Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
1 korintho 15; 35-38Ktk maandiko na kwa imani ya dini na vitabu vyote, maamdiko hayajaleza waziwazi kuwa wafu watafufuka vp, ila yamesema tu watafufuka... So hapo kwenye kufufuka sisi tuna imagine tu.. Bt Mungu mwenyewe anajua. So hata ufukiwe futi futi 30 kwenda chini, still utafufuka tu.
35Lakini mtu anaweza kuuliza: "Wafu watafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani wakati watakapokuja tena?" 36Hayo ni maswali ya kijinga! Ukipanda mbegu, isipokufa kwanza haitaota. 37Unachopanda ni mbegu tu, labda ya ngano au nafaka nyingine, na si mmea mzima ambao hutokea baadaye. 38Mungu huipa hiyo mbegu mwili anaoutaka mwenyewe; kila mbegu hupata mwili wake wa pekee. 39Miili ya viumbe vyote si sawa. Miili ya binadamu ni ya namna moja, ya wanyama ni ya namna nyingine, ya ndege ni ya namna nyingine na miili ya samaki pia ni ya namna nyingine. 40Iko miili ya mbinguni na miili ya duniani; uzuri wa miili ya mbinguni ni mwingine, na na uzuri wa miili ya duniani ni mwingine. 41Uko uzuri wa jua, wa mwezi na wa nyota; hata nyota nazo huhitilafiana kwa uzuri.
1 korintho 15; 53-55
| 53 | Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. |
| 54 | Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda. |
| 55 | Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? |