Aliyeng'atwa na Nyoka afia Kituo cha Afya kisa hana 150,000 Wilayani Babati

Mzee,
Kua uyaone....tembea ujionee.. mwezi wa 8 mwaka huu tulimpoteza ba mkubwa so tulisafir kwenda msibani kilicho tokea ni kua tukiwa kwenye kikao Cha familia ghafla nyoka mkubwa akaja mbio akakatiza mbele kiasi kikao kila mtu akakimbia na wengine sisi wanaume kubeba fumbo na mawe.

Kaka akatukataza kumpiga na kumponda mawe akamwita jamaa mkamata majoka na kuyafuga yeye na familia yao wakamkamata kwa mikono na kumchukua..

Wanakua na dawa za kuwapumbaza majoka

Hizi sio hekaya ama story za alfa ulela ulela 😅
 
...Hivi hao Wasaidizi na Dakitari Mkuu Wao Bado Wako Kazini ?? WanatakiwaMgonjwa alipofariki Kwa Kujizungusha kwao, Hapo Hapo wanatakiwa Kuchapa Lapa'!
Yaani Binadamu mwenzetu afariki Kukosa Dawa Kwa Sababu haba Shs 150, 000/ - ??
Hivi Dawa ya Kuumwa na Nyoka ni Shs Laki Moja na Nusu ??
Na ule utaratibu ahudumiwe kwanza kama Hana Hela Umeishia wapi ?
Huyo Dakitari Mkuu Kwa Nini amuambie Mume wa Marehemu awaambie Wasaidizi wamsaidie Marehemu Badala ya Kuwaambia yeye ??? R.I.P Mama Mpendwa. Yana Mwisho Haya..
 
...Wanakujia Wangapi ambao Wameumwa na Nyoka, na Wako Hatarini Kupoteza Maisha ??
 
Goli la Mama 5 Million
 
Mbona mnawasema waajiriwa ikiwa wanapewa maagizo na boss wao.

Wapo pale wameambiwa ukitoa ugonjwa huu na huu basi wengine wote watoe hela basi ndy utaratibu upo hvyo.

Sasa tatzo lipo mbali sio kama mnavyo liona
.
 
Naona wahudumu wanashambuliwa sana humu, na nimesikia kuna waliosimamishwa kazi.

Lakini haya yote ni matokeo ya kuendekeza siasa kwenye kila jambo nchi hii. Wanasiasa badala ya kuwekeza kwenye uundaji na utekelezaji wa sera nzuri hasa katika sekta nyeti ikiwemo hiyo ya afya (ikiwemo kupunguza gharama za matibabu na kurahisisha upatikanaji wa vifaatiba), wamewekeza kwenye kukurupuka na maamuzi ya mizuka tu.

Ninaamini kama hao wahudumu wangeamua kutoa huduma kinyume na utaratibu kulinda uhai wa mgonjwa na akapona hata wasingeonekana mashujaa kwani hata wazo la kuwa wameokoa uhai wa mtu lisingekuwepo. Na kama mwenye mgonjwa angeingia mitini ushujaa wao ungegeuka ujuha na wangeishia kuonekana wa ajabu na kuchukuliwa hatua na walewale wazee wa mikurupuko ya kisiasa.

Tatizo kuu hapo ni mifumo, then wahudumu wanafuata baadaye.
 
Nilisoma sehemu kwamba watoa huduma wamesimamishwa ila kiukweli anayetakiwa kuwajibika ni mganga mfawidhi.

Mwananchi inaonyesha alikaa muda mkubwa nyumbani kabla ya kwenda hospitali hii ni kwakua sumu ya nyoka haiui kwa short time kiasi hicho, mpaka mkono kuvimba.

Hiki kifo kilikua kinaweza kuzuilika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…