Elections 2010 Aliyetuhumiwa Kumtukana Kikwete sasa Kugombea jimbo la Musoma Vijijini.......

Elections 2010 Aliyetuhumiwa Kumtukana Kikwete sasa Kugombea jimbo la Musoma Vijijini.......

Naona unajisifia kuwa ulimtukana kikwete, huji hiyo ilipunguza kura zako Temeke? Pia hujazungumzia kuwa uligombea ubunge Temeke, huoni hiyo itachanganya watu wadhani ni yule aliyehongwa akampitisha mkono bila kupingwa?
Pia hujasema kura ulizopta Temeke ili tujue nguvu yako kisiasa katika jimbo ambalo hukujiandaa?

Hoyce dadangu,cjifii coz sikumtukana,ila nimesema aliyetuhumiwa...pili hilo la kutukana halikunipunguzia kura TMK kwa sababu halikutokea...tatu nilipata kula elfu28,8 na ushee...nne ni kweli kuna walionichanganya ila mimi nidhani wataona hiyo avata na kujua kuwa huyu ni mwingine..Mwisho nakutakia kila la kheri
 
Mimi naunga mkono miguu na mikono; maana tusibaki kuongelea pembeni mikia chini ya kitovu na mara mtu mwingine anapodiriki kujitokeza hadharani tunaanza kumvunja moyo ili naye afyate mkia kama mbwa koko!

Nilishawahi kusema huko nyuma ili cdm ifike huko vijini kwa urahisi ni lazima tupate watu wenye nia ya kugombea maeneo yale ili waanze kazi ya kukijenga chama na kuweka mahusiano mazuri na watu wale.
Mabo ya kupeleka sura zetu 2014 eti tunataka kura haitaKuwa. Mtu anayetaka kugombea ni lazima awekeze siyo chini ya miaka mitatu akifanya kazi ya kukijenga chama kwa kuwa na watu wenye ushawishi kila kona ya jimbo na wanachama waaminifu watakao kitanganza chama

Mimi nashauri chadema iwaruhusu watu ambao wana nia ya kugombea waanzenze leo kazi hiyo na sikusubiri utaratibu wa chama kama wanamagamba. Lazima cdm ilichukulia swala la kugombea ni haki ya msingi na kila mtu anaruhusiwa ni kazi yake kwenda kujiuza na kukubalika kwa wananch hiyo siyo kazi ya uongozi wa cdm.

Kama kuna watu zaidi ya mmoja wanataka kugombea jimbo moja iwe ni kazi yao kujiuza kwa wananchi mpaka wakati wauteuzi utakapo fika.
Mimi naamini mtu atakeye fanikiwa kukijenga chama pia atakuwa amekubalika na hakutakuwa na sababu ya kutompitisha kugombea ili hali amekiletea faida pia chama.
Pia itakuwa rahisi kwa watu kuwachuja hawa wagombea maana watakuwa wakishirikiana nao kwa muda mrefu zaidi kuliko ilivyo sasa mtu anaweza kutumia lambalamba kwa muda mfupi akwateka watu. Lakini hawezi kutoa lambalamba kwa muda wa miaka minne mfululizo hata kama yeye ni tajiri atachoka tu.

Tukumbuke mtu mwenye nia yakuwaletea watu mabadiliko ya kweli na sikupata jimbo, hachoki hata akishindwa bado ataendelea kushirikiana na hawa watu mpaka watakubaliana naye maana ataendelea kutimiza ahadi zake hatakama ameshindwa.

Once again mimi na unga mkono na kama kuna mtu mwingine anataka pia kupambana na huyu brother ni ruksa ajitokeze pia wakati huu maana mwisho wa siku ni wananchi ndo wanaamua ni yupi anawafaa na siyo uongozi wa cdm.

Haya ni mshambulizi mazuri kwa wana magamba kabla hawajaanza kuchakachua ni lazima wajue kabisa 2015 cdm siyo tena mambo ya kuzima moto kama vyama vya akina DOVUTWA.


Mh. Ngonini...Nashukuru kwa mchango wako....Ubarikiwe sana...
 
Sijuhi ilikuwaje lakn uenda unapandwa na jazba bila msingi kama pale Temeke mtu anakudrive tu kidogo unapanda mori,unakuwa mkali,unatoa lugha mbaya (easy to tease) ,ni lazma ujifunze kuvumilia na kujenga hoja,jibu hoja kwa hoja,hyo ndo siasa ya CDM

lakini pia sie hatuhtaji kujua hayo sahv,ww nenda jimboni piga kazi,simika chama,buni miradi katika jamii,shiriki kutatua matatizo ya wananchi then ndo uje hapa jamvini utwambie umeishafanya nini... kwa njia hyo you can defeat your opponent,otherwise sisi hapa ni washauri tu kazi ni kwako,take t!

