Niiwekeje ndugu yangu....Naomba msaada wako..
Ushindi unao endelea kuung`ang`ania.
kwa uwezo wako wa kufikiri na nafasi unayoomba kwa wananchi wa Musoma vijijini unaona heading hiyo inafaa??
watu wamesafiri kuja kukuomba ugombee....wengine wamekupigia simu........hakika wametumia pesa na rasilimali nyngi tu......sasa wewe lini unakwenda kule.........halafu kama wewe ni mzaliwa wa kule kwa nini hukugombea kule mwaka jana?.......una mikakati gani katika kipindi hiki mpaka kufikia 2015?........
kingine wengi hawana access na internet huko...wewe unatangaza rasmi hapa! je umeshawataarifu hao wananchi wako huko musoma vijijini?
la mwisho badilisha avata yako............
Ndugu yangu, wewe umeisha tangaza nia wewe nenda kagombee. kama akijitokeza mwingine basi kura ndani ya chama zitaamua. Hata mimi naweza kutangaza kuwa ninakuja hukohuko msoma vijijini kwani kunashida gani mtu akitangaza nia jamani? Acha CDM iende mbele. Temeke atajitokeza mwingine.
Ndo maana nimejibu kuwa tuombe uzima na afya, nilichofanya mimi ni kukubali ombi je kuna kosa hapo!Nihukumu kama kwa kukubali ombi nimefanya kosa...Hata hivyo nimesema na nitarudia kusema kuwa Chama kikiteua mtu mwingine, sina tatizo, nitashirikiana naye na mimi sitagombea jimbo lolote...
Kumbe utaratibu wa kugombea ubunge kwa Chadema ni rahisi hivi, tunashukuru kwa kutuarifu. Yaani mimi nikiwa nataka kugombea jimbo fulani ninatangaza tu na basi tayari nimekuwa mgombea?
Hata hivyo nina mashaka na uwezo wako wa kujenga hoja. Kama hivyo ulivyoandika hapo juu ndivyo utakavyokuwa unajenga hoja Bungeni iwapo utachaguliwa basi Chadema tumepata seti tupu. Jimbo kuwa nyuma kimaendeleo siyo sababu ya wewe kugombea wakati hakuna ushahidi kwamba wewe ndiyo maendeleo yenyewe na bila mkakati vile utakavyofanya basi kutuletea hayo maendeleo.
Yaani ulichosema kama sapoti ya kugombea kwako ni sawa kabisa na kauli ambazo tumekuwa tukizisikia kwa wagombea wa ccm. Unaleta maendeleo gani, kwa vipi. Uwezo huo wa kuleta maendeleo wewe umeupata wapi? Kwamba umeishi huko siyo hoja, wengi wanaishi huko hadi sasa hivi. Kwamba wazazi wako walizaliwa huko siyo kigezo cha wewe kuwa mbunge wa eneo hilo, wengi wamezaliwa huko na bado hawana vigezo vya kugombea.
Kwanza umekiri kwamba umeshindwa kujibu hoja hapa janvini, na unatumia kigezo hicho eti kututangazia kwamba utagombea. Nashauri ukae kimya kama ulivyosema kwamba ulikaa kimya watu walipokuwa wanahoji uadilifu wako.
Ningependa wote wanaokusudia kugombea nafasi mbali mbali 2015 kujua kwamba it will not be business as usual, we want the best.
Asante ingawa nina wasiwasi na kauli iliyopitwa na wakati ya "nimeombwa nigombee" 2015. Hata hivyo naamini kauli yako hapo juu imeingia kwenye "hansard" na utakuwa mwanifu kwazo ikiwepo kutokuwa msaliti hapo baadaye. Yaliyoandikwa yameandikwa. All the best.
(wewe si ndiyo inasemekana ulilambishwa chapaa na yule jamaa wa Bank M? hahaha! yule jamaa anavaaga kibaragashia chenye mkia kama mzee small!?)
hapa ngoja niwe mwepesi wa kusikia kwanza; nisiwe mwepesi wa kusema,
MKUU TUPO PAMOJA japo naona kuna viwavi wanakula hii hoja yako lakini hiyo sio kitu unawa handle vizuri sana na kwa upole
mimi ni mwana-jimbo tuwasiliane tuone kama naweza kukupa mchango wa mawazo katika kulikomboa jimbo
hachana na hao WA MJINI MJINI