Aliyerekodi tukio jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) apewe maua yake

Aliyerekodi tukio jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) apewe maua yake

Ni dhahiri pia kuwa, watekaji ni waoga sana,

Na soon wananchi watatumia chance hivyo vyema,

Watekaji wamekimbia na kuacha pingu,

Ndugu huyu atumie hizo pingu kuwalocate Kwa finger print zao.
Ulishawahi kusikia kisa cha “kesi ya nyani kapelekewa ngedere?” Ndio ulichokiandika hapo mkuu

Yaani unaenda kumshtaku Dula kwa Abdalla
 
Mfano yule smbdy mziba wa kule mikocheni watu wamemchukua tokea 2023 mpaka leo jiii
Nliuliza je anafanyaga clean business wadau wengi walisema hapana jamaa alikuwa mtu wa wash wash .....so inaelekea labda alingia anga za watu wakapita naye mazima

Ova
Kuna mmoja alipotea watu wakasema alikuwa anafanya ma-deal ya madini akakwaruzana na mtu wa ikulu (inaonekana na yeye yuko kwenye hizi deal). Kama nakumbuka vizuri nadhani ni huyu.
 
Kwa hiyo una taka kusema ni watu wa kulipa kisasi,je pingu wametoa wapi?
Pingu zinapatika kama bunduki zinavyopatikana au sare za polisi. Hakuna kitu kisichopatikana mitaani, ni fedha yako tu. Siku hizi kwa sababu nchi ni kama haina uongozi, baadhi ya polisi wamejipa kazi ya kukodiwa ili kulipa kisasi kwa maadui wa mtu anayewakodi. Ukishakuwa na jeshi linalotumika na watawala kufanya uhalifu hili lazima litokee..
 
Oyaaa, huyo sio mtu karekodi na simu yake, ni mfumo wa CCTV ulikuwa ukirekodi na hao askari wa mchongo mabangubangu hawakujua kuwa kuna camera ya CCTV hapo! CCTV inaonyesha tukio limetokea tarehe 11/11/2024. Jumatatu, saa nane mchana

View attachment 3151315
Angalia ile clip anayoingizwa kwenye gari. Ile imerekodiwa na mtu. Hii ndiyo CCTV
 
Nadhani Kuna mahali una tatizo la afya ya akili, na nimekuonya mara nyingi, ukiendelea kwa kinywa na vidole vyako kuendelea kufurahia dhuluma na mateso dhidi ya binadamu, wakati utafika na ukiwa hai utaona matunda yake kwako na familia Yako! Ikiwa hata mtu amedhulumu ambapo (huna hakika) katika nchi inayofuta utawala wa Sheria hastahili kutwezwa utu wake Kwa kiasi hiki. Dhamira Yako itasema na wewe kwa wakati wake sahihi.
Mjinga kama huyuni kumweka kwenye ignore list ili usione michango yake ya kijinga. Mimi nilishamweka zamani sana. Akikosa attention ataacha kuandika. Huwa anaandika kwa sababu anaona kuwa anaweza kuwa-provoke watu na wanajibizana naye.
 
Salaam, Shalom!

Wakati umma wa watz ukilaumu watu waliokuwa wakiangalia tukio lile la ndugu bonge akijaribu kutekwa na wasiojulikana,wenye pingu na silaha za moto.

Kwa jicho la Umakini, yupo shujaa aliyetumia vizuri simu yake na kurekodi tukio Zima tena sauti zikisikika kabisa, hii Ina maana kuwa alikuwa karibu sana na tukio hili.

- Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

Hii ni hatua kubwa huko tuendako maana ujasiri wa wenye Nchi kujilinda utaenda ukiongezeka.

Shujaa huyu hakuogopa KUPIGWA risasi na dreva aliyekuwa ndani ya gari, Abarikiwe huko aliko shujaa wetu.

Na Hadi hivi sasa wasiojulikana wamejulikana katika tukio lile Kwa picha na sura zao, na soon Majina Yao yatakuwa wazi maana wanatoka ndani ya JAMII zetu, tutajua ni Ushimen wa nani, na ni Jirani wa nani,

What comes around, goes around.

