Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Tanga, ahamia CCM

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe Hamza, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), akieleza kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hali iliyomfanya kuona hana sababu ya kuendelea kuwa upande wa upinzani.

Jumbe amepokelewa rasmi Julai 6, 2026, katika Ofisi za CCM Mkoa wa Tanga, ambapo amesema uamuzi wake umefanywa kwa hiari bila kushawishiwa wala kulipwa fedha, akisisitiza kuwa miradi aliyokuwa akiidai kwa miaka mingi sasa imetekelezwa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah, amesema kujiunga kwa Jumbe ni nyongeza muhimu kwa chama hicho kutokana na ushawishi aliokuwa nao katika siasa za upinzani, akieleza kuwa hatua hiyo inaonyesha kuimarika kwa CCM mkoani humo.

Screenshot 2026-07-06 181439.png
 
Kwani alikuwa na mkataba na Chadema.
 
Uchafu unajichuja........na hao siyo watu wa hivyooooo kwenye mambo ya self awareness....sijashituka na hilo. Wali na ndizi mbivu zatosha
 
Kwa hiyo waliopo upinzani hawaridhiswi na maendeleo yaliyopo?! Waliokuwa wanampinga mkoloni hawakuridhishwa na level ya maendeleo!
 
Back
Top Bottom