Aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli azikwa Chato mkoani Geita

Hongera sana kamati ya mazishi ya hayati JPM ikiongozwa na mheshimiwa Majaliwa kwa design nzuri ya kaburi la kuslide kama geti yaani mmefanya professioalism.

Ila mmetunyima haki ya kuona jeneza likishushwa kaburini
Kilo 500 za mfuniko unazivuta bila kutumia nguvu.
 
Nakerwa sana na hii kauli iliyozoeleka miongoni mwa jamii yetu, kuwa, eti, "tunaenda kumweka marehemu kwenye nyumba yake ya milele".

Ingekuwa kauli hii inatolewa na watu wa kawaida, wasiojua mafundisho ya dini, wala nisingeshangaa. Lakini, cha kushangaza zaidi, nimekuwa nikiwasikia hata hao wanaojiita viongozi wa dini, Mapadre, Wachungaji, Manabii na Maaskofu wakiongea bila aibu eti, kaburi ni nyumba ya milele.

Jamani, nani kasema kaburi ni nyumba ya milele? Je, YESU KRISTO, alikaa kaburini milele?

Je, siyo YESU aliyesema kifo ni usingizi tu na siku atakapokuja tena, atawafufua wafu?

Sasa kama wafu watafufuliwa, iweje basi tuambiwe na hao wanaojiita viongozi wa dini kuwa kaburi ni nyumba ya milele??
Nini maana ya neno milele? Milele maaana yake, "isiyokuwa na mwisho".
Kwa maandiko yetu sisi Wakristo (Biblia), makaburi yana mwisho, maana yake wafu watafufuliwa na kutoka makaburini, na hao wafu wataishi tena, yaani hawatakufa tena bali wataishi milele katika Ufalme wa MUNGU, na siyo kaburini.

Sasa kama ni hivyo kwanini tunasema kaburi ni nyumba ya milele wakati siyo kweli.

Kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu, kaburi ni nyumba ya muda mfupi tu. Na hilo tulioneshwa wakati wa kifo cha YESU, alikaa kaburini kwa muda mfupi, siku tatu, na kisha akafufuliwa na kupaa Mbinguni.

Nawaomba ndugu zangu Wakristo, tuache huu "ujinga" wa kusema; "tunampeleka marehemu kwenye nyumba yake ya milele". No! Hapana! Kaburi siyo nyumba yetu ya milele na kamwe kaburi haliwezi kuwa nyumba yetu ya milele.

Tukisema kaburi ni nyumba ya milele, basi ni sawa na tunashiriki kumtangaza YESU kuwa ni "muongo", kwani Yeye alisema, "atatufufua siku atakaporudi tena".

Na YESU KRISTO siyo "muongo", alichokisema ni KWELI kuwa atatufufua na hilo litatimia.

Nina uhakika hata ndugu zetu Waislamu wanatambua kuwa siku ya "kiama", wafu watafufuliwa. Sasa kama ni hivyo, kaburi haliwezi kuwa nyumba ya milele.

Jamani, tubadilike, hasa hasa ninyi mnaojiita viongozi wa dini, acheni upotoshaji! Acheni kuongea ongea vitu kimazoea!
 
Hongera sana kamati ya mazishi ya hayati JPM ikiongozwa na mheshimiwa Majaliwa kwa design nzuri ya kaburi la kuslide kama geti yaani mmefanya professioalism.

Ila mmetunyima haki ya kuona jeneza likishushwa kaburini
nazote hizi nijuhudi za serikali y'a awamu y'a tano
 
..
Mpaka hapa ni maneno tu lakini hakuna hata mmoja anayetupia japo kajipicha tu ili kuhakiki Uzi! [emoji848]

Ulimsikia vizuri CDF Jana? Watu watupie picha ili tuwe mfano wa uimara wa jeshi?
 
Sema hii tabia ya kuficha ficha imenikera sana....pale mazishi ni walikuwepo watu wengi tu walioruhusiwa kama 200 hivi wao waliona kila kitu pale sasa wale kama wakiona kila kitu iweje sisi wengine tusishuhudie kupitia runinga?shida iko wapi?

wananchi tulio mbali tungeharibu nini kama tungeshuhudia jeneza likishushwa na kaburi kufunikwa?mbona kwenye kutupia mchanga tulionyeshwa?
 
Wajuvi wa haya mambo. Mnisaidie mimi mwana wa kwenu huku Chato.
Lile kaburi la muheshimiwa lilikua la aina gani? Je! Lilijengwa pembeni likawekewa reli au ni ule mfumo wa kisasa. Botion kwaajili ya kuokoa muda baadae watalisakafia?
Ule ni uzikaji wa kisasa, kwa wakristo yaani kaburi haliwekwi mchanga, linakuwa kama shimo tu, kunakuwa tayari na funiko, kama tulivyoona pale kwa mheshimiwa hayati.. Na wameweka zile reli ili iwe rahisi kusukuma ili kuziba kaburini.. Hata marehemu Ruge alifanyiwa vile..
 
Kama ndo hivyo nadhani watu wazikwe juu ya miti au mawe makubwa wasifukiwe maana pia mtu amezikwa huko miaka yote hiyo atatokaje chini ya udongo?

Wengine imani zao zinaamini roho ndiyo itakayoinuliwa si mwili. Maana mwili utakuwa umeshaoza.
Wambie mkuu, maana sijui wale walioliwa na mamba wao wangefufukaje.

Tutavikwa mwili mpya usio wa nyama wala usiohitaji pacemaker.
 
Umeandika andiko linalofikirisha sana
 
Hongera sana kamati ya mazishi ya hayati JPM ikiongozwa na mheshimiwa Majaliwa kwa design nzuri ya kaburi la kuslide kama geti yaani mmefanya professioalism.

Ila mmetunyima haki ya kuona jeneza likishushwa kaburini.

Kilichofutikwa ni uvundo
 

Wako Sahihi ,
Mwili utakua hapo kwenye nyumba ya Milele kaburini,
Kwani utapo fufuliwa utafufuka Na mwili mpya hivyo huo utabaki hapo hapo mavumbini milele kumbuka mwili ni nyumba tu ya Roho ,hivyo Roho imeshatengana na mwili
Basi utapofufuliwa Roho itakua kwenye mwili mpya
So ni sahihi kusema Mwili utakua hapo kwenye nyumba ya milele kwani hutafufuka nao Bali mwili mwingine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…