Aliyetangaza Agosti 23 kuwa siku ya Mapumziko kwa ajili ya Sensa hakufikiria?

Aliyetangaza Agosti 23 kuwa siku ya Mapumziko kwa ajili ya Sensa hakufikiria?

Nasema Uongo Ndugu Zangu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
279
Reaction score
779
Kwa mujibu wa Mama Anne Makinda, Zoezi litaendelea kwa Siku 7, yaani endapo hukufikiwa Leo, utafikiwa siku zijazo, sasa ni nini mantiki ya kupumzika leo?

Tumeambiwa tupumzike ili tupate muda wa kuona picha za viongozi wakihesabiwa?

Haya kesho inafika saa 11 tunaingia barabarani kupambana na foleni kuelekea kazini, tukitoka kazini tunaelekea Bar mpaka saa 6 tunarudi kulala.
 
Itakuwa ni kughafilika na wenge taslimu la tozo. Wameyakanyaga.
 
Ila wamezingua sana. Ni bora jana wangepita wanagawa ile fomu, leo ingekuwa rahisi kuzikusanya na kujaza kidogo. Sasa mi kesho naingia mzigoni
 
MTU akilamba asali hawezi kueleweka .........ngoja mtumbwi WA vibwengo ufike ukingoni watajua hawajui......
 
Nimekaa ndani Hadi saa6 bila kuhesabiwa.

Nikajiuliza tulikaa nyumbani ili iweje wakati zoezi ni endelevu.

Siku ambazo hatutakuwa nyumba itakuwaje.

By the way nchi maskini hatuna mambo mengi ya kufanya nimekasirika Sana.

Mpaka Sasa sijahesabiwa.

Ningekuwa Raisi Sensa ingefanywa na wajumbe wa nyumba kumi mwezi wa 12 siku za weekend.
 
Mapumzimko yaliwahusu viongozi na hatuambiwi, maana hakuna kiongozi ambaye hajahesabiwa leo ila wananchi wengi Sana hawajahesabiwa Leo nikiwemo mimi. Ila kesho, kesho kutwa bado watakuja.
 
Watanzania bwana, yaani mmekaa zenu nyumbani kabisa kusubiri sensa, dah! Hivi mnajua mwisho wa siku wanafanya majumuisho na makadirio tu? Na mbona mko tayari sana kutoa taarifa zenu kwa serikali ambayo kwa muda mrefu imeonekana kutowajali?

Sensa iliyopita wewe imekusaidiaje?
 
Ilikuwa ina maana gani kuifanya siku ya leo kuwa mapumziko..... Kumbe hesabu ni 15% tu kwa siku nchi nzima, ina maana hata wiki haitoshi itabidi waongeze siku. KUMBE MH. MAKINDA ALILIJUA HILI NDIO MAANA ALIKATAA MAPUMZIKO.
 
Yaani ni usanii sanii tu fulani ivi ws kidwanzi
 
mihemko ya viongozi wetu, inaonyesha hakuna aliye serious na kazi hii, hatuna viongozi wenye maono..Tutapata tabu sana yaani, hadi kufika 2025 tutakuwa tumechoka sana🙂
 
Haipo wala hakuna maana. Kesho kama kawaida na sensa inaendelea.
Kuna miaka sikukuu ikiangukia week end ilikuwa inasogezwa ilimradi tu tusifanyekazi. Kukopa tunapenda

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Kwa ajili viongozi wote warudi makwao wakahesabiwe na kupigwa picha kuwekwa mitandaoni tuone majumba na fanicha zao
 
Umekaa ndani angalau hata wanafamilia wamekuonaaa ... kuna wengine wakiondoka saa kumi na moja usubuhi hurejea nyumbani saa tatu/nne usikuuu...

anyway, watu wengi tulijua ni jambo la siku moja wanamaliza, ila kwa hesabu za muda wanaotumi ni ngumuuu
mahojiano ni kati ya dakika 45 - hadi dakika 90 kwa kaya moja
akitembelea kaya 10 = dk 450 - 900 = ni sawa na masaa 7.5 - 15. Endapo ana kaya 20 basi ni siku mbili hadi tatu

kikubwa tujifunze namna nzuri ya kuandaa taarifa mapema kwenye kaya na wao makarani waje kufanya verification (twaweza pewa karatasi na wenye viti wa mtaa na kuzijaza ama kwa walioko kidigitale kutumiwa kupitia simu na kujaza kisha kuja fanya verification)

mie ni muumini wa Civil Registration and Vital Statistics mfumo huu unasaidia sana kupunguza gharama za sensa ama survey nyinginezo zifanywazo kwenye nchi
 
Tatizo Vishkwambi Yaani Mara Vizime Mara Havina Network
 
Back
Top Bottom