Mwigizaji wa tamthilia nchini, Chado Masta, ameelezea tukio linalosambaa katika mitandao ya kijamii, video inayoonyesha dereva akizongwa na umati wa watu kwa madai ya kumgonga bodaboda, huku mmoja wa watu hao akichukua jiwe na kupasua kioo cha nyuma ya gari.Amesema gari hilo ni la kwake dereva alikuwa akimfuata.
Halikumgonga bodaboda, bali dereva ndiye aliyegongwa, na kwamba bodaboda huyo hakufariki kama ambavyo wengi wanadai. Jalada la kesi hiyo tayari limefunguliwa polisi, huku mtuhumiwa aliyepasua kioo cha gari akishikiliwa na polisi.
“Kwanza anaomba msamaha. Pili, hajui tukio lilikuwa vipi. Yeye alikuwa amembeba mke wake, akasikia kelele kwamba hili gari limeua, kwa hiyo ilibidi na yeye aingilie na akapasua kioo bila kujua kinachoendelea,” amesema Chado Masta.
Pia Soma: Kigoma: Bodaboda wachoma Gari baada ya mwenzao kugongwa, Polisi wawatawanya kwa mabomu ya machozi