Mungu Mbariki mpiga picha.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Na walaaniwe Hawa waovu, na wote tuseme aamin!
Mchukua video ukiangalia vizuri alichukua video akiwa ndani ya nyumba na hata ukiangalia vizuri ni ndani ya jengo lenye madirisha ya Aluminium na huenda yakawa na rangi ya one way black tinted hivyo waliopo nje ni vigumu kumuona aliyepo ndani lakini wa ndani anamuona wa nje clearly
 
Ila mchukua video apewe maua yake ile ni zaidi ya sacrifice,hata ule ulikuwa ni msaada mkubwa nashangaa mapimbi yanayomlaumu wao wangeweza ?wqngekuwa na guts za kuchukua hiyo video?bila hiyo video mngejua kama kunautekaji umefanyika?
 
ALierekodi sidhani kama ni raia wa kawaida Kwa ujasiri wake!

Ni rasmi Kuna pande mbili ndani ya system ambazo hazielewani kwenye kutekeleza mission Fulani fulani!!

Labda kama tukio limekua staged kwa lengo maalum!

Kitu ambacho hakuna afya Kwa ustawi wetu kama taifa!!
Aliyerekodi ni mfanyakazi wa hiyo bar ,sijui hoteli. Na ni maagizo alopewa arekodi na boss wake kwa ajili ya matumizi ya baadaye maana hilo tukio alikuanzia hapo,, lilianzia ndani ya uzio wa hiyo hoteli. Kwa hiyo bonge akavutana nao hadi kwenye gari ilopakiwa nyuma ya geti la uani.
 
Ni ushujaa haswa maana angeweza pigwa hata risasi mzee.
Ila mchukua video apewe maua yake ile ni zaidi ya sacrifice,hata ule ulikuwa ni msaada mkubwa nashangaa mapimbi yanayomlaumu wao wangeweza ?wqngekuwa na guts za kuchukua hiyo video?bila hiyo video mngejua kama kunautekaji umefanyika?
 
Salaam, Shalom!

Wakati umma wa watz ukilaumu watu waliokuwa wakiangalia tukio lile la ndugu bonge akijaribu kutekwa na wasiojulikana,wenye pingu na silaha za moto.

Kwa jicho la Umakini, yupo shujaa aliyetumia vizuri simu yake na kurekodi tukio Zima tena sauti zikisikika kabisa, hii Ina maana kuwa alikuwa karibu sana na tukio hili.

- Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

Hii ni hatua kubwa huko tuendako maana ujasiri wa wenye Nchi kujilinda utaenda ukiongezeka.

Shujaa huyu hakuogopa KUPIGWA risasi na dreva aliyekuwa ndani ya gari, Abarikiwe huko aliko shujaa wetu.

Na Hadi hivi sasa wasiojulikana wamejulikana katika tukio lile Kwa picha na sura zao, na soon Majina Yao yatakuwa wazi maana wanatoka ndani ya JAMII zetu, tutajua ni Ushimen wa nani, na ni Jirani wa nani,

What comes around, goes around.

Mungu Mbariki mpiga picha.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Na walaaniwe Hawa waovu, na wote tuseme aamin!
Inasemekana kulikuwa na CCTV karibu.
 
Ni aibu sana maana familia zao yaani mke watoto, baba , mama, kaka , dada ndugu jamaa na marafiki washajua Hawa jamaa wakiombwa vihela vya matumizi wanawapaga hela za laana...... Za utekaji na uuaji zilizojaa damu. Na hata biblia inasema mshahara wa mbwa usitolewe sadaka...... Sasa huu ni mshahara wa mbwa NOTE: kumbukumbu la torati 23:18

Kum 23:18 SUV​

BHNSUVNenoSRUV
Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili.
Tusubiri report tutaambiwa ni watu wa asili ya kusini mwa Sahara walisikika wakiongea lugha za afrika magharibi.
 
  • Kicheko
Reactions: rr4
relax na upunguze mihemko gentleman,
kwani kwa raia na kwa watu kibao hakuna bastola au bunduki gentleman?

kwani shukuru Kawambwa kipindi fulani video yake ilienda viral sana alitaka kufungwa pingu na raia au askari walipokua wakigombania mpaka?

kwamba kumiliki pingu ni anasa zaidi ya kumiliki bunduki right? Kwani unaishi wap gentleman 🐒
Wenzako enzi za Mchemia walikuwa. na kiburi na jeuri zaidi yako.

Mkuu be humble yana mwisho haya.
 
Hakuna mazoezi pale,

Kimemsaidia urefu na mapana yake.
Kuwakabiri watu watatu waliokwisha kutisha kwa mabundiki na Gari sio jambo dogo. Deo Uzito wake Mungu alimpa kwa makusudi. Umemuokoa.
 
Back
Top Bottom