Nashukuru Mkuu....
 
Mh. Ivuga, nashukuru sana kwa mchango wako coz uko na uhuru wa kusema chochote unachoweza bila kuvunja shria za nchi...Na hapa kusema ukweli haujavunja shria yeyote...Labda nikusahihishe kuwa sio Kigoma ila ni Musoma Vijijini...Ubarikiwe sana...
ndio huko huko
 
mkuu kwa nini ulimtukana Rais wao wa ccm?

Mkuu me sikumtukana na kwa kuwa hilinilikwishalitolea ufafanuzi humu humu, basi wewe search 'asiyefunzwa na mamaye ni tusi' hapo utapata majibu ya swali lako kaka...asante na usiku mwema...
 
Mkuu me sikumtukana na kwa kuwa hilinilikwishalitolea ufafanuzi humu humu, basi wewe search 'asiyefunzwa na mamaye ni tusi' hapo utapata majibu ya swali lako kaka...asante na usiku mwema...

Dah kamanda nakukubali...manake ile siku Dk Dlaa alikuachia maik tu usalimie...aagh palikuwa hapatoshi, nayakumbuka sana hayo maneno ''asiyefunzwa na *****"...duh we kweli ni noma,ulivyokuwa mkali siku ile,nimeshangaa hapa JF umekuwa mpole kweli. Isitoshe kipindi cha uchaguzi ulikuwa mrefu mrefu na mwembamba laakini kwenye picha yako inaoneka ni mfupi na mnene, au ndo mambo ya ruzuku??

bt all the best mkuu!!
 
Mheshimiwa Speaker, nashukuru kwa maswali yako ila sidhani kama ni busara kuyajibu sasa...hebu ngoja nikijenge CHAMA kwanza kwa kushirikiana na wananchi pamoja na wana CDM. Na pia nashukuru kwa daut zako coz kama mwanadamu una haki ya ku-dought na nimezipenda sana na wakati ukifika,WanaCDM wakanipa ridhaa na Tume ikaniteua nitakuprov wrong na hata kama sikuteuliwa mimi,akateuliwa mwanaCDM mwingine,nitafanya naye kazi bega kwa bega ili kukuprov wrong juu ya imani yako kwa Mkono...Naomba kuwasilisha mkuu..

Naomba niwe hai mda huo ili nione utanunuliwa kwa bei gani na mkono
 
Dah kamanda nakukubali...manake ile siku Dk Dlaa alikuachia maik tu usalimie...aagh palikuwa hapatoshi, nayakumbuka sana hayo maneno ''asiyefunzwa na *****"...duh we kweli ni noma,ulivyokuwa mkali siku ile,nimeshangaa hapa JF umekuwa mpole kweli. Isitoshe kipindi cha uchaguzi ulikuwa mrefu mrefu na mwembamba laakini kwenye picha yako inaoneka ni mfupi na mnene, au ndo mambo ya ruzuku??

bt all the best mkuu!!

Hahaha...Mkuu Sizinga, nanifurahisha sana kaka...mbona hiyo picha niliipiga hata kabla sijasimama pale mwembeyanga na ndo niitumia kama mabango yangu kwenye kampeni.Hivyo kama naonekana mnene na mfupi basi uje ndo maumbile yangu hayo na kama pale mwembeyanga uliniona mref mwembamba basi uje kampeni ndo zilinikondesha...Kwa majib hayo ina maana suala la ruzuku hapo halipo kaka...Ila umenifurahisa sana...Kuhusu ukali,mimi sijui kama ni mkali ila inawezekana but sina hakika kabisa, sasa siku ile pale mwembeyanga, hiyo ndo aina yangu ya uzungumzaji ninapokuwa kwenye majukwaa ya nje kisiasa.Unasema hapa JF nimekuwa mpole kweli...hahahahaha...pia hili linawezekana ila hakika sana coz hii ndo aina yangu ya uzungumzaji kwa Great Thinkers...mkubwa mimi nakushukur na ninakutakia kila la kheri...
 
