Aliyeng'atwa na Nyoka afia Kituo cha Afya kisa hana 150,000 Wilayani Babati

Kwenye hz hospital zetu ukiwa na huruma utatumia mpaka mshahara wako,tatzo hujui uhalisia huwa unakuwaje
Sio Kwa scenario hiyo mtu amegongwa na nyoka na unajua kabisa baada ya muda atafariki asipopata huduma,sio malaria hiyo sio tb sio gonorea tunazungumzia mtu yupo katika mstari wa kifo ana sumu mwilini,hiyo n zaid ya roho ya kishetani..
Hao wat wanapaswa kushtakiwa Kwa kosa la kuua Kwa kukusudia
 
Hata hekima ya kawaida ya kiutu iliwafanya hao watatu waliokuwa na mgonjwa washindwe kupokea bond ya pikipiki ya mume wa mgonjwa ili matibabu yatolewe?

Ndiyo kwenye kazi kuna boss lakini ishu mezani ni nzito mtu anataka kufa kuna opti ya kufanya atibiwe malipo baadae hata huyo anayejiita dk mkuu angeelezwa tu mgonjwa kwa hali yake ilibidi mumewe aweke dhamana chombo chake funguo hii hapa atakuja kulipa basi wangekuwa wameokoa maisha tatizo hao hawakuumbwa wawe madaktari sometimes waliumbwa kuwa mafundi magari.
 

Sio kosa la wauguzi, ni mifumo Mibaya na Policies za hovyo za afya!
 
Angekuwepo Dkt. Gwajima D kwenye hiyo wizara kusingetokea huo upuuzi
 
Huyo Mganga Mfawidhi amechangia hiyo mauti kutokea, ingefaa awajibishwe haraka, hafai kuwa mtumishi wa umma
 
Mambo ya hovyo kabisa, Kung'atwa na nyoka ni dharura! Hapakuwa na ulazima wa kumtembeza na kumsubirisha mgonjwa, alipaswa ahudumiwe haraka sana, hata kama hakukuwa na dawa, hata huduma ya kwanza?? Mganga mfawidhi anataarifiwa mgonjwa ameng'atwa na nyoka anajibu yupp mbali wawasiliane na wahudumu wengine? Serious? Badala apige simu yeye atoe maelekezo ya haraka! Wote wamefanya makosa makubwa sana, Wanapaswa kufikishwa mahakamani, na familia ya huyo mama ilipwe fidia kwa uzembe wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…