Aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli azikwa Chato mkoani Geita

Kwa maelezo ya Majaliwa kuna uwezekano watu walitaka zima mashine ya mama yake JPM asiendelee kupumua aungane na mtoto wake...
Heko rais kwa kulisimamia hilo...
 
Eehh basii eehhh...Hayaaa

Ndugu zanguu..asanteni sana

Barikiwa sana A .H. Mwinyi
 
[emoji120]
 
Umeandika mambo mazuri Ila huko mwishoni umeharibu....
RIP Jemedari wetu JPM
 
Wale wenye chuki nae hawakutegemea kabisa kile kinachotokea baada ya kifo chake, sasa maumivu yamekuwa makali ndani ya nafsi zao kuliko awali.

Kipindi yupo hai waliombea sana afe ,wakiamini maumivu yaliyotokana na chuki zao binafsi kwake yangekwisha kabisa baada ya kifo chake.

Ajabu sasa baada ya kifo chake maumivu na wivu ndio vimeongezeka Mara dufu ndani ya mioyo yao, kwa sasa wana maumivu makali kuliko hata wale waliompenda tangu awali,hawakutegeme mwitikio huu ndio sababu wanashindwa kujizuia kuonyesha maumivu na chuki zao kwa kila aina ya maneno mabaya ili tu kujifariji kwa maumivu waliyonayo.

Sababu ya yote haya, ni wao kujaribu kupingana na ukweli tangu mwanzoni kabisa,wakajitungia UKWELI wao,wakausambaza kwa kadri ya uwezo wao wakautetea na kuupigania kwa kadri ya uwezo wao,mwishoni ndani ya akili zao wakaamini WaTanzania wamekubaliana na UKWELI wao,wakaamini Dunia imekubaliana na UKWELI wao.

Waliosema usibishane na ukweli waliona mbali, na ukibishana nao matokeo yake ndio kama hayo.

sasa baada ya kifo chake,ukweli umejionyesha kinyume na UKWELI wao,hali hiyo imepelekea maumivu makali sana miongoni mwao.

Kuthibitisha hilo la maumivu waliyonayo, angalia comments zao hapa! Ama pitia baadhi ya nyuzi zao na michango yao utayaona maumivu yao yalivyo dhahiri.

Ukweli utakuweka huru ila kwa akili zao,wataendelea kukomaa na UKWELI wao,usiwachukie bali waonee tu huruma!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…