Kama ni hivyo basi asingeitisha press conference kumbe wadhamini wanafahamu kila kitu. Ametusumbua kutuita kwasababu gani kama kila kitu kinafahamika kwenye kamati. Mo peke yake ndiye katoa 20b za 49% ya hisa, kanuni inasema hivyo?
Press ya jana ilikua ni kuueleza umma juu ya walipofikia katika uwekezaji na mchakato wa mabadiliko ya Simba.
Haimaanishi kwamba jana ndio wameeleza kila kitu (further details) pale. Ndio maana nikashauri kama wewe unataka hizo deep info unaweza kuzipata kama ukifuatilia kwenye ngazi husika (FCC, kwenye vikao vya klabu, kupitia vyanzo mbalimbali vya habari vya klabu, n.k). Kama kukwambia ufanye hivi ni kumaanisha kwamba press ya jana haikua na umuhimu, basi unisamehe sana.
Nitoe mfano mdogo tu:
Udhamini wa bidhaa za Mo kwenye jezi za Simba ni wa kimkataba, ilifanyika press wakasaini na kutangaza kwa umma.
Sasa wewe unapotumia suala la udhamini huu kama ishara ya "utapeli" wa Mo, ina maana ama haufuatilii kinachoendelea, au umeamua tu kutuuliza "akina sisi" ili kama hatuna kumbukumbu juu ya hili tuungane nawewe katika kumlalamikia Mo.
Kwanini usingejiridhisha kwamba udhamini ule si wa kimkataba na klabu haipati pesa, ndipo hoja hiyo uijumuishe katika madai yako hapo juu ?
Ina maana unataka Mo aanze kuyazungumzia mambo haya kwenye press mkuu ?
Sikubezi katika hoja zako, ila naona kwamba mengi unayoyahoji unaweza kuyapatia majibu katika ngazi sahihi endapo ukiamua kufuatilia.
Kuhusu suala la MO PEKE YAKE kutoa 20B:
Kama kwenye structure ya Simba inaruhusu mtu mmoja kuweka 20B na akachukua 49% ya hisa, kosa la Mo hapa linakua ni lipi ?
Kama unafahamu kwamba structure ya Simba inataka wawekezaji wanne ndio wagawane hizo 49% sema hapa ili tujue kwamba Mo amekiuka kipengele hicho, na useme ni ibara ipi au sheria ipi iliyokiukwa.
Kama unafanya marejeo kwenye timu nyingine nadhani utakua unakosea na unalazimisha mambo yaende your way.
Ripoti za mapato na matumizi ya klabu zipo, unataka Mo aje kwenye press kuzisoma pale ili nawewe ufahamu kwamba deficit zilikua kiasi gani na akaongezea hela yake ?
Hivi ndivyo taasisi zinaendeshwa ?
Kusomeana mapato na matumizi kwenye vyombo vya habari ?
Ndugu yangu mambo mengi uliyoyahoji hapo unaweza kuyapatia majibu kirahisi sana, haujaamua tu. Niamini mimi.