Aliyekuwa mtumishi wa TAKUKURU Tanga ahukumiwa kulipa faini ya Tsh. milioni 1 kwa kupokea rushwa ya dola 2500

Aliyekuwa mtumishi wa TAKUKURU Tanga ahukumiwa kulipa faini ya Tsh. milioni 1 kwa kupokea rushwa ya dola 2500

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Januari 16, 2023, Jamhuri imeshida kesi ya Jinai yenye namba CC 56/2021 iliyokuwa ikiendeshwa na Mwendesha Mashtaka Joseph Mulebya pamoja na Khadija Luwongo kutoka TAKUKURU.

Katika kesi hii mshtakiwa alikuwa Bw. Hilton Njau aliyekuwa mtumishi wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga ambaye amekutwa na hatia ya makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa ya Dola za Marekani 2500, kutoka Kwa mfanyabiashara mwenye asili ya kihindi, ili asimchukulie hatua kwenye masuala ya ukwepaji kodi yaliyokuwa yakifanyiwa kazi na mshtakiwa akiwa kama Afisa Uchunguzi wa Taasisi hiyo.

Mshtakiwa ameamriwa kulipa faini ya shilingi 500,000/= kwa kila kosa ambapo kwa makosa mawili ametakiwa kulipa jumla ya shilingi 1,000,000/=. Mshtakiwa amelipa faini.
 
Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Januari 16, 2023, Jamhuri imeshida kesi ya Jinai yenye namba CC 56/2021 iliyokuwa ikiendeshwa na Mwendesha Mashtaka Joseph Mulebya pamoja na Khadija Luwongo kutoka TAKUKURU.
Kwani rushwa si jela miaka 30
 
Kwa kukosa uadilifu bado huyu mtumishi ana rejea kazini?

Rushwa itaisha kweli?
 
Wale wanaohukumiwa kwenda jela, ni kwamba huwa wameshindwa kulipa faini au?

Kila siku matangazo ya rushwa lkn kila kukicha, rushwa inachukuwa sura mpya. Najaribu kutafakari au labda basi taarifa haijitoshelezi, sasa pesa aliyopokea $2500 yenyewe kwa sasa iko upande gani? Uwiano wa $2500 kwa faini ya $ 450 hivi uko wapi?

Tutafika mbinguni tukiwa hoi
 
Kisheria, kukutwa kwake na hatia mahakamani kunampa Mamlaka yake ya Nidhamu nafasi ya kumshughulikia kiutumishi. Kimsingi, ajira yake 'imeshakoma' kuanzia siku hiyo. Kupoteza kazi ni adhabu kubwa kuliko hiyo faini ya milioni moja. Milioni tano zimemponza. Ajiongeze tu!
 
Hapo hana tena kazi maana amehukumiwa na mahakama angeonekana hana hatia ndio ingekuwa salama yake lakini kashamwaga unga tayari kwa milioni tano, atajuta maisha yake yote maana ajira za kibongo zilivyo ngumu ni balaa kabisa. ukute aliingia kazini kimchongomchongo pia
 
Kwa hiyo Akitoa faini anaendelea na kazi au kibarua chake tukafyeke nyasi?
Ninavyoelewa, mtumishi wa umma akishitakiwa na kupatikana na hatia, kazi huwa kantolee!
Angelishinda kesi hapo tungeliongea vinginevyo.
 
Kwahiyo kapata faida ya milioni nne kati ya Tano alizokuwa amepokea awali?
 
Hapo kaambiwa pokea teeana na omba sana rushwa umeona faini ni ndogo.
 
Takukuru watamrudisha kazini na kumlipa haraka Sana pesa zake!!!hii ndio Tz
 
Back
Top Bottom