ephen_
JF-Expert Member
- Oct 28, 2022
- 14,949
- 54,485
Mungu ampe faraja huko gerezani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mungu ampe faraja huko gerezani.
Ooh maana usikute serikali inatumia hadi uchawi kuona vilivyojificha nikajikoroga😂😂😂Nakumbuka moja ya alama aliyoacha ni kitendo cha kujitumia sms kwenye simu ya mke wake yaani sender na receiver wote wanasoma mnara mmoja na location moja yaani amejisahau kabisa watu wa mitandao hao walitoa data za lissu kwa serikali😁😁
Kuingiza ndugu kwenye ndoa ndio vyanzo vya ugomviInaonekana ndugu walizembea sana kuchukua hatua mapema, kuna stori jamaa alishalazimisha taraka ikawa dana dana
Jamaa likuwa mweupe kabla ya kuingia jela.Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo Februari 26,2025 imeanza kusoma hukumu ya kesi ya mauaji, inayomkabili Mfanyabiashara Khamis Luwonga (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa.
Katika kesi hiyo ya mauaji namba nne ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.
=======
Kijana Khamis Luwonga (45) maarufu Meshack aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kumuua mke wake, Naomi Marijani na kisha kuuchoma mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Hukumu hiyo imetolewa leo Februari 26,2025 na Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi 14 wa upande wa Jamhuri ambao wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo.
Luwonga alimuua mkewe Naomi na kisha kuuchoma moto mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa nyumbani kwao eneo la Gezaulole, wilayani Kigamboni, Dar es Salaam Mei 15, 2019.
Baada ya kuuchoma mwili huo ndani ya banda la kuku, alienda kuzika masalia ya mwili huo na majivu shambani kwake na kupanda migomba juu yake.
TBC