Aliyeng'atwa na Nyoka afia Kituo cha Afya kisa hana 150,000 Wilayani Babati

KATIKA hali ya kusikitisha, mkazi wa Magugu, Wilaya ya Babati, Juliana Obedy (44), amepoteza maisha baada ya wataalamu katika Kituo cha Afya Magugu, kudaiwa kumcheleweshea huduma kituoni hapo kutokana na kugongwa na nyoka.

Imedaiwa kuwa, sababu za kucheleweshwa kwa huduma hiyo ni wataalamu kutaka kulipwa Sh. 150,000 ikiwa ni gharama za matibabu.

Akisimulia mkasa huo jana, mume wa Juliana, Obedy Laizer, alisema Desemba 16, mwaka huu, akiwa anavunja jengo la Kanisa la Katoliki Magugu, mke wake alipita akiwa anachuma mboga za majani na kung'atwa na nyoka ambaye hakujua ni wa aina gani.

Laizer alisema baada ya muda mfupi mke wake kuondoka, alikuja mtoto wake na kumwambia anaitwa na mama yake ambaye alidai kung'atwa na nyoka, ndipo alipokimbia kumpeleka Kituo cha Afya Magugu.

Alipomfikisha kituoni hapo kulikuwa na foleni na kushauriana na mke wake waingie ndani na kujisajili, lakini wauguzi waliwaambia kuwa daktari alikuwa chumba cha wazazi na kuomba apigiwe simu ili kuja kumsaidia.

"Daktari alipigiwa simu mara ya kwanza hakupokea, akapigiwa simu mara ya pili ndipo alipopokea akasema anakuja na alitoa huduma na mgonjwa kuandikiwa dawa," alisema Laizer.

Hata hivyo, alisema alipoenda duka la dawa aliambiwa anatakiwa kulipia Sh. 150,000 ambapo Laizer aliomba mgonjwa ahudumiwe na fedha itafuata, lakini wauguzi wawili na daktari mmoja waliokuwapo hawakukubali na kuamua kumpigia Mganga Mfawidhi simu na kujibiwa kuwa anatakiwa alipie Sh. 150,000 na kukata simu.

Laizer alisema baada ya kuvutana na wataalamu hao alitoka na kwenda kutafuta fedha aliporudi alitoa Sh. 130,000 na badala ya kuanza kutoa huduma, wataalamu hao walianza kupigiana simu ndipo mmoja alisikika akisema mgonjwa ahudumiwe.

Aidha, alisema baada ya kulipia fedha hiyo muuguzi anayehusika na dawa alimpeleka duka la dawa na kumpatia na walirudi kwa mgonjwa ambako alifukuzwa wodini, lakini aligoma akitaka kushuhudia mke wake akihudumiwa.

Alisema mgonjwa aliulizwa anajisikiaje naye akajibu kuwa anajisikia vibaya huku akisema “Bwana Yesu nisaidie” ghafla aliacha kuongea na ndugu na majirani waliokuwapo walianza kumwombea kwa kushirikiana naye bila mafanikio.

Alisema baada ya mke wake kukata kauli wauguzi waliendelea kumchua na kumwekea oksijen, lakini alipoona haisaidii aliwaambia waitoe.

"Baada ya kuona hivyo niliwaambia mke wangu ndio anaondoka hivyo, tulienda duka la dawa wakanipa dawa ya Sh. 6000 ya kumpunguzia maumivu na sikupewa risiti, wala ile ya 150,000 sikupewa," alisema.

Akiongea kwa uchungu alisema licha ya kuwaomba aweke rehani pikipiki yake na kuwapa funguo wauguzi ili wamhudumie mke wake waligoma na kudai akikimbia wao ndio wanawajibika.

Mtoto wa marehemu, Abednego Obedy, alisema mama yake alimwonesha mkono ukiwa umevimba na kumwambia ameng'atwa na nyoka na kumshauri kwenda kituo cha afya.

Aidha, Enoti Philipo ambaye alikuwa akimwita marehemu shangazi, alisema alitoka nyumbani kwake kuchuma mboga za majani na baadaye aliona mume wake anamkimbiza hospitali.

