Aliyerekodi tukio jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) apewe maua yake

Aliyerekodi tukio jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) apewe maua yake

Mkuu ina maana haujui kuwa pingu ni bidhaa inayouzwa hata kwa raia?. Nenda maduka ya silaha na vifaa vya ulinzi utazikuta tena bei ya kawaida tu.
Pamoja na hayo ni rare cases kwa mwananchi wa kawaida ambaye hajihusishi na ulinzi na usalama kujinunulia pingu wakati makofuli yamekaa madukani.
Lazima Kuna namna ambayo mnunuzi anadhamiria Kwa ajili ya security purpose! Kwenye Clip rejea neno "gogoni"
 
Aliyerekodi ni mfanyakazi wa hiyo bar ,sijui hoteli. Na ni maagizo alopewa arekodi na boss wake kwa ajili ya matumizi ya baadaye maana hilo tukio alikuanzia hapo,, lilianzia ndani ya uzio wa hiyo hoteli. Kwa hiyo bonge akavutana nao hadi kwenye gari ilopakiwa nyuma ya geti la uani.
Awekewe ulinzi, ikibidi aende nje ya Nchi kutulia kidogo maana KAZI yake ni ya kutukuka.
 
Unavyojiamini sasa, tangu lini CCTV ikatoa Sauti.
Upo Dunia ya wapi mkuu alokwambia CCTV camera hazitoki sauti nani..ingia hapo google utazikuta zinachukua picha na video hata kukiwa na Giza na mvua Totoro na sauti
 
Salaam, Shalom!

Wakati umma wa watz ukilaumu watu waliokuwa wakiangalia tukio lile la ndugu bonge akijaribu kutekwa na wasiojulikana,wenye pingu na silaha za moto.

Kwa jicho la Umakini, yupo shujaa aliyetumia vizuri simu yake na kurekodi tukio Zima tena sauti zikisikika kabisa, hii Ina maana kuwa alikuwa karibu sana na tukio hili.

- Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

Hii ni hatua kubwa huko tuendako maana ujasiri wa wenye Nchi kujilinda utaenda ukiongezeka.

Shujaa huyu hakuogopa KUPIGWA risasi na dreva aliyekuwa ndani ya gari, Abarikiwe huko aliko shujaa wetu.

Na Hadi hivi sasa wasiojulikana wamejulikana katika tukio lile Kwa picha na sura zao, na soon Majina Yao yatakuwa wazi maana wanatoka ndani ya JAMII zetu, tutajua ni Ushimen wa nani, na ni Jirani wa nani,

What comes around, goes around.

Mungu Mbariki mpiga picha.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Na walaaniwe Hawa waovu, na wote tuseme aamin!
Okay
 
Pamoja na hayo ni rare cases kwa mwananchi wa kawaida ambaye hajihusishi na ulinzi na usalama kujinunulia pingu wakati makofuli yamekaa madukani.
Lazima Kuna namna ambayo mnunuzi anadhamiria Kwa ajili ya security purpose! Kwenye Clip rejea neno "gogoni"
Bila kutafuna maneno, moja kwa Moja hao waliohusika na tukio hili ni Mawakala wa TISS, watu wa Abduction Squad. That's why unaona kwamba hata Polisi nao wameshikwa na ganzi katika kushugulikia suala hili.
 
Huyo deo bonge ni nani na anajishugulisha na nini!
Au naye mwanaharakati

Ova
Ndio hapo sasa ushangae
Hii mimi naona ilikuwa shoo ya tiktok, ila imebumburuka
Maana hata huyo mtekwa bonge kaiingia mitini kuogopa soo.....
 
Ndio hapo sasa ushangae
Hii mimi naona ilikuwa shoo ya tiktok, ila imebumburuka
Maana hata huyo mtekwa bonge kaiingia mitini kuogopa soo.....
Kaingia mitini kivipi wakati kwa millard yupo kahojiwa?
 
Bila kutafuna maneno, moja kwa Moja hao waliohusika na tukio hili ni Mawakala wa TISS, watu wa Abduction Squad. That's why unaona kwamba hata Polisi nao wameshikwa na ganzi katika kushugulikia suala hili.
Tatizo ni kwamba wenye akili wamekaa kimya hawachukui hatua ikiwemo kulishitaki jeshi la polisi kwa kushindwa kusimamiwa usalama wa raia na kuishia kuwa na "uchunguzi unaendelea"
 
Hakika Mpiga Picha apewe Maua yake. Jamaa hatimaye wamejulikana
Huyo no 2 anavuta ndumu. Sisi ma FBI wa mtaa tunajua sign za mvutaji.
Hawa jamaa wanatumwa kwa ujira mdogo sana sio hata wa kutoboa maisha. Hivi wanaweza kupewa hata mil 10 kila mtu kweli ? Au ndio njaa chochote wanachukua.
Wafanya biashara wakodishe mafia wawafanye kitu kibaya hawa jamaa.
Nchi yeyu sijui kwa nini haina MAFIA wa mtaa kama South Africa au USA.
 
Back
Top Bottom