Uchaguzi 2020 Aliyemshauri Lissu baada ya kuadhibiwa na NEC anaweza kuendelea na shughuli za chama amemshauri vibaya

Tusiyumbishane waTanzania.
NEC tunawaombeni muandae MDAHALO wa wagombea URAIS wote haraka iwezekanavyo tuwasikilize ndipo tuwe na maMuzi. Hii zuia zuia mara mapumziko ni ujanja ujanja tu. Na wawe live bila kukatakata mdahalo huo.
 
Kama Tundu Lissu ameshauriwa vibaya si ndio itakuwa faida kwenye CCM?Badala ya kufurahi mpinzani wako ameshauriwa vibaya wewe upate faida,kwanini unakuja kulialia hapa ?
 
katika maisha ukiwa unajifanya mjuaji sana, watu wanakuekea kitu kinaitwa ENVY, short code ya mikosi: hakuna mtu anapenda kua inferior zaidi ya mwenzake lakni ukijishusha automatically Binadam wanakupandisha wenyewe kwa sababu wanajiona kama wamekufundisha kuishi, hata kwenye Biblia imeandikwa: Ukijishusha Anakupandisha, Ukijiona sana Anakushusha tena kwa aibu!

Hebu ngoja tuangalie kauli za Mkuu mmoja mnyenyekevu na anaependa kujishusha mbele za watu:

Wananchi:Mzee huku Geita tuna janga la njaa.

Mh:Mlitaka mimi nije niwapikie.

Suala la Korosho:

Mh:Mngewaacha wajiletee kimbelembele,ningepiga shangazi zake.

Wananchi:Tunasubiri kujua hatma yetu khs janga hili la tetemeko mzee.

Mh:Nyie wa bukoba mtetemeke tu,serikali haikuleta tetemeko hapa.

Wananchi:Mzee pesa ya kupanda pantoni ni nyingi?

Mh😛igeni Mbizi
 
Lisu ana kiburi, makusudi na ujuaji

Dawa ya wakaidi mithili ya Lisu ni kuchukuliwa hatua zaidi na zaidi
Ili upambane na Ukaidi,ni vyema nawe ukawa mkaidi kwa mambo kadhaa.
 
Lissu anayajua hayo yote anatumia loop holes za watunga sheria kuwafundisha sheria hapa ametengeneza precedent ambayo hawakuitarajia ni jambo la kufikirisha kisheria, serikali yetu haina watu makini.
Hiyo advantage wanayo pia ccm na huitumia vyema na pengine kwa kuifuja kabisa. Kwakuwa mgombea wao ndo rais na hatuwezi kumtenga na urais, basi gharama na uratibu shughuli zake hubebwa na serekali, chama kinaongezea tu.
 
Hakuna chochote. Leo nimemuona Charles Hillary wa Azam News akimhoji mwanasheria wa NEC na mjumbe wa kamati ya maadili bwana Kawishe kuhusiana na matembezi anayofanya Lissu hasa matukio ya leo 07 Oktoba kama amekiuka sheria za uchaguzi, lakini majibu yalikuwa kama ifuatavyo; "Lissu hajakiuka sheria kwani hajafanya kampeni"
Wanaotaka asitoke naona wanalinganisha adhabu alipewa kuwa sawa na kifungo cha nyumbani, kitu ambacho si sahihi. Imenikumbusha kule Uganda Mseveni alipombana mpinzani wake kwa kumnyima upenyo wa kufanya siasa, Besigye akabuni alibuni kitu kinacho itwa "walk to work" iliyopa umaarufu mkubwa. Watu waliunga mkono mkono wakawa wanatembea kwa mguu kwenda makazini.
Matokeo yake jamaa alipigwa kifungo cha nyumbani rasmi.
 
