PreGE2025 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Shinyanga, Emmanuel Ntobi na Glory Tausi wajiunga na ACT Wazalendo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi amehamia chama cha ACT Wazalendo na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu.

Akizungumza leo Juni 03, Ado amesema "wapiganaji ambao wamegonga mlangp hapa ACT tumekuwa tukiwapokea leo ninayo furaha ya kuwaleta mbele yenu wapigananaji wakubwa wawili katika siasa za Tanzania ambao wamepata heshima ya kupokelewa na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo"

"Tunao wapiganaji wawili hapa tunaye ndugu yetu Emmanuel Ntobi yeye mpaka hivi sasa ni kada mwandamizi wa CHADEMA ameniandikia barua rasmi jana na kusema anayo nia ya kujiunga na ACT Wazalendo wa pili ni ndugu Glory Tausi na yeye ni kada mwandamizi"

Ado ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha watu wengine ambao wanataka kujiunga na chama hicho kuwa nafasi zipo.

Baada ya kuwapokea wanachama hao wapya Ado amewakabidhi Kadi ya mwanachama ya Maalim Seif pamoja na Katiba ya chama hicho.

"Tulikaa na baadhi ya wenzangu tuliokuwa G55 tukapitia baadhi ya katiba, tukapitia baadhi ya vyama, lakini kiukweli kwa sasa hivi anayeweza kuiangusha CCM ni ACT Wazalendo." - Emmanuel Ntobi, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga

yote ni kutafuta ubynge, let us wait and see!
 
Hana muda huko atakimbia.... . ACT hawawezi kubeba gunia la misumari. Hyu hana ushawishi wowote kwenye siasa za Tanzania. Walikuwa wanabebwa na CHADEMA hawa. CHAUMMA wamefungua mkutano Mwanza, wanahutubia nyasi. Na CCM soon ikiona hawana mvuto kwa raia watawatosa baharini.
 
exactly! nimeona live stream hakuna watu
 
Wafundisheni adabu hawa vijana wenu. Hata kama Gwajima amekosea, hizi lugha sio sawa
 
Attachments

  • IMG-20250603-WA0502.jpg
    IMG-20250603-WA0502.jpg
    53.9 KB · Views: 14
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi amehamia chama cha ACT Wazalendo na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu.

Akizungumza leo Juni 03, Ado amesema "wapiganaji ambao wamegonga mlangp hapa ACT tumekuwa tukiwapokea leo ninayo furaha ya kuwaleta mbele yenu wapigananaji wakubwa wawili katika siasa za Tanzania ambao wamepata heshima ya kupokelewa na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo"

"Tunao wapiganaji wawili hapa tunaye ndugu yetu Emmanuel Ntobi yeye mpaka hivi sasa ni kada mwandamizi wa CHADEMA ameniandikia barua rasmi jana na kusema anayo nia ya kujiunga na ACT Wazalendo wa pili ni ndugu Glory Tausi na yeye ni kada mwandamizi"

Ado ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha watu wengine ambao wanataka kujiunga na chama hicho kuwa nafasi zipo.

Baada ya kuwapokea wanachama hao wapya Ado amewakabidhi Kadi ya mwanachama ya Maalim Seif pamoja na Katiba ya chama hicho.

"Tulikaa na baadhi ya wenzangu tuliokuwa G55 tukapitia baadhi ya katiba, tukapitia baadhi ya vyama, lakini kiukweli kwa sasa hivi anayeweza kuiangusha CCM ni ACT Wazalendo." - Emmanuel Ntobi, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga

Chadema wakiona hivyo wanaumia kinyama yaani, sijui kwanini hata 🐒
 
Back
Top Bottom