Mkazi wa kijiji hicho, Yona Laizer, alisema kitendo kilichofanywa na wataalamu hao ni uzembe na unyama ambao kama wakiendelea watasababisha vifo vingi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Magugu, Lohay Amos, alilaani tukio hilo na kuwataka wauguzi na madaktari kutii viapo vyao.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Magugu, Dk. Kusta Ndunguru, alikiri kupigiwa simu na Laizer huku akisema alijua anathibitisha malipo aliyoambiwa.

Dk. Ndunguru alisema alimwambia aongee na wataalamu waliopo hospitali ili wamsaidie kwa kuwa yeye yuko nje ya kituo na hakumrudia.

Alisema mtu aking'atwa na nyoka mwenye sumu kali haitakiwi kuzidi nusu saa kwasababu ikizidi anapoteza maisha ndio maana alimwambia awaeleze wataalamu ili wamsaidie asipoteze muda.

Chanzo: Nipashe
Kwa nini Dr. Ndunguru hakuongea mwenyewe na hao wataalamu?

Amandla...
 
Poor training, supervision na management ya afya.

Ndio kiini cha tatizo, sera na sheria zipo wazi.

Kwanza katiba airuhusu discrimination ya huduma afya, pili lazima kuna sheria kwa kanuni za WHO medics hawatakiwi kumuacha mteja anaehitaji huduma yao hasa kwenye kuokoa maisha yake kumuacha kisa hana hela.

Kuna mambo luluki ya ku-justify na kuweza kuhutimisha shida ni management.

Kama wewe ni consultant unatakiwa uelezee tatizo la hii case. Msingi wa tatizo ni training ye (below par), kuna skills nyingi medics wanatakiwa kuwa nazo top of the list ni empathy (it’s the top of five pillars za medical ethics) kwa sababu wanakutana na vulnerable people ambao only their intervention can change the outcome.

Mtu kufa kisa kukosa, hela maana yake hawana empathy (top of the hierarchy on five pillars of medical medical ethics.

Hadi medics kutokuwa na empathy maana yake ni poorly trained and supervised. Na kama case hiko public maana yake wizara nzima ya afya imeoza.

Embu nchi iweke watu wenye uwezo wa kusimamia hiyo sector.
 
Sio Kwa scenario hiyo mtu amegongwa na nyoka na unajua kabisa baada ya muda atafariki asipopata huduma,sio malaria hiyo sio tb sio gonorea tunazungumzia mtu yupo katika mstari wa kifo ana sumu mwilini,hiyo n zaid ya roho ya kishetani..
Hao wat wanapaswa kushtakiwa Kwa kosa la kuua Kwa kukusudia
Hakika ni wanastahili kushitakiwa, mtu katoa laki na thelathini ila still mkewe anakufa kweli?
 
Hata hekima ya kawaida ya kiutu iliwafanya hao watatu waliokuwa na mgonjwa washindwe kupokea bond ya pikipiki ya mume wa mgonjwa ili matibabu yatolewe?

Ndiyo kwenye kazi kuna boss lakini ishu mezani ni nzito mtu anataka kufa kuna opti ya kufanya atibiwe malipo baadae hata huyo anayejiita dk mkuu angeelezwa tu mgonjwa kwa hali yake ilibidi mumewe aweke dhamana chombo chake funguo hii hapa atakuja kulipa basi wangekuwa wameokoa maisha tatizo hao hawakuumbwa wawe madaktari sometimes waliumbwa kuwa mafundi magari.
Shida iliyopo sasa watu wengi hawana passion na kazi zao ila wanafanya ili tu waweze ku survive kimaisha. Yani mtu focus ni mshahara wake tu.

Hio hali imeenea sector zote ndio maana mtu ana hofu ya kupoteza kibarua chake kiasi kwamba hata humanity hakuna. Tendo la ubinadamu tu ni mpaka uwe na hela. Watu wametanguliza maslahi mbele sana ila kuna situations zinaumiza sana. Imagine unapoteza mke kwa sababu ya uzembe wa madaktari. Nilishampoteza kaka kisa sh.elfu 5 ya sindano ya kulegeza kifua cha pumu.
 
Hiyo ni kazi kama kazi zingine .Mnahimizwa sana muwe na bima ya afya ila hamzingatii.

Wewe hapo unapofanya kazi unaweza kumuhudumia mtu bure?
Huu ni upumbavu wa hali ya juu, huduma ya afya ni tofauti na biashara zingine.