Amesimamishwa kufanya kampeni ya uraisi na sio shughuli za siasa. Ili asimpiku mgombea wa ccm yaani amelazimishwa kupumzika ili kupunguza speed
 
katika maisha ukiwa unajifanya mjuaji sana, watu wanakuekea kitu kinaitwa ENVY, short code ya mikosi: hakuna mtu anapenda kua inferior zaidi ya mwenzake lakni ukijishusha automatically Binadam wanakupandisha wenyewe kwa sababu wanajiona kama wamekufundisha kuishi, hata kwenye Biblia imeandikwa: Ukijishusha Anakupandisha, Ukijiona sana Anakushusha tena kwa aibu!
Nyie mlivyompiga risasi ndo mlijishusha sio??
 
Kuna tofauti ya kujifanya unajua sana na kuwa unajua sana.
katika maisha ukiwa unajifanya mjuaji sana, watu wanakuekea kitu kinaitwa ENVY, short code ya mikosi: hakuna mtu anapenda kua inferior zaidi ya mwenzake lakni ukijishusha automatically Binadam wanakupandisha wenyewe kwa sababu wanajiona kama wamekufundisha kuishi, hata kwenye Biblia imeandikwa: Ukijishusha Anakupandisha, Ukijiona sana Anakushusha tena kwa aibu!
 
Lissu hakuwekwa kizuizini asitoke nje. Hakuambiwa asitoke au asiende popote. Sasa ukaidi ni upi. Mbona watu wapenda sana kujenga hoja za kiwivu wivu tu.
Ina maana angeenda kujifungia ndani aangalie TBC1

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Imeandikwa, kiburi si maungwana na mtoto mkaidi hawezi kufaidi hadi siku ya Iddi. Tundu Lissu anaingia katika kundi hili kwa kushauriwa vibaya au kukaidi ushauri mzuri.

1. Aliemshauri Lissu kuwa baada ya kuadhibiwa na Kamati ya Maadili ya NEC anaweza kuendelea na shughuli za Chama kama Makam Mwenyekiti wa Chama amemshauri vibaya.

Tundu Lissu ni mmoja, hakuna nafsi mbili ktk mtu mmoja. Popote atakapokuwa Tundu Lissu ndipo alipo Mgombea wa Urais wa Chadema na Makam wa Mwenyekiti wa Chadema. Hakuna mstari wowote wa kutenganisha kati ya Lissu Mgombea na Lissu M/Mwenyekiti.

Kukosekana kwa tofauti hiyo ndio maana popote alipo mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli ndipo alipo Rais wa JMT. Huwezi kuutofautisha ugombea wa John Pombe Joseph Magufuli na Urais wake au Uenyekiti wake wa CCM. Hivyo hivyo huwezi kuutofautisha ugombea wa Tundu Lissu na Umakam Mwenyekiti wake vinginevyo ni kujidanganya tu.

Aliemshauri Lissu kuwa baada ya kuadhibiwa anaweza kuendelea na kazi za kisiasa amemdanganya, amemshauri vibaya na amempotosha bure. Anachagiza vurumai za bila sababu. Lissu ashauriwe vizuri, ugombea wake na Umakam Mwenyekiti wake ni alfa na Omega, huwezi kuvitenganisha. Kimoja kinaathiri kingine!

2. Aliemshauri Lissu kuwa, kufungua matawi ya Chama au kutembelea masoko sio shughuli za Kampeni amemshauri vibaya, amemdanganya. Ni bahati mbaya kuwa Lissu licha ya kuwa Mwanasheria amedanganyika kirahisi mno. Mazingira na wakati vinanguvu zaidi ktk kuamua kesi, Lissu anafahamu hilo. Hakuna mstari wowote unaotenganisha kufungua matawi ya chama, kutembelea masoko na shughuli za Kampeni kwa wakati huu. Wakati uliopo sasa na mazingira anayokwenda kutembelea Tundu Lissu ni ushahidi wa wazi kuwa ameamua kufanya kampeni kwa mlango mwingine. Ni kosa, ni ukaidi.

