Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola adaiwa kuwa chini ya ulinzi

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola adaiwa kuwa chini ya ulinzi

Bado wale wanaounga mkono juhudi, ipo siku watakamatwa. Chama Cha kishetani ndivyo kilivyo!!!!
 
Wakuu, nimepata taarifa hivi punde kuwa Aliekua Waziri wa mambo ya ndani Ndg Kangi Lugola amekamatwa na Jeshi la Polisi. Je habari hizi ni za kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
.
IMG-20200130-WA0011.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Takukuru wa anza kazi ya kumchunguza kangi lugola kutokana na manunuzi ya vifaa vya jeshi la zima moto kutiliwa mashaka kuwa na ubadhifu wa pesa za serikali.

Hatua hiyo imekuja baada ya kauli ya raisi JPM kuikabidhi kesi hiyo katika tasisi ya kupambana na rushwa siku ya makabiziano ya nyumba za mageleza.

CHANZO: Cloudsfm

. Kangi Lugola awekwa kizuizini na ...ri ya raisi JPM https://youtu.be/xRMfaQSxjbU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Takukuru wa anza kazi ya kumchunguza kangi lugola kutokana na manunuzi ya vifaa vya jeshi la zima moto kutiliwa mashaka kuwa na ubadhifu wa pesa za serikali.

Hatua hiyo imekuja baada ya kauli ya raisi JPM kuikabidhi kesi hiyo katika tasisi ya kupambana na rushwa siku ya makabiziano ya nyumba za mageleza.

CHANZO: Cloudsfm

. Kangi Lugola awekwa kizuizini na Takukuru/ Tunaitekeleza amri ya raisi JPM

Sent using Jamii Forums mobile app

Sioni jipya hapo zaidi ya Unafiki na kutaka Kuwafanya Watanzania wote ni Mambumbumbu.
 
Takukuru wa anza kazi ya kumchunguza kangi lugola kutokana na manunuzi ya vifaa vya jeshi la zima moto kutiliwa mashaka kuwa na ubadhifu wa pesa za serikali.

Hatua hiyo imekuja baada ya kauli ya raisi JPM kuikabidhi kesi hiyo katika tasisi ya kupambana na rushwa siku ya makabiziano ya nyumba za mageleza.

CHANZO: Cloudsfm

. Kangi Lugola awekwa kizuizini na Takukuru/ Tunaitekeleza amri ya raisi JPM

Sent using Jamii Forums mobile app

Kumbe Takukuru hivi sasa inafanya kazi kwa maagizo ya Mheshimiwa Rais?

Ina maana kama Rais hataki uchunguzi ufanywe dhidi ya raia fulani, hata kama raia huyo amethibitika kufanya uhalifu huo, Takukuru haitafanya uchunguzi huo?

Haya ni maajabu yanayopatikana Tanzania pekee!
 
Yanayofanywa na Ccm miaka hii inakumbusha marehemu raisi samora machel Wa msumbiji aliwa kuja Tanzania kwenye sherehe za Ccm ambazo Ccm walikuwa wanapenda kuaandàa magwaride na michezo ya halaiki ya kisekta za ulinzi utamaduni kilimo viwanda na michezo ile ilikuwa inachezwa na wanafunzi waliopewa jina la chipukizi Wa Ccm na hao ndio kizazi cha kina jiwe na ,lugola . marehemu samora jioni alivyorudi ikulu alikaza roho akamuuliza marehemu nyerere hivi kwanini unatumia mafunzo ya kijeshi kwa watoto unaotaka wawe wanachama Wa Ccm haya mambo yanawasaidia nini kama nchi kuwangiza katika kujenga mawazo ya siasa badala ya kuwaimarisha fikra za uzalishaji na kujitegemea .mwl alikasirika hakumjibu akaenda kulala akamwacha samora sebuleni . alichofanya samora akawasha video akachukua mkanda Wa vide Wa sherehe zile akawa anaangalia ilivyofika gwaride la chipukizi linatembea gwaride mwendo Wa haraka na muziki Wa brass bendi ukawa unapigwa samora akawa anaulisha maneno ile nyimbo akawa anaimba ile wimbo anasema
Tazama kapanya kadog
tazama kapanya kadogo kanateembea
Tukamuuliza akasema vyama vyetu vya Ccm na frelimo vina viongozi waizi na waopenda kula kama panya na kutia hasara jamii sasa hivi nikiangalia Ccm inaazidi kuandaa panya wadogo wakikuwa wakubwa hawa utaniambia!
Leo ndio naona ya kina lugola waliokuwa chipukizi Wa miaka ya 77 hawa ndio walikuwa panya wadogo wanatembea tembea kwenye viunga vya siasa
 
"Sijawahi kumwona CAG mwongo kama Profesa Assad" ... Kangi Lugola, 2019.
 
Mkuu hii stori ni kweli au umetunga?
 