Emergency ya mtu anayehitaji instant treatment haipaswi kusubiria malipo. Huyo mgonjwa angepewa huduma stahiki kwa sasa angekuwa hai. What is 150,000 compared na uhai wa mtu. Chukulia aliyeafanyiwa hivyo angekuwa mama yako mzazi still ungeropoka the same way?
 
Huko hospital wamejaa vilaza waliofeli form four wakakosa option nyingine,wao hutumia nguvu badala ya akili.
Alafu labda mi sielewi mgonjwa akilazwa si bill ni badae?
Wapumbavu sana tena nina hakika hao waliokuwa wanamkwepa ni wanawake wenzake kabisa😐. Sizungumzi kwa ubaya ila in case mtoto au mke wangu akifa kwa uzembe wa aina hio sitaacha hao watu waishi. Nipo tayari kwenda kufia jela.
 
Siku moja miaka mingi iliyopita jioni tukiwa makazi mapya ndio tumehamia nikatoka nje niende dukani kununua vocha.

Nikitembea gizani nikakanyaga nyoka akaning'ata kwenye vidole viwili vya miguu kumulika anatokomea vichakani..

Nilitoka mbio mpaka nyumbani sebureni nikamkuta shangazi, mama yangu mzazi na ndugu zangu wengine wakaanza kunipa first aid

Shangazi akasema yeye pia aliwai kun'gatwa na nyoka hivyo aitwe mmama mmoja jirani aje kunitibu ilikua ni jumapili..akaenda kuitwa akaja akachukua wembe kunichana kidogo kwenye jeraha akaenda nje akaja na mizizi akaniambia nitafune nimeze maji yake then nilipo Tena akachanganya na majani kisha akabandika mguuni..

Akasema Kama ni nyoka wa kawaida umepona Kama ni vice versa Sito ponaa Akaondoka.

Nikalala usiku kwa hofu maana sikujua Yale majani TU yanitibu haaahaa nilipona ☺️😊

From Rock City Mwanza.
Ulipata bahati ya kugongngwa na nyoka asiye na sumu kali.
Kuna nyoka wana sumu kali balaa huyoboi kwenye dawa za ujanja ujanja.
 
Shida iliyopo sasa watu wengi hawana passion na kazi zao ila wanafanya ili tu waweze ku survive kimaisha. Yani mtu focus ni mshahara wake tu.

Hio hali imeenea sector zote ndio maana mtu ana hofu ya kupoteza kibarua chake kiasi kwamba hata humanity hakuna. Tendo la ubinadamu tu ni mpaka uwe na hela. Watu wametanguliza maslahi mbele sana ila kuna situations zinaumiza sana. Imagine unapoteza mke kwa sababu ya uzembe wa madaktari. Nilishampoteza kaka kisa sh.elfu 5 ya sindano ya kulegeza kifua cha pumu.
Hii point, watu hawana passion na kazi zao
 
Kabisa, wanashindwaje hata ikibidi walatwe kwenye salary zao, sijajua ni mazingira ya namna gani yaliwafanya wasiwe na huruma kwa kitu urgent?😭
Sasa kama hujajua mazingi ra kwa Nini unahukumu! Ungeuliza kwanza ,hii michakato na urasimu ilichukua muda gani, na je mgonjwa alipelekwa Kituoni muda gani baada ya kugongwa nyoka,na je sumu ya hiyo nyoka inaruhusu haya yote! RIP mama Laizer tuna mengi ya kujifunza!
 
KATIKA hali ya kusikitisha, mkazi wa Magugu, Wilaya ya Babati, Juliana Obedy (44), amepoteza maisha baada ya wataalamu katika Kituo cha Afya Magugu, kudaiwa kumcheleweshea huduma kituoni hapo kutokana na kugongwa na nyoka.

Imedaiwa kuwa, sababu za kucheleweshwa kwa huduma hiyo ni wataalamu kutaka kulipwa Sh. 150,000 ikiwa ni gharama za matibabu.

Akisimulia mkasa huo jana, mume wa Juliana, Obedy Laizer, alisema Desemba 16, mwaka huu, akiwa anavunja jengo la Kanisa la Katoliki Magugu, mke wake alipita akiwa anachuma mboga za majani na kung'atwa na nyoka ambaye hakujua ni wa aina gani.

