Aliyemtungia Mungu nickname ya Jah ni nani?

Aliyemtungia Mungu nickname ya Jah ni nani?

Sijaongea kuhusu dini ila kuna maneno ukitumia ukichanganya na lugha tofauti ndio huleta tatizo maana lugha unayoitumia inaweza kulitafsiri neno tofauti. Huwezi kwenda kanisani alafu uanze kusema jah awabariki, direct utaonekana umewadharu kwanza watu mnaosali nao.
Kanisani wapi na wanatumia lugha gani wasikokuelewa?unajua kwamba Mungu ana majina zaidi ya 1000 na hilo Jah likiwemo?u unajua maana ya nickname?
 
Kanisani wapi na wanatumia lugha gani wasikokuelewa?unajua kwamba Mungu ana majina zaidi ya 1000 na hilo Jah likiwemo?u unajua maana ya nickname?
Najua kila lugha na jina lake, ila dha ya kutumia jina la taifa nyingine katika lugha yetu huoni inaaribu? Basi kama inatumika lugha zaidi ya moja sidhani kama itatumiza lugha au neno lenye utata.
 
Habari wana na binti wa Mungu.

Naomba kuuliza aliyempa Mungu jina la jah ni nani? Na je alikuwa na kusudi gani?
Au pengine ni mimi nimefikiria jah ni Mungu? Maana naona mitandaoni tu " jah bless, jah akulinde" au kuna miungu mingine inaitwa jah? Maana niko njia panda.
Kwani huyo Mungu jina lake anaitwa nani?
 
Habari wana na binti wa Mungu.

Naomba kuuliza aliyempa Mungu jina la jah ni nani? Na je alikuwa na kusudi gani?
Au pengine ni mimi nimefikiria jah ni Mungu? Maana naona mitandaoni tu " jah bless, jah akulinde" au kuna miungu mingine inaitwa jah? Maana niko njia panda.
Jah sio nickname. Kuna andiko kwenye Zaburi tafsiri ya Union Version ya Kiswahili ameitwa YAHU ambaye ni YHW yaani YEHOVA.

Vv
 
Jah ni jina la Mungu anaeabudiwa na Rastafarians. Wao wanaamini Haile Selassie wa kwanza wa Ethiopia ni messiah wa pili aliyetumwa baada ya Yesu. Na jina Jah wamelitohoa kwenye biblia, yani Yahwe. (Zab 68:4).
Lakini kwa sababu wametoa jina hilo kwenye biblia haimaanishi wanamwabudu Mungu anaeabudiwa na wakristo au waislam. Ni kama watu kadhaa wakiitwa Sikitu, haimaanishi wote ni mtu mmoja.
Ukitaka kufahamu zaidi soma kuhusu imani ya Rastafarians.
Kuna wale wanaotumia neno Jah wakimaanisha Mungu huyu tunaemwabudu. Lakini hawaelewi maana halisi ya jina hilo.
Na pia kuna watu wanaojiita Rastafarians, lakini hawapractice imani hasa ya rastafarians.
 
Habari wana na binti wa Mungu.

Naomba kuuliza aliyempa Mungu jina la jah ni nani? Na je alikuwa na kusudi gani?
Au pengine ni mimi nimefikiria jah ni Mungu? Maana naona mitandaoni tu " jah bless, jah akulinde" au kuna miungu mingine inaitwa jah? Maana niko njia panda.

Updates....

Tayari nimeshapata jibu, asanteni wote mlio nijuza maana nilikua sijui.
Zaburi 68:4 (UV Swahili Bible )
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,Mtengenezeeni njia ya barabara,Apitaye majangwani kama mpanda farasi;Jina lake ni YAHU; shangilieni mbele zake.

Vv
 
Wajamaica nao watakua na uzi wao wanauliza aliempa Jah jina la Mungu ni nani? [emoji12] [emoji12]
 
Mleta maada elewa kwamba nomino ni utambulisho wa kitu kwa hiyo hata neno Jah linasimama kumaanisha MUNGU,
Allah kwa waarabu linasimama kumaanisha MUNGU.

God kwa kiingereza
Jehova kwa kiiebrania/ kiyahudi
Wewe mswahili unaita Mungu
Wabantu wanaita Mulungu.

Kwa hiyo usiweke ligi juu ya hayo majina as long as hayo majina hutamkwa kwa kusudio la MUNGU aliye mmoja,
Ingawa MTU mwingine aweza kutumia jina/majina tajwa hapo juu kumaanisha majina ya mungu/ miungu.
 
Back
Top Bottom