Kumbe Takukuru hivi sasa inafanya kazi kwa maagizo ya Mheshimiwa Rais?

Ina maana kama Rais hataki uchunguzi ufanywe dhidi ya raia fulani, hata kama taia huyo amethibitika kufanya uhalifu huo, Takukuru haitafanya uchunguzi huo?

Haya ni masjabu yanayopatikana Tanzania pekee!
Ndio. Huoni issue ya makontena ya Makonda haikuchunguzwa wala kuongelewa tena?
Baba hakuamuru mwanae achunguzwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumekuwa tukiwaona Hao wengine mfano wakina ruge... Tito... Kabendera etc walinyakuliwa juu juu na kuwekwa lupango hku uchunguzi ukifanyika wao wakiwa ndani
Kwanini Sasa Hawa mpaka sahv wako uraiani
Au ndiyo double standard, alikuwa denti wangu

Ova
Ndio. Huoni issue ya makontena ya Makonda haikuchunguzwa wala kuongelewa tena?
Baba hakuamuru mwanae achunguzwe

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAKUKURU nao watumbuliwe, hawafanyi kazi yao ya KUZUIA Rushwa, wamekua kama polisi NAO WANASUBIRI WAPELEKEWE AMRI ZA KUCHUNGUZA NA KUPELELEZA.

HII taasisi sijawahi kuelewa majukumu na wajibu wao ni nini. Kwanini isichunguzwe? Rushwa imeongezeka na ipo kila kona, sasa wao wanafanya nini?
Rais ndiye kawa Takukuru na Takukuru ndio wamekuwa RAIS. Yani mpaka rais aseme pale kuna rushwa nendeni mkachunguze, wao primary job yao ni ipi?!
 
Kwa sasa mjadala mkubwa ni juu ya "mkora" mpya wa taifa aliyetaka kupiga Trilioni 1.2 kupitia Jeshi la zimamoto. Hii ni moja ya skendo kubwa kuwahi kutokea. Ile ya Richmond iliyomuondoa Lowassa ilikuwa Bil.133, ile ya Escrow inayowatesa akina Ruge na Singasinga ni Bil.380. Hii ya Kangi ni kubwa kuliko.

Rais Magufuli aliliambia taifa kuwa Kangi alisaini mkataba wa mkopo kutoka Romania ili kununua vifaa vya jeshi la zimamoto. Alifanya hivyo akijua hana mamlaka hayo kisheria. (Tabia za wakora).

Mbaya zaidi walivizia Mwanasheria mkuu wa Serikali Dr.Adelarus Kilangi alipofiwa na mkewe ndio wakaenda kusaini mkataba. Huu ni ukora wa Unga Ltd.

Kangi hakupaswa kuwa uraiani kwa sasa. Alitakiwa apumzike Keko akisubiri mashtaka ya uhujumu uchumi. Trilioni 1.2 ni 4% ya bajeti ya nchi. Sasa fikiria kikundi cha wakora wachache kinataka kula peke yake. Je zingefanya nini kama zingewekwa kwenye miradi ya maendeleo?

Bil.133 ilimchafua Lowassa na kuzima ndoto zake za Urais. Akaitwa fisadi, akatukanwa, akabezwa. Lakini huyu aliyetaka kupiga mara 10 zaidi yake hajachukuliwa hatua yoyote.

Hii si mara ya kwanza Kangi kutuhumiwa kwa makosa ya kimaadili. Mwaka 2016 yeye na wabunge wenzie Sadiq Murad (Mvomero) na Victor Mwambalaswa (Lupa) walifikishwa Mahakamani Kisutu kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Mil.30 kutoka kwa DED wa Wilaya ya Gairo, Mbwana Magote.

Mwaka 2019 CAG alisema jeshi la polisi lilipewa Bilioni 16.6 kwa ajili ya kununua sare lakini hazikununuliwa. Kangi alisimama bungeni na kusema zimenunuliwa. Akadai kama itathibitika hazikununuliwa atatembea bila nguo (Tabia za wakora).

Hoja hiyo ikazimwa maisha yakaendelea. Lakini leo kamati ya bunge ya PAC imesema kuwa Lugola alidanganya kuhusu sare hizo. Halima Mdee ameomba iundwe kamati teule kufanya uchunguzi.

Lugola alitumia madaraka yake kunyanyasa watumishi wa chini yake hasa askari magereza na askari polisi. Aliwahi kumfukuza Kamishna Jenerali wa jeshi la magereza Dr.Juma Malewa kama mtu anayefukuza inzi kwenye chakula.

TAKUKURU wameanza uchunguzi wa tuhuma dhidi yake. Nashauri ashtakiwe kwa uhujumu uchumi ili iwe fundisho kwa wakora wengine wanaojificha kwenye kivuli cha uzendo na ilani ya chama!

Credit G malisa

FB_IMG_1580437457158.jpg
 
Back
Top Bottom