage kabisa
 
Magufuli aliupata uRais kwa Zali/hakujiandaa. Samia naye ameupata Urais kwa zali pia, hakujiandaa.
Tuendapo ni Mungu anajua.

Kama hujui uongozi unamfaa sana unayemwangukia,na si anayeutafuta.

Rejea hata kauli za nyerere, urais sio kichaka ni zigo la misumari.
 
kama hujui uongozi unamfaa sana unayemwangukia,na si anayeutafuta.

rejea hata kauli za nyerere,urais sio kichaka ni zigo la misumari.
Karne ya 21 kwanini tuendelee kuongozwa na viongozi wanaoangukiwa na uongozi kama Unabii?
 
Back
Top Bottom