Aliyepasua kioo cha gari akidai bodaboda amegongwa akamatwa

Aliyepasua kioo cha gari akidai bodaboda amegongwa akamatwa

Ndiyo sababu watu hawasimami kutoa msaada hata kama wamesababishiwa ajali.

Bodaboda hawajali nani kasababisha ajali,wao wanachuki zao tu na wenye magari na msukumo ukiwa kwenye kupora.

BTW: Alitaka kuonekana shujaa kwa wife hope ni ndoa changa hiyo.😁
 

Mwigizaji wa tamthilia nchini, Chado Masta, ameelezea tukio linalosambaa katika mitandao ya kijamii, video inayoonyesha dereva akizongwa na umati wa watu kwa madai ya kumgonga bodaboda, huku mmoja wa watu hao akichukua jiwe na kupasua kioo cha nyuma ya gari.Amesema gari hilo ni la kwake dereva alikuwa akimfuata.

Halikumgonga bodaboda, bali dereva ndiye aliyegongwa, na kwamba bodaboda huyo hakufariki kama ambavyo wengi wanadai. Jalada la kesi hiyo tayari limefunguliwa polisi, huku mtuhumiwa aliyepasua kioo cha gari akishikiliwa na polisi.

“Kwanza anaomba msamaha. Pili, hajui tukio lilikuwa vipi. Yeye alikuwa amembeba mke wake, akasikia kelele kwamba hili gari limeua, kwa hiyo ilibidi na yeye aingilie na akapasua kioo bila kujua kinachoendelea,” amesema Chado Masta.

Pia Soma: Kigoma: Bodaboda wachoma Gari baada ya mwenzao kugongwa, Polisi wawatawanya kwa mabomu ya machozi
bodaboda ni wadogo zetu na huwa wanatuwaisha tukiwa na matukio ya ghafla lakini wengi wao sijui kwa sababu ya mkumbo au kuvuta mibangi wana tabia za kipumbavu sana.
 
Tena ashukuru amepelekwa police, kwa jinsi nilivyo ona ile video anaenda kutafuta tofali na kupasua kioo cha gari, wallah roho imeniuma sana as if gari ni langu.
Mimi ningemtafuta nimtoe roho kimya kimya ili iwe funzo kwa wengine. WaTz tuna roho za chuki na umasikini tukiona mtu ana maisha mzuri tunataka kumrudisha nyuma.
 
Back
Top Bottom