Uchaguzi 2020 Aliyemshauri Lissu baada ya kuadhibiwa na NEC anaweza kuendelea na shughuli za chama amemshauri vibaya

Kwa hiyo unataka kutuaminisha hata Raisi anakosea sasa hivi pale anapoendelea kufanya shughuli za urais wakati yuko kwenye kipindi cha kampeni? maana yake naye anafanya kampeni kwa sababu huwezi tenganisha mtu kwa nafasi mbili

Waliofikiri kama wewe ndiyo wale tunao waitaga POYOYO

leta hoja za maana siyo tunapoteza muda wetu kusma utumbo

wewe ndiyo mwenye ushauri mbaya sasa
 
Hakuna chochote. Leo nimemuona Charles Hillary wa Azam News akimhoji mwanasheria wa NEC na mjumbe wa kamati ya maadili bwana Kawishe kuhusiana na matembezi anayofanya Lissu hasa matukio ya leo 07 Oktoba kama amekiuka sheria za uchaguzi, lakini majibu yalikuwa kama ifuatavyo; "Lissu hajakiuka sheria kwani hajafanya kampeni"
 

Unataka kutuambia akizuiwa kufanya kampeni asiende sokoni kununua mahitaji yake au NEC watakuwa wanamnunulia.
Ndugu yangu umeandika sana lakini ufahamu kuwa Mbowe na timu yake wanafanya makusudi ili Lissu aangamie moja kwa moja.Mbowe ni smart,anajua Lissu ni mpenda Sifa na atalipokea hilo kwa haraka bila kufikiria athari zake.Kwa ujumla hawamtaki.
 
Aahaa tangu lini Mamba akamshauri Swala avuke mto wenye Mamba kusudi asijeliwa na SImba upande aliopo? ahaa kumbe imewauma saana kesho anaenda kumkatia ticket ya basi shangazi yake anayeelekea Singida, alikuja kumtembelea na kumpa pole ya kupigwarisasi..sipati picha sasa hivi Mamlaka zinavyochanganyikwa na maagizo kutoka chama tawalaili kumzuia kesho asienda ubungo kwa visingizio vya kusababisha msongamano usiokuwa na haja ...changamoto waliyonayo ni kwamba hawajui atakwenda saa ngapi au anaweza asiende kesho au akaenda usiku pia ahaa...yaani hizi akili ni balaa
 
Polisi kwa Lissu washalegea kwa bao 3 bila tayari.
Polisi wamdhuru Lissu kwani wao hawajipendi na familia zao?
Usiwaingize chaka wenzio ndugu!!
 
Ushauri wako ungekuwa na mashiko kama usingeonyesha wazi kuwa unamfanyia Mtu fulani kampeni.

Rudi tena ulikotoa au ulikopatia bandiko lako kisha uje kivingine.

Mimi ningekushauri kitu kimoja: Ingekuwa ni busara kama ungeweza kumshauri yule aliyeleta utengano kwenye Taifa letu. Watangulizi wake wote waliweza kutuweka pamoja kama Watz bila kujali tofauti zetu za Kisiasa Kikabila na Kidini.

Siasa ilikuwa na ladha yake hasa ktk kipindi kama hiki cha kampeni. Lkn kwa sasa wewe mwenyewe ni shahidi kwa yanayoendelea hivi sasa. Yaani ni uadui chuki na hata visasi.

Ushauri wangu ni kwamba kwa sasa kinachohitajika kutumiwa na Watendaji wote wa Serikali/Vyombo vya Dola pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni BUSARA NA SI VITISHO/UBABE kuliko wakati mwingine wowote.

Watz wengi wameumizwa sana ktk Uongozi wa awamu ya tano. Hivyo wengi wana majeraha mioyoni mwao. Hivyo kundi kubwa liko tayari kwa lolote kwani hivi sasa wamechoka kudharauliwa.
 
Kwa mtazamo wako, Leo Rais wa Malawi amekutana na Magufuli Kama "Mwenyekiti wa CCM" au Kama "Rais wa Tanzania??"
 
Ndugu yangu umeandika sana lakini ufahamu kuwa Mbowe na timu yake wanafanya makusudi ili Lissu aangamie moja kwa moja.Mbowe ni smart,anajua Lissu ni mpenda Sifa na atalipokea hilo kwa haraka bila kufikiria athari zake.Kwa ujumla hawamtaki.
Am smart too.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…