TANZIA Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brig. Jen Mstaafu Emmanuel Maganga afariki Dunia

TANZIA Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brig. Jen Mstaafu Emmanuel Maganga afariki Dunia

Usiogope kifo,hakikwepeki ndiyo maana ukaambiwa kila nafsi itaonja Umauti ni swala la muda tu!!

Hakuna aogopaye kifo. Ila ni kifo cha kijinga kutokiepuka kifo kama yawezekana. Hata Masiah aliomba kikombe kile kimwepuke panapo uwezekano.

Tusidanganyane!

Watu wanapukutika uwezo wa kuchukua hatua au kuwataka watu kuchukua hatua upo. Tunadanganyana kijinga jinga tu?

Ukweli mchungu siku moja majina ya wote waliotelekezewa gonjwa hili yatatajwa mbele zake na atawajibika vilivyo hata kama leo anajiita jiwe.
 
Nilikutana na huyu mzee JM mall samora 04/01/2021 akinunua pikipiki, nikasalimiana nae alikua bukheri wa afya.
 
Una uhakika amekufa na Corona?.
Au ndo furahisha genge

Corona ni ugonjwa na unauwa kama yanavyouwa magonjwa mengine.

Kwanini kuna mijamaa hasa ya chama fulani mtu akifa inahaha sana kudai kuwa siyo corona? Kwani corona haiuwi?

Kwani kama corona inauwa kwanini kuhangaika mno kutaka kuonyesha kuwa siyo corona iliyomwua marehemu fulani? Ikizingatiwa kuwa dalili ziko wazi na mhusika mkuu asiyetaka ijulikane kiini cha vifo kapiga marufuku mambo ya postmortem kujua sababu za vifo, achilia mbali kutangazwa takwimu za corona?

Ama kweli, "wajinga kama mjinga mimi ndiyo waliwao."
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig.Jen Mstaafu Emmanuel Maganga amefariki Dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Milambo Mkoani Tabora usiku huu.

View attachment 1682982
#RIPMaganga
Ameenda kumuandalia makao yule mtu! Yani huko kwa sasa anasema sikiliza sauti itokayo nyikani, nimekuja kumuandalia makao yule atakayekuja kwa ajili ya kuwa mkuu wenu. Amin nawaambieni yu njiani kuja!
 
Lala salama Brig.Jen Mstaafu Emmanuel Maganga
Pole kwa familia na wote walioguswa na msiba
 
Mkuu Aligombea ubunge kama sikosei....Siku zetu huisha..MUNGU amlaze pema.
 
Alipostaafu ukuu wa mkoa niliona kaenda kwa Mama yake ili ampe baraka maana alitaka kugombea ubunge kwao, mimi nilijua alipenya na ni mbunge kumbe hakufanikisha ndoto yake?

Pole kwa wahusika. Bwana awafariji kuna tumaini ng'ambo ya kaburi Kristo atakaporejea mara ya 2, kwa wale waliolala upande wake
 
Corona itatumaliza
Kila Mtu akifariki corona, kwani Kabla ya corona Watu walikuwa hawafi.

Please tuache Kejeli za kishamba. Watu wa Kigoma tunamheshimu saaana, ndiye muasisi wa Uboreshaji wa zao la Michikichi.

R . I .P Brigedia Mstaafu Emmanuel Maganga Mzee wa Sauti ya Zege/Sauti nzito.
 
Ameenda kumuandalia makao yule mtu! Yani huko kwa sasa anasema sikiliza sauti itokayo nyikani, nimekuja kumuandalia makao yule atakayekuja kwa ajili ya kuwa mkuu wenu. Amin nawaambieni yu njiani kuja!
Na liende tu
 
Yupo mtu akifa huyo tutasema korona ipo na tutakuwa sehemu ya Ulimwengu tena. Kwasasa tupo kwenye jela baya la afya
 
Hivi ndani ya mwezi huu wamekufa watu wangapi wenye/walikuwa nyazifa kubwa?
Samahani nauliza tu
 
Zamani ukuu Wa mkoa ilkuwa cheo cha hatari,ilkuwa ni lazima uwajue wakuu Wa mikoa yote Tanzania.

Maana wakati mwingine unaweza kuulizwa swali kwenye mtihani,mf taja mkuu Wa mkoa Wa Mwanza?,unataja chapu.

Ila toka wameanza kuwekwa vijanavijana hawa mwendo kasi ka kina Gambo,Makonda,Hapi nk,wameharibu hicho cheo tokana na matendo yao hasa hicho cheo kuwa cha kisiasa zaidi.

Mi nilikuwa hata sijui mkuu Wa mkoa huo JIna ndo naskia Leo baada ya Ku RIP,hata ukiniuliza sa hii mkuu Wa mkoa nilioko saa jina lake sijui mpaka niingie Google.
Hata kipindi nasoma maswali ya hivi kuulizwa majina ya wakuu wa mikoa /mawaziri yalikuwa yanatoka sana kwa sasa Sina uhakika Mara kila kukicha wanabadilika
 
Nimeona clip tweeter akimkaripia mama eti hajalipa kitambulisho. Unaona kabisa kuwa hana utu kabisa kwa yule mama masikini!
 
Back
Top Bottom