GE2025 Aliyekuwa RC Mbeya, Dkt. Juma Homera achukua fomu ya Ubunge Namtumbo

GE2025 Aliyekuwa RC Mbeya, Dkt. Juma Homera achukua fomu ya Ubunge Namtumbo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
KAZI ZA WAKUBWA HUWA ZINALIPA SANA, kuna muda huwa simshangai bwana mwashambwa, wewe endelea kujikuta mtakatifu huku ukisubiria mbingu isiyokuwepo.

Kila la kheri comrade JUMA HOMERA , Vita kawawa tutampa hata viti maalum ikibidi
 
Huyo mikono yake imejaa laana ya damu za Wana Mbeya, yule dogo aliyechana picha ya Rais...yeye kama RC alitoa kauli ya hovyo ya kushawishi mtu kupotezwa na kweli dogo Hadi Leo haonekani, mdude naye amekuwa akitoa kauli za mashaka kuhusu kupatikana kwa mdude. Huyu hafai kuwa mbunge wa wananchi kwasababu hizi chache tu, ukichukua udhaifu wake wote atakuwa hafai hata kuishi na kuchangamana na raia wema mitaani huyu
 
Vita Kawawa yupo pale kwa sababu anatakiwa kuwepo pale, kujalibu kimtoa haiwezekani, Ni Kama kimtoa lizwan jimboni
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Juma Zubeir Homera anatarajia kuchukua Fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Namtumbo Jumamosi June 28.

Dkt. Homera amesema tayari yuko Namtumbo akisubiri zoezi hilo Jumamosi.

"Nitachukua fomu Jumamosi hapa Namtumbo, mengine tutasema wakati ukifika" amesema Dkt. Homera.
View attachment 3384351
Chanzo: Kitenge TV​
Mdude
 
Anataka kupewa Ubunge kwa kazi nzuri ya kusimamia mauaji ya Mdude?
 
Back
Top Bottom