Kwa sasa mjadala mkubwa ni juu ya "mkora" mpya wa taifa aliyetaka kupiga Trilioni 1.2 kupitia Jeshi la zimamoto. Hii ni moja ya skendo kubwa kuwahi kutokea. Ile ya Richmond iliyomuondoa Lowassa ilikuwa Bil.133, ile ya Escrow inayowatesa akina Ruge na Singasinga ni Bil.380. Hii ya Kangi ni kubwa kuliko.
Rais Magufuli aliliambia taifa kuwa Kangi alisaini mkataba wa mkopo kutoka Romania ili kununua vifaa vya jeshi la zimamoto. Alifanya hivyo akijua hana mamlaka hayo kisheria. (Tabia za wakora).
Mbaya zaidi walivizia Mwanasheria mkuu wa Serikali Dr.Adelarus Kilangi alipofiwa na mkewe ndio wakaenda kusaini mkataba. Huu ni ukora wa Unga Ltd.
Kangi hakupaswa kuwa uraiani kwa sasa. Alitakiwa apumzike Keko akisubiri mashtaka ya uhujumu uchumi. Trilioni 1.2 ni 4% ya bajeti ya nchi. Sasa fikiria kikundi cha wakora wachache kinataka kula peke yake. Je zingefanya nini kama zingewekwa kwenye miradi ya maendeleo?
Bil.133 ilimchafua Lowassa na kuzima ndoto zake za Urais. Akaitwa fisadi, akatukanwa, akabezwa. Lakini huyu aliyetaka kupiga mara 10 zaidi yake hajachukuliwa hatua yoyote.
Hii si mara ya kwanza Kangi kutuhumiwa kwa makosa ya kimaadili. Mwaka 2016 yeye na wabunge wenzie Sadiq Murad (Mvomero) na Victor Mwambalaswa (Lupa) walifikishwa Mahakamani Kisutu kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Mil.30 kutoka kwa DED wa Wilaya ya Gairo, Mbwana Magote.
Mwaka 2019 CAG alisema jeshi la polisi lilipewa Bilioni 16.6 kwa ajili ya kununua sare lakini hazikununuliwa. Kangi alisimama bungeni na kusema zimenunuliwa. Akadai kama itathibitika hazikununuliwa atatembea bila nguo (Tabia za wakora).
Hoja hiyo ikazimwa maisha yakaendelea. Lakini leo kamati ya bunge ya PAC imesema kuwa Lugola alidanganya kuhusu sare hizo. Halima Mdee ameomba iundwe kamati teule kufanya uchunguzi.
Lugola alitumia madaraka yake kunyanyasa watumishi wa chini yake hasa askari magereza na askari polisi. Aliwahi kumfukuza Kamishna Jenerali wa jeshi la magereza Dr.Juma Malewa kama mtu anayefukuza inzi kwenye chakula.
TAKUKURU wameanza uchunguzi wa tuhuma dhidi yake. Nashauri ashtakiwe kwa uhujumu uchumi ili iwe fundisho kwa wakora wengine wanaojificha kwenye kivuli cha uzendo na ilani ya chama!
Credit G malisa