Aliyepanga na kuamua sherehe za kuzima mwenge zifanyike kwenye tarehe ya "Nyerere day" ni nani?

Aliyepanga na kuamua sherehe za kuzima mwenge zifanyike kwenye tarehe ya "Nyerere day" ni nani?

Ishu ni kuwa kuzima mwenge kusiingiliane kabisa na siku ya kumbukizi ya baba wa Taifa! Wangezimia huko huko chato lakini kwa tarehe tofàuti!!
Rais alimuongelea Baba wa Taifa pale pale uwanjani na imetosha kumpa heshima. Kumbuka Mama Maria mjane wa mwasisi wa Taifa alikuwepo pale uwanjani. Tupunguze nongwa.
 
Kulalamika mpaka mnajikuta mkionekana kama wajinga fulani hivi. Ungezimiwa Butiama mngesema mbona Chato imesahauliwa!. Mdomo kuongea ni kazi nyepesi sana, fikra ya unachokiongea ndio mtihani huwa mgumu.
wewe ndio mjinga fulani. mimi sijalalamika. Halafu mimi sio fala kama wewe niulizie habari za Chato,chato ni kitu gani kwenye historia ya nchi hii mpaka nihangike nayo. Alipotokea dikteta?
 
Fala ni wewe mkuu, unayepinga kila kitu kinachomhusu Mheshimiwa Rais.
Wewe imba mapambio mimi nipinge,kwani shida nini si tumegawana majukumu tu!ili imbeni mapambio mkitumia akili,maana tu kuna mambo ya hovyo mnayaimbia mapambio sisi tukipinga yanarekebishwa halafu marekebisho yale mnayaimbia mapambio vilevile 😂😂😂😂
 
Wameiwekea hafla kibao zisizoakisi siku yenyewe ili waitokomeze kabisa, watakufa wao lakini hiyo siku itabaki na umuhimu wake vilevile.......
 
Wewe imba mapambio mimi nipinge,kwani shida nini si tumegawana majukumu tu!ili imbeni mapambio mkitumia akili,maana tu kuna mambo ya hovyo mnayaimbia mapambio sisi tukipinga yanarekebishwa halafu marekebisho yale mnayaimbia mapambio vilevile 😂😂😂😂
Maisha ni haya haya mkuu vinginevyo utaumia moyo tu.
 
Mambo mengine yanakera!! Mwenge unaweza kuzimwa siku yoyote!! Kwa nini ipangwe kuzima mwenge siku ya kumbukizi maalumu ya baba wa Taifa?? Kwa nini zipangwe shughuli zingine za kiserikali katika siku ambayo ni Public holiday iliyotengwa kama siku ya kumbukizi ya baba wa Taifa? Dhambi hii ni mbaya!!

Naomba ufanyike uchunguzi tumjue aliyeamua kuifunika siku hii muhimu kwa kuweka shughuli nyingine ya kitaifa ili kulipotosha Taifa juu ya umuhimu wa shughuli hii!! Nahisi kuna watu wanataka kumchafua mama katika hili na wamefanya hivyo kwa makusudi!!
Ifahamike tu kuwa jambo hili limekera!! limeudhi!! Ni tusi kwa watanzania!!

Lazima aliyehusika AWAJIBISHWE!!
Kwani ndio mara ya kwanza mwaka huu kuzima mwenye tar 14 mwezi wa 10.
 
Ni kweli ningetamani kumbukizi za waasisi wetu zibaki kwa ajili yao tu isichanganywe na mambo mengine.
 
Back
Top Bottom