Wakati mwingine unaweza kupata kazi sana kum-support Jiwe,anafanya mambo kinyumenyume sana mpaka unashindwa kuelewa nia yake hasa katika haya mambo ya rushwa ipo wapi??Maana tukumbuke huyu mtu naye atatoka madarakani,na nchi yetu itabaki.Ina miaka mitano tu mbele...maana ni hakika kwa mfumo wetu,huo mwezi October atashinda tu.
Huyu Kangi Lugola hakupaswa kabisa kuwepo kwenye hilo baraza na hii Wizara,huyu na Mwambalaswa na yule Mbunge wa Morogoro Mvomelo,walikutwa na shutuma za rushwa,kesi ikaisha kiajabu ajabu ili kutokukichafua chama,huyohuyo Lugola tena unampa wizara unategemea nini??
Halafu kwa sasa,ili kiongozi wa Serikali asafiri nje ya nchi,ni lazima awe na kibari cha Kutoka Msajili wa Hazina na Ikulu.Msajili wa Hazina anajiridhisha kuwa safari hiyo ina manufaa kwa nchi na haitaigharimu serikali pesa nyingi,kama safari inahusisha nauli,per diem n.k toka serikalini,msajili lazima ajiridhishe kuwa jambo hilo lina manufaa kwa nchi.
Hawa wa ngazi za kina Kangi Lugola,Katibu Mkuu na wengine wenye uteuzi wa ki-Rais,Mzee lazima ajue wanatoka nje ya nchi.Kwa wizara kama ya Mambo ya ndani ambayo ni ya Kiulinzi,Waziri kila siku kabla hajalala lazima afikishe report ya mambo ya usalama wa raia na nchi.Sasa kama alienda safari zote huko Romania huyu Jiwe hakujua??Yaani mpaka unasainiwa mkataba yeye hakuwa na taarifa??
Kama hakuwa anajua lolote,basi hapa tatizo kubwa ni Jiwe na hawa kina Kangi na Andengenye ni "bangusilo" tu.
Inashangaza sana.Ile hotuba ya Rais mwenye vyombo vyote anaishia kulalamika,analialia mbele ya Raia...Mzee kama Rais unatakiwa usilielie,toa suluhisho,ukiona wizara inakutesa ujue wewe pia umeshindwa?Inaposhindwa Wizara ujue na Rais kashindwa...Hii ndio dhana ya "Collective Responsibility"