TANZIA Aliyekuwa Sultani wa Mwisho Zanzibar, Sultan Sayyid Jamshid Al Said, Afariki Usiku Huu, Omani

watanganyika ni viherehere sana kwenye mambo ya zanzibar, cha kushangaza sijawahi kuona wazanzibari wakiwa na viherehere kwenyemambo ya Tanganyika
Kuuliza si ujinga, nahitaji kujifunza...

Ni kwanini wazanzibari wanatamani kutawaliwa na sultan?

Sultan alikuwa mzuri kiasi gani kwa wazanzibari hadi waone hakustahili kuondoshwa?
 
Kuuliza si ujinga, nahitaji kujifunza...

Ni kwanini wazanzibari wanatamani kutawaliwa na sultan?

Sultan alikuwa mzuri kiasi gani kwa wazanzibari hadi waone hakustahili kuondoshwa?

Kwa kifupi tu Zanzibar ilikuwa na maisha bora kipindi cha utawala wa Sultan, ilikua imeendelea sana ukilinganisha na nchi nyingi za jirani, wabara walikuwa wanazamia Zenj kama vile ulaya.
Hali chini ya utawala wa CCM imekuwa ni mbaya sana hivi sasa wazenj wanavamia bongo kutafuta maisha bora. ndio mana hawaachi kumkumbuka Sultan. ni kama vile Libya wanavyolia na kumkumbuka Gaddafi.
CCM ni zaidi ya masultani kwa vile tu tunawona weusi wenzetu tunawachukulia poa.

Jengine Wazanzibar wanawachukulia ma sultan ni kama wananchi wenzao amabapo view ya watanganyika kwa ma sultan wanaowaona kama ni wakoloni kitu ambacho sio sahihi, masultan walikuwa raia halali wa zanzibar na sio wakoloni. Watanganyika walio wengi wana uduwanzi wa akili wakuwaona kila mtu mweupe kuwa sio raia hata kama amezaliwa kwenye hii nchi, at the same time walishangiria Obama alipokuwa raisi U.S. Nchi nyingi jamii ya zanzibar ambazo zina muingiliano mkubwa wa jamii tofauti hakuna mambo kama hayo hata ukienda Mauritius seashells pia, watu wa jamii na rangi tofauti wanaishi kwa pamoja bila ya shida na wote wanajitakidi kama ni wamoja.
 
Huyu si umesema anazikwa Muscat?
Alo,kama Seyyid Said hakutoka Oman,alitoka wapi?

Kuzikwa Oman hakukufanyi wewe kuwa Mu Oman.
Na Sayyid Said kutoka Oman kunamfanaje Jemshid naye kuwa Mu Oman? wewe una uhakika kuwa babu yako wa 6 alizaliwa Tanganyika? Mbona unajita mTanganyika?
 
Tunauliza atazikwa wapi? Kwa maana yule ni mzanzibar, mzaliwa wa zanzibar na zanziba ni home land yake japo huko oman alikimbilia ukimbizini alikotoka babu wa babu zake sultan seyyid said aliyekuja kuishi zanzibar na kuwa sultan wa kwanza wa zanzibar

Mkuu taratibu za Uislmau huwa unazikwa unapofia, Na hasa kwa waarabu huwa hawatoki kwenye misingi
 
Undani wa Sultani Jamshid Abdullah akiwa skuli Unguja, shule tajwa ya St. Victoria mjini Alexandria Misri kisha American University mjini Beirut Lebanon na baadaye kuandikishwa katika jeshi la majini la Uingereza alikotumika kama baharia kwa miaka miwili.


View: https://m.youtube.com/watch?v=x56Fv6h3dvg
Akarejea nchini Zanzibar na chini ya uangalizi wa babu yake akaelekezwa jinsi ya kuongoza dola ikitokea atakuwa Sultani, mamlaka yake yapo vipi, wajibu wake kwa raia wa kizanzibari ni upi, haki za raia wa kizanzibari...
 
Aliitawala Zanzibar ila akaja kufurushwa kwa mapinduzi, akakimbilia uzunguni alikoishi kwa kipindi hatimaye akahamia Uarabuni huko Oman....

Jamshid bin Abdullah, the last Sultan of Zanzibar died on December 30, 2024, in Oman after a prolonged illness and advanced age. He died at Sultan Qaboos Royal Hospital in Muscat, members of the royal family said.
He was buried at the royal family cemetery in Muscat.

Abdullah was Sultan until the 1964 revolution, which toppled his government and forced him to flee to Britain, where he lived in Portsmouth with his family for 56 years before moving to Oman on September 15, 2020.

Born in Zanzibar on September 16, 1929, Sultan Jamshid acquired primary education on the islands, then Egypt, and later in the United Kingdom. He served in the British Royal Navy for two years before returning to Zanzibar.
 
leo ndio maadhimisho ya kwanza ya Mapinduzi ya Zanzibar bila Sultan of Zanzibar duniani!。
Mwana JF, Paskali, anakutakia wewe na familia yako HERI YA SIKUKUU YA MAPINDUZI MATUKUFU
YA ZANZIBAR!
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…