Kampeni ni hamasa, kampeni ni ushawishi. Kufungua matawi ya vyama ni hamasa na ushawishi kuwa Chama kipo hai, hii ni kampeni zaidi kuliko kufanya mkutano wa hadhara.
Kuwatembelea watu ktk soko na maeneo ya wazi ni hamasa na ushawishi pia. Watu waliosoma elimu maalumu watanielewa vzr hapa kwamba kuna lugha ya picha na alama. Unaweza kufika mahala bila kuongea jambo lolote, ukasabahi kwa ishara na kuondoka lkn mavazi yako na muda vika-deliver ujumbe uliokusudiwa kwa watu. Kwenda Kibaha, kukutana na Wanachama au Wananchi hata bila kuongea jambo lolote ni kampeni kwa Lissu. Kati ya nafasi ya Umakam Mwenyekiti na nafasi ya Ugombea Urais kwa Lissu inayotangulia kwa sasa ni ya Ugombea. Hii ni principle ya wakati!!

Ushauri:

1. Mwambieni Tundu Lissu akili nyingi mbele ni giza. Awasikilize wenzake, aachane na mpango huu hauna faida. Polisi watamzuia kwa sababu hawawezi kutofautisha Ugombea wake na Umakam Mwenyekiti wake. Sio Polisi tu, hata wewe huwezi kwa sababu hakuna tofauti hiyo.

Polisi ndicho chombo chenye dhamana ya kusimamia na kushurutisha utekelezaji wa sheria. Ninahisi wataendelea na kusimamia utaratibu huu bila kujali kwa sababu ni wajibu wao, tusiwalaumu.

2. Mwambieni Tundu Lissu aache kukifanya kichwa chake kigumu, kitavunjika na asipate dawa. Aache kutukana watu kila kukicha, binadamu tumeumbwa na vinyongo. Siku Polisi wakikinai kuitwa wajinga au siku wakitamani kuufanya ujinga hadharani itakua hatari kwa nchi yetu. Hii ni nchi yetu sote, tuilinde!!

3. Mwambieni Lissu, walio nyuma yake ni ndugu zake ktk Chama, ndugu zake ktk damu na ni Watanzania wenzetu. Asiwatumie vibaya, majuto ni mjukuu. Likitokea la kutokea hasara ya kwanza ni kwetu sisi kama nchi, aachane na mzaha huo. Ni kosa kutumia njia haramu kuutafuta mwisho halali, Ikulu mtu hawezi kwenda kwa kupita ktk mifereji ya damu za watu. Aache mara moja!!
#MitanoTenaKwaJPM.
Umepanic! Lissu amezuiwa kufanya kampeni. Hayo mengine ni kanuni zenu za chumbani za Uchaguzi
 
Kukosekana kwa tofauti hiyo ndio maana popote alipo mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli ndipo alipo Rais wa JMT. Huwezi kuutofautisha ugombea wa John Pombe Joseph Magufuli na Urais wake au Uenyekiti wake wa CCM. Hivyo hivyo huwezi kuutofautisha ugombea wa Tundu Lissu na Umakam Mwenyekiti wake vinginevyo ni kujidanganya tu.
Wewe huoni hili limeua hoja yako nzima, au huelewi?
 
Hayo ndiyo mawazo yako, Kama Ni nafsi basi hata kulala asilale maana Ni mgombea. Tofautisha kupanda jukwaani kuomba kura na kuongea na wanachama wako.
 
Umemnsikiliz ajana mwenyekiti wa Tume ya madili waliompa adhabu jana ? au unakurupuka tu?
 
Lissu anayajua hayo yote anatumia loop holes za watunga sheria kuwafundisha sheria hapa ametengeneza precedent ambayo hawakuitarajia ni jambo la kufikirisha kisheria, serikali yetu haina watu makini.
Hata kama asiposhinda ila tundu Lisu ametufundisha ujasiri
 
Back
Top Bottom