Aliyepigwa ngumi akiomboleza msiba wa Lowassa kutua Monduli

Jina lake halisi ni Benedict Michael Mwakanyamale, lakini wengi katika Jiji la Arusha hasa eneo la Mbauda wanapenda kumuita Chuma. Huyu ndiye muombolezaji aliyeshambuliwa kwa kupigwa ngumi ya uso na mmoja wa watu walionekana kama ni walinzi waliokuwa wakilinda msafara uliobeba mwili wa Waziri Mkuu mstaafu, hayati Edward Lowassa.

“Yalikuwa ni mapenzi tu kwa baba yetu Lowassa,” haya ni maneno ya Benedict Michael Mwakanyamale (43), aliyeshambuliwa jana kwa kupigwa ngumi wakati akiomboleza msiba wa Waziri Mkuu mstaafu, hayati Edward Lowassa.

“Mimi ni mkazi wa hapa Mbauda na hadi kutoka pale barabarani yalikuwa ni mapenzi tu kwa baba yetu tukitaka kumpa heshima za mwisho baada ya kutupambania sana vijana enzi ya uhai wake. Lakini, badala yake nikaambulia kofi la kwenye taya. Kwa sasa najiandaa kwenda Ngarash kushiriki mazishi yake, ili kumpa heshima anayostahili,” amesema Chuma.

“Yaani kupigwa kwangu hakuzuii kabisa kwenda msibani maana sijaumia hivyo, hainikatishi tamaa na hii ni falsafa yetu makamanda wote majasiri, lazima niende msibani kutoa heshima za mwisho kwa mzee wetu,” ameongeza

Source: Mwananchi
Daaaa! Mie hii ngumi nimeiangalia zaidi ya mara Tano. Yule mlinzi alipeleka ngumi nzito na Jamaa aliyepigwa alidondoka kama anakwenda kukata moto kabisa Hadi yule mlinzi ikabidi ageuke nyuma kuona kama Jamaa kavuta mazima
 
Huyo jamaa Kama Ana umri Wa 43 yrs basi anabidi kujitafakari Sana .

Hiyo ni Kama weak up call ya kujifanyia self-evaluation
 
Jina lake halisi ni Benedict Michael Mwakanyamale, lakini wengi katika Jiji la Arusha hasa eneo la Mbauda wanapenda kumuita Chuma. Huyu ndiye muombolezaji aliyeshambuliwa kwa kupigwa ngumi ya uso na mmoja wa watu walionekana kama ni walinzi waliokuwa wakilinda msafara uliobeba mwili wa Waziri Mkuu mstaafu, hayati Edward Lowassa.

“Yalikuwa ni mapenzi tu kwa baba yetu Lowassa,” haya ni maneno ya Benedict Michael Mwakanyamale (43), aliyeshambuliwa jana kwa kupigwa ngumi wakati akiomboleza msiba wa Waziri Mkuu mstaafu, hayati Edward Lowassa.

“Mimi ni mkazi wa hapa Mbauda na hadi kutoka pale barabarani yalikuwa ni mapenzi tu kwa baba yetu tukitaka kumpa heshima za mwisho baada ya kutupambania sana vijana enzi ya uhai wake. Lakini, badala yake nikaambulia kofi la kwenye taya. Kwa sasa najiandaa kwenda Ngarash kushiriki mazishi yake, ili kumpa heshima anayostahili,” amesema Chuma.

“Yaani kupigwa kwangu hakuzuii kabisa kwenda msibani maana sijaumia hivyo, hainikatishi tamaa na hii ni falsafa yetu makamanda wote majasiri, lazima niende msibani kutoa heshima za mwisho kwa mzee wetu,” ameongeza

Source: Mwananchi
WaTz hawana kazi ndio maana wanajazana kwenye shughuli hizi!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Sio kweli. Ukizingatia Tukio kama hili hutokea kwa nadra sana, watu wengi hupenda kwenda kushuhudia live. Lakini pia nakubaliana na wewe kwani hii nayo huenda ikawa ni fursa.
 
Anaonekana ni mlevi fulani hivi wa kongo. Pumbavu zake akome kusogelea misafara ya wakubwa yenye ulinzi mkali anaweza kuawawa palepale. Misafara ya wakubwa ina itifaki yake, na iwe funzo kwa viherehere wengine wanaopendapenda kusogelea wakubwa bila kujali itifaki
Wakubwa ni akina nani?
 
Umeniangusha port yaani kofi tu umeanguka kama mgomba wa wa matoki kule kk tukuyu.Pole Mwakanyamale mweeh!
 
Aah! Alikuwa hajajiandaa bhana -ameshtukizwa. Mwambie jamaa arudie tena aone kama malafyale ataanguka kizembe hivyo.
 
Jina lake halisi ni Benedict Michael Mwakanyamale, lakini wengi katika Jiji la Arusha hasa eneo la Mbauda wanapenda kumuita Chuma. Huyu ndiye muombolezaji aliyeshambuliwa kwa kupigwa ngumi ya uso na mmoja wa watu walionekana kama ni walinzi waliokuwa wakilinda msafara uliobeba mwili wa Waziri Mkuu mstaafu, hayati Edward Lowassa.

“Yalikuwa ni mapenzi tu kwa baba yetu Lowassa,” haya ni maneno ya Benedict Michael Mwakanyamale (43), aliyeshambuliwa jana kwa kupigwa ngumi wakati akiomboleza msiba wa Waziri Mkuu mstaafu, hayati Edward Lowassa.

“Mimi ni mkazi wa hapa Mbauda na hadi kutoka pale barabarani yalikuwa ni mapenzi tu kwa baba yetu tukitaka kumpa heshima za mwisho baada ya kutupambania sana vijana enzi ya uhai wake. Lakini, badala yake nikaambulia kofi la kwenye taya. Kwa sasa najiandaa kwenda Ngarash kushiriki mazishi yake, ili kumpa heshima anayostahili,” amesema Chuma.

“Yaani kupigwa kwangu hakuzuii kabisa kwenda msibani maana sijaumia hivyo, hainikatishi tamaa na hii ni falsafa yetu makamanda wote majasiri, lazima niende msibani kutoa heshima za mwisho kwa mzee wetu,” ameongeza

Source: Mwananchi
Lakini kasema amesamehe shida yake ilikuwa kuaga tuu..
Kwa ile sura hata kama ni wewe mlinzi usingemuacha
 
Back
Top Bottom