Apo suhala la kuhoji ni ayo mapato ya timu ata mm kwa upande wang sijaelewa timu ina mikataba zaid ya minne ukijumlisha na mengne inaweza kufka ata 2bl kwa mwaka,sasa mo anasema anatoa pesa kama yeye karbu 5 bl sio kama haiwezekan ila vzur angeelezea kwamba simba pamoja na mikataba yake na mapato yake yote kwa mwaka ni kias fulan matumiz ya timu kwa ujumla ni kias fulan kwaiyo apo ingekua rahis kujua kat ya mapato ya simba mo anaongezea kias gan ukisema ww unatoa kias fulan bila kusema timu inaingiza kias gan apo kuna ukakasi,ayo mengine sio kama mo analalamika ila ni anaongea kile anachofanya mtu ambae anatoa ela au ktu ikitokea siku anaongea hadharan lazma aseme kile anachofanya maana aliaid kufanya ayo anayosema kama atakaa kimya tu nan atajua sasa ,kama unakumbuka gsm walipishana kidogo kaur na uongoz wakatishia kujitoa ktk barua yao walielezea meng kuanzia mkataba wanachotakiwa kufanya lkn wakaongeza na mengine ambayo walisema wanafanya kwa mapenz nje ya mkataba sio kama waliongea vile kwa kulalamika ila umma ujue nin umuhimu wao na nn wanafanya
Mkuu, kwanza jana Mo hakwenda kwenye press kusoma ripoti ya mapato na matumizi.
Pili, kulikua na maneno mitandaoni kwamba Mo hataki kuweka ile 20B kwa sababu anaona ameshaihudumia timu na "Duniani hakuna cha bure" hivyo watakatana juu kwa juu.
Lengo la kusema kwamba hizo 24B kwa miaka minne alikua anatoa kwa mapenzi yake kuisaidia klabu lakini hiyo 20B iko palepale na anaitoa.
Tena alisema pale kabisa kwamba anaweka 20B ili kuondoa hayo maneno maneno (maana yake maneno yalikuwepo).
Sasa je, kusema hivyo ni kosa ?
Kusema hivyo kunamaanisha Simba ilikua haina chanzo kingine cha mapato ?
Leo hii tuseme kwamba GSM haisaidii Yanga pale hivi tutakua na akili kweli ?
GSM akisema alikua anatoa hizo pesa kwa sababu ya mapenzi yake Yanga litakua ni kosa ?
Akisema hivyo atakua anamaanisha Yanga ilikua haipati pesa toka Sportpesa, viingilio n.k ?
Ili kuyazungumza hayo tunahitaji kusomewa ripoti ya mapato na matumizi kwanza ?
Haya, mapato ya Simba au Yanga kwa mwaka (miaka minne iliyopita) tuseme ni roughly bilioni 3.
Hivi wewe unaweza kuendesha klabu ya Simba au Yanga msimu mzima kwa 3B ? Mtu akisema aliongezea inakua nongwa ?
3B unawezaje kusajili wachezaji wazuri, ukalipa mishahara mizuri, posho nono, wakasafiri kwa ndege msimu mzima, wakalala kwenye hoteli za maana, wakala vizuri, program za mazoezi zikaenda vizuri, ukaboresha benchi la ufundi kwa kuleta wataalam wa kila namna na mengineyo ?
Labda tusaidie wewe mkuu, huenda tatizo haliko kwa Mo na halitakuwepo kwa GSM, labda tuna shida kwenye budgeting.
Help us, utakua umesaidia soka la nchi hii.