Naomba niwe hai mda huo ili nione utanunuliwa kwa bei gani na mkono

Mkuu, tuombe uzima..Inshallah Mwenyezi Mungu atatujalia uhai na utashuhudia jinsi mkono atakavyogalagazwa na pesa zake na jimbo linaenda CDM....Afu kuna mtu kanipigia simu na kuniambia kuwa Mkono anaweza asigombee au kwakuwa kwa tamko la rais Musoma vijijini imegawanywa kuwa wilaya mbili ya Butiama na Musoma (V) Basi huenda akagombea wilaya ya Bitiama...Ila kama nilivyosema nimeambiwa kwa simu so sina hakika na hivyo sitilii maanani hiyo taarifa...Ila mimi ningependa CCM wamteue yey (Mkono) na CDM waniteuwe mimi..Kaka hapo ngoma ingekuwa tamu sana..Hata hivyo tusiyajadili haya na tusubiri wakati ufike na vyama vyetu respectively vituteue na NEC nayo ituteue afu tuingie uwanjani...Mwisho, nakombea sana ili Mwenyezi Mungu akupe UHAI na AFYA JEMA ili uyashuhudie matendo makuu...itakuwa ni historia ya aina yake na kama ni msomaji wa vitabu vitakatifu basi kesi yangu na mkono itakuwa kama kesi ya Daudi na Goliath.....Kaka nisiseme sana...
 
Dadangu Judith,

Inawezekana ukawa umenichanganya...sijawahi kuwa CCM-CCK-CDM-CCM-CDM...Ila ni ukweli usiopingika kuwa nilikuwa CCM na nikatoka nikawa CCJ ambayo nilikuwa mmoja wa viongozi wake wajuu kitaifa. Hata hivyo CCJ ilifanyiwa mizengwe na hivyo kutokuqualify kupata usajili..Baada ya hapo, tulitoa tamko la kuunganisha nguvu na CDM na hivyo ndivyo ilivyo so sijawahi kutoka tena CDM tangia hapo....Nimekuwa na msimamo huo na sitarajii wala sitegemei kuubadili. Sasa CCK ni baadhi ya wale ambao hawakwenda CDM, nasikia kwa ushauri wa mzee Tendwa wakaamua kuanzisha Chama kingine kinachoitwa CCK....Sasa sijui kama nimekujibu ipasavyo dadangu...

umenijibu vizuri kaka, ubarikiwe sana.

katika mambo ya siasa, ni vizuri ukawa unajua unasimamia nini. kama ulitoka ccm, ukaanzisha ccj maana hukuona chama chochote cha maana na chenye uelekeo unaouamini katika kupigania maendeleo ya wananchi na ikiwemo hii chadema uliyolazimika kuingia baada ya chama chako kushindwa kupata usajili. hata tendwa si wa kulaumiwa sana kwa sababu ilionekana shida yenu ilikuwa usajili tu kisha mgawane mmoja agombee urais na wengine ubunge basi, kwa hiyo watanzania wengi waliona kuwa tendwa aliwasaidia kuwaonyesha nyie ni watu wa aina gani.

huu uzuri wa chadema unaouona sasa ina maana wakati wa ccj hukuuona?

sitaki kuwa hakimu wa dhamira yako na ya wenzako, ila sio siri, "nakuogopa" sana

nakutakia kila la heri ila kwa kweli hujaipata bado kura yangu ikitokea uchaguzi unaitishwa sasa hivi.

uwe na amani na Mungu akubariki
 
umenijibu vizuri kaka, ubarikiwe sana.

katika mambo ya siasa, ni vizuri ukawa unajua unasimamia nini. kama ulitoka ccm, ukaanzisha ccj maana hukuona chama chochote cha maana na chenye uelekeo unaouamini katika kupigania maendeleo ya wananchi na ikiwemo hii chadema uliyolazimika kuingia baada ya chama chako kushindwa kupata usajili. hata tendwa si wa kulaumiwa sana kwa sababu ilionekana shida yenu ilikuwa usajili tu kisha mgawane mmoja agombee urais na wengine ubunge basi, kwa hiyo watanzania wengi waliona kuwa tendwa aliwasaidia kuwaonyesha nyie ni watu wa aina gani.

huu uzuri wa chadema unaouona sasa ina maana wakati wa ccj hukuuona?

sitaki kuwa hakimu wa dhamira yako na ya wenzako, ila sio siri, "nakuogopa" sana

nakutakia kila la heri ila kwa kweli hujaipata bado kura yangu ikitokea uchaguzi unaitishwa sasa hivi.

