Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
TUKIO la mtoto wa mwaka mmoja na nusu kudaiwa kunyongwa hadi kufa na msichana wa kazi limechukua sura mpya baada kuhusishwa na imani za kishirikina huku ikidaiwa kuwa ni tukio lake la tatu.
Wakizungumza jana na Nipashe kwa nyakati tofauti, majirani wa eneo la tukio walizungumzia mazingira ya mauaji hayo huku Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkeriyani, Kata ya Olasiti jijini Arusha, Aminiel Mollel, akitoa tahadhari kwa waajiri kufahamu mazingira wanapotokea wasaidizi hao.
Mollel alisema alipata taarifa ya tukio hilo na kwenda kumchukua mtoto huyo hadi Hospitali ya Mount Meru, ambako baada ya uchunguzi waligundua ameshafariki dunia.
“Katika kumhoji msichana wa kazi alisema huyo ni mtoto wa tatu kumnyonga na wakati anamnyonga hakuwa na akili yake, lakini akishamaliza ndiyo inarudi, tunafikiri ni nguvu za giza zinamwendesha kufanya matukio haya,” alisema mwenyekiti huyo.
“Watu walipofika nyumbani walimkuta anaosha vyombo kama hakuna kilichotokea,” alisema.
Mwenyekiti huyo, aliwashauri wazazi na walezi kuwaajiri wasaidizi wanaojulikana mazingira waliyotokea ili kuwafahamu kabla ya kuwaleta majumbani mwao.
Mmoja wa majirani aliyejitambulisha kwa jina moja la Natalia alisema taarifa za kuuawa kwa mtoto huyo walizipata Juni 19, mwaka huu, majira ya saa 4: 00 asubuhi wakati mama wa mtoto alipokuwa ameshaenda kazini.
"Mama yake huwa amezoea kumwandalia kila kitu mwanawe, kabla ya kuondoka kwenda kazini anahakikisha amempikia na kumwogesha mtoto ndio amwachie binti huyu, na alikuwa akifanya hivyo kwa kuwa msichana alikuwa mdogo na pia alikuwa bado mgeni, tangu aje alikuwa na wiki mbili tu hapa," alisema Natalia.
Jirani mwingine ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Rose, alisema mtoto wake aliitwa na msichana huyo wa kazi akimwambia kuwa haelewi kwanini mtoto haamki anapomuamsha jambo lililomfanya mtoto huyo akimbie kumuita.
"Nilikuja kumwona mtoto ikabidi nimwangalie joto la mwili lilikuwa bado lipo, lakini mtoto alikuwa hafanyi chochote nikambeba na kumtoa nje, tukaangalia tukaona shingoni kwekundu na kama kumenyofolewa nyofolewa,” alisema na kuongeza;
“Nilimuuliza dada mtoto amefanyeje kwa haraka nilidhani labda zipu ya nguo imemuumiza, lakini alinyamaza huku akiendelea kuosha vyombo…ni tukio baya sana inauma sana,” alisema jirani huyo.
Naye mama mkubwa wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Judith, alidai baada ya binti huyo kumnyonga mtoto aliendelea na shughuli zake za kufua bila kujali tukio hilo.
“Mtoto aliyenyongwa alizaliwa njiti na nilimlea mwenyewe tangu hospitalini hadi kuletwa nyumbani, walikaa kwangu na baadaye walirudi kwao,” alisema.
"Awali, ilisikika kelele ya kilio kikali kimoja kabla ya mtoto kufariki na jirani mmoja alipofika kuuliza shida iliyomfanya mtoto kuangua kilio alijibiwa na binti kuwa alikuwa anampa uji, hivyo mtoto hana shida amelala," adai Judith.
Alisema baada ya tukio hilo baba mwenye nyumba alimuita msichana huyo na kumuuliza chanzo cha tukio hilo, na alidai kukiri kumnyonga mtoto na kwamba ni tukio lake la tatu, mengine akidaiwa kuyafanya kwenye maeneo mengine aliyowahi kuishi.
"Binti huyu alipoletwa takribani wiki mbili sasa nilimuuliza mdogo wangu mbona huyu msichana ni mdogo ataweza kuishi na mtoto, alinijibu kuwa hata yeye ameona kuwa ni mdogo hivyo anafanya harakati za kumrudisha nyumbani kwao ili watafute mwingine, lakini katika hatua za kuendelea kumwandalia mazingira ya kumrejesha kwao ndio yametokea haya," alisema.
Baba mkubwa wa marehemu Amedeus Benedict, alisema marehemu Tifan Oswald ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia ya Oswald na mazishi yanafanyika leo mkoani Kilimanjaro ambako ni chimbuko la wazazi wake.
Mtuhumiwa huyo ambaye jina limehifadhiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa upelelezi.
Chanzo: Nipashe