Laizer alisema baada ya muda mfupi mke wake kuondoka, alikuja mtoto wake na kumwambia anaitwa na mama yake ambaye alidai kung'atwa na nyoka, ndipo alipokimbia kumpeleka Kituo cha Afya Magugu.

Alipomfikisha kituoni hapo kulikuwa na foleni na kushauriana na mke wake waingie ndani na kujisajili, lakini wauguzi waliwaambia kuwa daktari alikuwa chumba cha wazazi na kuomba apigiwe simu ili kuja kumsaidia.

"Daktari alipigiwa simu mara ya kwanza hakupokea, akapigiwa simu mara ya pili ndipo alipopokea akasema anakuja na alitoa huduma na mgonjwa kuandikiwa dawa," alisema Laizer.

Hata hivyo, alisema alipoenda duka la dawa aliambiwa anatakiwa kulipia Sh. 150,000 ambapo Laizer aliomba mgonjwa ahudumiwe na fedha itafuata, lakini wauguzi wawili na daktari mmoja waliokuwapo hawakukubali na kuamua kumpigia Mganga Mfawidhi simu na kujibiwa kuwa anatakiwa alipie Sh. 150,000 na kukata simu.

Laizer alisema baada ya kuvutana na wataalamu hao alitoka na kwenda kutafuta fedha aliporudi alitoa Sh. 130,000 na badala ya kuanza kutoa huduma, wataalamu hao walianza kupigiana simu ndipo mmoja alisikika akisema mgonjwa ahudumiwe.

Aidha, alisema baada ya kulipia fedha hiyo muuguzi anayehusika na dawa alimpeleka duka la dawa na kumpatia na walirudi kwa mgonjwa ambako alifukuzwa wodini, lakini aligoma akitaka kushuhudia mke wake akihudumiwa.

Alisema mgonjwa aliulizwa anajisikiaje naye akajibu kuwa anajisikia vibaya huku akisema “Bwana Yesu nisaidie” ghafla aliacha kuongea na ndugu na majirani waliokuwapo walianza kumwombea kwa kushirikiana naye bila mafanikio.

Alisema baada ya mke wake kukata kauli wauguzi waliendelea kumchua na kumwekea oksijen, lakini alipoona haisaidii aliwaambia waitoe.

"Baada ya kuona hivyo niliwaambia mke wangu ndio anaondoka hivyo, tulienda duka la dawa wakanipa dawa ya Sh. 6000 ya kumpunguzia maumivu na sikupewa risiti, wala ile ya 150,000 sikupewa," alisema.

Akiongea kwa uchungu alisema licha ya kuwaomba aweke rehani pikipiki yake na kuwapa funguo wauguzi ili wamhudumie mke wake waligoma na kudai akikimbia wao ndio wanawajibika.

Mtoto wa marehemu, Abednego Obedy, alisema mama yake alimwonesha mkono ukiwa umevimba na kumwambia ameng'atwa na nyoka na kumshauri kwenda kituo cha afya.

Aidha, Enoti Philipo ambaye alikuwa akimwita marehemu shangazi, alisema alitoka nyumbani kwake kuchuma mboga za majani na baadaye aliona mume wake anamkimbiza hospitali.

Mkazi wa kijiji hicho, Yona Laizer, alisema kitendo kilichofanywa na wataalamu hao ni uzembe na unyama ambao kama wakiendelea watasababisha vifo vingi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Magugu, Lohay Amos, alilaani tukio hilo na kuwataka wauguzi na madaktari kutii viapo vyao.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Magugu, Dk. Kusta Ndunguru, alikiri kupigiwa simu na Laizer huku akisema alijua anathibitisha malipo aliyoambiwa.

Dk. Ndunguru alisema alimwambia aongee na wataalamu waliopo hospitali ili wamsaidie kwa kuwa yeye yuko nje ya kituo na hakumrudia.

Alisema mtu aking'atwa na nyoka mwenye sumu kali haitakiwi kuzidi nusu saa kwasababu ikizidi anapoteza maisha ndio maana alimwambia awaeleze wataalamu ili wamsaidie asipoteze muda.

Chanzo: Nipashe
Goli la mama ni milioni tano
 
Back
Top Bottom