Aliyepandisha gharama za Toto Afya kadi ni muuaji. Magufuli tunamkubuka kwa hili

Aliyepandisha gharama za Toto Afya kadi ni muuaji. Magufuli tunamkubuka kwa hili

Tatizo lilianzia pale Nyerere aliposema Elimu bure, Afya bure... Tuwe responsible basi. Mtoto uzae mwenyewe...
Hakuna anayeuliza gharama halisi ni kiasi gani? Kila mtu anataka alipiwe tu, nani analipa?
 
Tatizo serikalini wamejaa watu wasio na maono full stop. Siku ambayo hii nchi itapata viongozi hata 20 huko serikalini wenye maono, utu na uthubutu na wapo "serious" na wakamua kufanya mambo ya muhimu tu na kuacha yasiyo na tija basi watoto wote chini ya miaka 10 watatibiwa bure kabisa nchi nzima bila hata kukata bima ya afya na hata elimu itakuwa bure kabisa. Hesabu ndogo hii hapa chini:-

1. Uza maprado yote ya wakurugenzi wa idara na wizara zote, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, wakurgenzi wa miji na majiji wape landcruiser hardtop "mkonga". Pesa zote peleka serikalini wizara ya afya ndio iwe kipaumbele. Asiyetaka hardtop basi ajinunulie shangingi lake serikali imwekee mafuta tu. Mbona enzi za Nyerere magari yote ya serikali kwa asilimia kubwa yalikuwa landrover "mandolin" tena nchi ilikuwa na barabara mbovu hazina lami iliwezekana kwa nini sasa hivi isiwezekane?
2. Pesa - mamilioni ya kununua magoli ya Taifa Stars, Simba na Yanga yote peleka wizara ya elimu na afya. Hata kama fedha hizo za magoli zitaokoa maisha ya mtoto mmoja itakuwa ni faraja. Kwa wenzetu maisha ya mtoto mmoja tu ni jambo la muhimu kuliko kitu kingine chochote kile. Ukitaka kujua maisha ya kila binadamu na hata mtoto ni muhimu basi pata msiba wa mtoto hata wa siku moja na mbaya zaidi ukute ni ugonjwa unaotibika hospitalini lakini hauna uwezo wa kumudu gharama za hospitalini.
3. Ondoa mabango yote yaliyotapakaa nchi nzima yanayosifia viongozi pesa itakayookolewa ipelekwe serikalini. Kwa hili hata kama haya mabango hayagharamiwi na serikali basi wale watu binafsi waliojitolea kuwasifia viongozi waelekezwe gharama wanazotegemea kutumia kusifia viongozi kwenye mabango wazielekeze hazina zikasaidie serikali.
4. Punguza misafara kwenye ziara za viongozi. Yawepo magari ya viongozi tu na wale watu wa vyombo vya usalama wanaolinda viongozi wetu basi. Wengine wote waliobaki wanaohitajika tu kwenye msafara pakia kwenye "coaster" au mabasi makubwa tena ikiwezekana makada wetu Shabbiby na Aboud waikodishie serikali kwa bei nzuri yenye faid kwao. Kama kwenye mkutano wa Umoja wa mataifa maraisi walipandishwa kwenye mabasi madogo na hawa kufa basi hata hapa nyumbani inawezekana. kuwapandisha mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, n.k. Hapa pia yataokolewa mabilioni ya shilingi kwani haina maana unakuwa na msafara wa magari 100 na watu kibao wanakula per diem wakati watoto wanakosa huduma ya afya.
5. Kifurushi cha afya toto cha umri wa 1 - 7 kijitegemee kisiunganishwe na kwenye bima ya wazaz kwani umri huu watoto wengi hasa vijijini wanakuwa hawajaanza shulei. Wazazi hawa hawa wanaokula mlo mmoja kwa siku bila kupenda watapata wapi milioni mbili za kukata kifurushi cha bima ya afya cha familia? Kwa nini tunawahukumu na kuwatesa watoto wa taifa hili kwa sababu ya uwezo mdogo wa wazazi wao? Kabla ya hiki kifurshi cha afya toto kuunganishwa na cha wazazi watu wengi walikuwa wanasaidia ndugu, majirani, na hata kwenye jumuiya mbalimbali kuwakatia walau watoto bima za afya kwa sababu ilikuwa na rahisi na iliokoa maisha ya watotot wengi. Lakini sasa nani anaweza kuwasaidia hao watoto ikiwa ni lazima ukate kifurushi cha familia nzima?
6. Serikali ipunguze au iondoe kabisa hafla, sherehe ambazo hazina tija kwa taifa kama sijui sherehe ya kutoa gawio kwa serikali toka mashirika ya uma, sijui sherehe ya kuipongeza Twiga Stars,n.k. Haya yote yanaweza kufanyika bila kufanya sehrehe na zaidi itaokoa muda wa kufanya kazi na kuzalisha mali.
7..........................................
8..........................................
9.........................................
10........................................


Ni mtizamo tu.
 
Back
Top Bottom