BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wakuu, naona kama Watu wengi pamoja na Taasisi ya MOI wamejielekeza na kutupia lawama upande mmoja wa Mgonjwa aliyeonekana akimbusu mpenzi wake Wodini. Kimsingi hakuna kosa lolote alilofanya pale, na sidhani kama kuna sheria inazuia jambo hilo. Labda kama aliyefanya naye kitendo kile ni mtoa huduma za afya katika Taasisi hiyo.
Yule Mgonjwa amevunjiwa Haki zake za Faragha kwa Kurekodiwa na Kusambazwa kwa Video ile. Nategemea Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) watachukua hatua kwa aliyerekodi na kusambaza video hiyo mtandaoni. Kitendo hicho ni ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwasababu Mgonjwa amerekodiwa bila ridhaa yake na pasipokujua.
Aidha aliyesambaza mtandaoni pia amevunja sheria ya makosa ya mtandao. Hivyo anapaswa kuwajibishwa kwa kusambaza maudhui yasiyopaswa kuwepo mtandaoni. Hapa mamlaka zisikwepe hili jambo, na pia mamlaka zikumbuke pia zenyewe zinapaswa kuwa mfano wa kulinda haki za faragha za wagonjwa na raia yeyote.
Itashangaza sana hili jambo likiishia upande mmoja wa mgonjwa kuonekana amekosea wakati yeye ndiye amekosewa pale kwa kuingiliwa faragha yake.