uwe na amani na Mungu akubariki

Dadaangu Judith, una haki ya kuniogopa na wala sina kinyongo na wewe kwa kuniogopa...dada Judy, katika maelezo yangu sikusema kuwa mimi ni mwanzilishi wa CCJ,kwamba nilitoka CCM na kuanzisha CCJ, ila nimesema nilikuwa mmoja wa viongozi wa juu kitaifa...Ni hivi dadangu,kila jambo ambalo mtu analianzisha anakuwa na strategy yake..Strategy ndo inayomuwezesha kusonga mbele coz inakila kitu...Na ni strategy hiyo ndo ilitufanya kwanza tuwe CCJ afu baadaye tushirikiane na hatimaye kujiunga na CDM. Sasa nisingependa Kuwataja waanzilishi wa CCJ coz wengine ni watu wakubwa sana katika serikali yetu hii...Haikuwa rahisi kwao kutoka na kuingia CDM japo waliishaiona CDM ndo chama makini. Hata hivyo siku tunaingia CDM, tulitoa tamko ambalo tulielezea ni kwa nini CCJ ilianzishwa na tukawambia watanzania kuwa hata wakati tuna push usajili already tuliishaanza mazungumzo na CDM juu na namna ya kushirikiana. So kunyimwa kwetu usajili hakuku2sh2a coz taarifa zote tulikuwa nazo maana waanzilishi wa CCJ walikua ni zaid ya wabunge 60 wa CCM na viongozi wengine wa CCM na Serikali yake akiwamo na mpendazoe ambaye yeye aliamua kujitoa muhanga mapema na wengine wakaogopa. Na ndiyo maana CCJ ilikuwa tishio kwa mda mfupi japo dadangu hilo wewe hujaliona. na kama una kumbukumbu, karibia vyama vyote vilituponda na kutukebehi lakini CDM walikuwa kimya walitusapoti katika kila move tuliyokuwa tunaiendea, walitushauri kwa kila kitu coz wao wamekuwepo kwa siasa za vyama vingi toka mfumo huo unarejeshwa Tz toka 92, na walijua CCJ ni wapambanaji wenzao.So uzuri wa CDM sijauona sasa nimeuona toka mwanzo na ndo maana tulishirikiana nao toka mwanzo...Unaweza kurajea hotuba ya Mh. Mbowe siku anatukabidhi kadi za CDM utauona ukweli wa hiki ninachokisema. Dada Judith, mimi sikulazimishi wewe unipe kura yako kwani una uhuru wa kumchagua mtu unayempenda...hata uchanguzi uliopita ulimpigia mtu unayempenda na kutokana na mwelekeo wa komenti zako inaonyesha wazi kuwa mimi hukunipigia, lakini pia kuna watu walionipigia ambao waliona mimi ninawafaa na hivyo kupata kura elf28.8 na ushee sina kumbukumbu nzuri unaweza kuangalia kwa tovuti ya NEC...Huu kwetu CDM ni ushindi mkubwa sana kwani uchaguzi wa mwaka 2005, mgombea ubunge wa CDM Temeke alipa kura 4000 tu...So ni hatua tumepia na ukweli nawashukuru wote walionipigia kura japo ndo hivyo sikushinda na waswahili wanasema asiyekubali kushindwa si mshindani...so tunajipanga na naamini 2015 TMK itenda CDM... hata Kikwete sio wote waliompigia kura kama mimi lakini ni rais sasa. Kura yako ni ya muhimu sana kwangu ila ndo hivyo, ushanikataa sasa mimi maskini wa watu nitafanya nini...sina cha kufanya zaid ya kumwomba Mwenyezi Mungu abadilishe fikra zako ili siku moja niipate kura yako coz ni ya MUHIMU SANA...dadangu Judith, natamani sana nikushawishi ili usiniogope kwani mimi ni binadamu wa kawaida, na kuwa kwangu upinzani si dhambi..upinzani ni serikali mbadala kesho CDM,CUF ,TLP,UDP au NCCR tutakuwa chama tawala, je na sisi twachukie wapinzani...Hapana hatuwezi fanya hivyo, na kama kuna watu wanafanya hivyo; NIMAKOSA. Hebu tutofautiane kwenye majukwaa lakini tuudumishe undugu wetu na mshikamano tulioasisiwa na wazee wetu...Japo unaniogopa lakini mimi nakupenda,nakuheshimu na nakuthamini bila kujali rangi yako, kabila lako, dini yako au itikadi yako ya kisiasa...
Mwisho nakutakia mafaniko mema katika shughuli zako za kila siku...Ubarikiwe na Bwana na nakuombea maisha marefu na afya njema...
 
Back
Top Bottom