The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Moja ya mambo yatakayotuchelewesha sana kama taifa, ni kutafuta majibu mepesi kwa maswali magumu. Unaanzaje kuingia gharama ya kumlipa kocha mamilioni ya pesa za kigeni huku ukijua fika kwamba aina ya wachezaji unaozalisha ni hafifu na uhafifu huo hauwezi kuondolewa na Kocha wa Timu ya Taifa?
Hiki kinachofanyika sasa ni kama kujaribu kunenepesha ngo'mbe siku ya mnaada Kwa kumlisha Kwa gharama kubwa sana. Najiuliza sana kwamba inamaana uwezo wetu wa kufikiri kama taifa ndio umeishia hapo?
Niliamini kwamba pale wazarani Kwa sasa pana watu wanaojua kanuni za kuucheza mpira hivyo wangetusaidia kuja na ramani sahihi ya kuelekea mafanikio makubwa ya mpira wetu.
Kocha kulipiwa na serikali sijui kama ni suluhisho la kitu gani? Tatizo letu kubwa kama nchi hatuna mfumo unaozalisha wachezaji mahili, jambo hili ni la wazi kabisa. Badala ya kutibu hilo serikali inaenda kumlipa kocha.!
Huyo kocha mnamleta amkochi nani? Hawa kina Boko, Mzamiru, Mauya, Mwamnyeto Sijui Nyoni, Kakolanya?
Kama serikali Iko serious na mpira wa Tanzania hebu iachane na mambo mepesi kama haya.
Kama serikali yetu inataka utaalamu basi itangaze tenda waje wataalam watakaotutengenezea mfumo wa kutengeneza wachezaji ambao kocha yeyote anaweza kuwakochi na wakapata matokeo kutokana na umahili waliojengewa.
Waletwe wataalam waliobobea huku chini kwenye ngazi za processing and production ya mpira, huku ndiko watatuzalishia wachezaji makocha marefa na watalamu wengine. Hao wataalam watushauri ligi yetu ichezweje na mpangilio mzima wa ligi zetu mbalimbali.
Watashauri pia nini kifanyike kwenye taasisi za elimu ili kuchangia kubadilika Kwa mpira wa Tanzania.
Kwa hapa tulipo timu yetu alitakiwa apewe kocha yeyote tu hata kama yuko field au wa kujitolea maana hatuna cha kupoteza. Huyo mzungu ni kumpa mihela ya bure tu wakati tunajua hatuendi popote.